Watu kadhaa wamejeruhiwa baada ya kutokea shambulio la watu wenye silaha mjini Bujumbura, Burundi.
Shirika la habari la Xinhua limemnukuu Mwese Nkurunziza, naibu wa
msemaji wa polisi ya Burundi akisema jana kuwa, wanajeshi wanne wa nchi
hiyo wamejeruhiwa. Mmoja wa wanajeshi hao waliojeruhiwa ana cheo cha
Kepteni. Wanajeshi hao walishambuliwa kwa guruneti wakati wakipiga doria
katika eneo la Musaga, kusini mwa Bujumbura.
Kwa mujibu wa naibu huyo wa msemaji wa polisi wa Burundi, wanajeshi
wengine waliokuwepo katika eneo hilo waliwafyatuliana risasi na
washambuliaji. Hata hivyo amesema, hakuna mtu yeyote aliyeuawa kwenye
ufyatulianaji risasi huo.
Musaga ni moja ya maeneo yenye wapinzani wengi wa serikali ya Rais Pierre Nkurunziza.
Eneo hilo ndilo lililoshuhudia upinzani mkubwa wa kushiriki
Nkurunziza katika uchaguzi wa rais wa mwezi Aprili 2015 kwa mara ya tatu
mfululizo.
Zaidi ya watu 400 wameripotiwa kuuawa hadi hivi sasa na karibu watu
laki mbili na 40 elfu wamekuwa wakimbizi tangu Burundi ilipotumbukia
kwenye machafuko yaliyotokana na Rais Nkurunziza kuamua kugombea tena
urais nchini humo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: