WAFUASI WA KABILA WASHINDA UCHAGUZI MAJIMBONI DRC

Wafuasi wa Kabila washinda uchaguzi majimboni DRC
Wafuasi wa Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamepata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa majimbo ambapo kati ya majimbo 19 wamepata ushindi katika majimbo 14.
Shirika la habari la Reuters limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, tume ya uchaguzi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imetangaza kuwa, viti vya majimbo hayo matano yaliyosalia vimechukuliwa na wagombea huru, na uchaguzi wa jimbo moja umeingia katika duru ya pili.
Wapinzani wanalalamikia matokeo hayo wakisema kuwa wafuasi wa Rais Joseph Kabila wamepata ushindi mkubwa katika uchaguzi huo kutokana na nguvu za vyombo vya dola na uchakachuaji wa matokeo.
Matokeo ya uchaguzi huo yamemuongezea nguvu Rais Kabila na kutoa uwezekano wa kuendelea urais wake kwa kipindi kingine hasa kwa kuzingatia kuwa wafuasi wake wanaendesha kampeni za kubadilisha katiba ili imruhusu kuendelea kugombea urais katika uchaguzi ujao.

0 comments: