Utawala wa Kizayuni wa Israel umekiri juu ya nguvu n uwezo wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon
Duru za Wazayuni zinaripoti kwamba, jeshi la Israel limekiri bayana kwamba, uwezo wake wa kijeshi wa anga hauwezi kukabiliana na makombora ya wanamapambano wa Hizbullah ya Lebanon.
Vyombo vya habari vya Israel navyo vimekiri kuwa, jeshi la Israel halina uwezo kamili wa kijeshi wa kukabiliana kivita na Hizbullah.
Sayyid Hassan Nasrullah Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Hizbullah ya Lebanon ametangaza mara kadhaa kwamba, endapo Israel itathubutu tena kuishambulia ardhi ya Lebanon itakabiliwa na pigo kubwa na zito zaidi.
Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel lilishindwa na Harakati ya Mapambano ya Hizbullah ya Lebanon katika mashambulio yake ya siku 33 dhidi ya Lebanon mwaka 2006. Kufuatia kipigo hicho, Israel ilipata hasara kubwa na kulazimika kuondoka kusini mwa Lebanon.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: