- L. P. 3021,
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mabasi yaendayo kasi (DART) yataanza
kufanyiwa majaribio ndani wiki moja kuanzia sasa ili madereva waanze
kuzoea njia na taa za kuongozea magari.
“Wataanza na mabasi kati ya 30 –
50 ambayo yatapita kwenye njia zote za mradi huo. Zoezi hilo litafanyika
ili watumiaji wengine wakiwemo waendesha daladala, bodaboda na watembea
kwa miguu waweze kutambua kuwa njia ya mabasi yaendayo kasi si ya kwao,
hivyo waanze kuzoea,” alisema.
Ametoa kauli hiyo leo mchana
(Jumanne, Machi 22, 2016) wakati alipofanya ziara ya ghafla katika Soko
la Kimataifa la Samaki la Feri iliyokuwa na lengo la kuangalia mfumo wa
majiko ya gesi sokoni hapo na kukagua ujenzi wa ukuta unaotenganisha
soko hilo na mabasi yaendayo kasi.
Waziri Mkuu ambaye ametembelea
soko hilo kuanzia saa 5:10 hadi saa 5:54, alitoa jibu hilo wakati
akijibu maombi ya mfanyabiashara mmoja, Bw. Sharifu Ramadhani ambaye
alisema wanatumia fedha nyingi kwa ajili ya usafiri kwa vile mabasi
mengi yanaishia Mnazi Mmoja. “Mabasi yanaishia Mnazi Mmoja na huku ni
mbali kwa hiyo tunalazimika kutembea kwa miguu kwa sababu kukodi taxi ni
gharama kubwa,” alisema.
Akifafanua kuhusu hatua
iliyofikiwa kwenye utekelezaji wa mradi huo, Waziri Mkuu alisema: “Hivi
sasa wanakamilisha ufungaji wa mitambo ya kukatia tiketi ambapo abiria
atakuwa na kadi kama za benki ambayo anaijaza fedha halafu anapita
kwenye mashine, kiasi cha nauli kinakatwa halafu anaingia kwenye basi,
hakutakuwa na muda wa kukata tiketi.”
Alisema tatizo la usafiri kwa wafanyabiasha wa feri litakwisha hivi karibuni baada ya mabasi hayo kuanza.
IMETOLEWA NA: OFISI YA WAZIRI MKUU
2 MTAA WA MAGOGONI,
11410 DAR ES SALAAM
JUMANNE, MACHI 22, 2016.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: