Posted by
khamisimussa77@gmail.com
at
3:06 PM
Katibu
Mkuu wa Ikulu Peter Ilomo akimkabidhi funguo za gari jipya la wagonjwa
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete lililotolewa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya shughuli ya
kubebea wagonjwa katika hospitali ya Wilaya ya Chalinze. Tukio hilo
lilifanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mbunge
wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akipokea na kuangalia nyaraka za gari
hilo la kubebea wagonjwa kutoka kwa Katibu Mkuu wa Ikulu Peter Ilomo.
Mbunge
wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akishukuru mara baada ya kukabidhiwa gari
la kubebea Wagonjwa na Katibu Mkuu wa Ikulu Peter Ilomo kwa niaba ya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe
Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mbunge
wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akiwasha gari jipya la Wagonjwa
lililotolewa na na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli kwa ajili ya kubebea wagonjwa katika hospitali ya Wilaya
ya Chalinze.
Sehemu ya Ndani ya gari hilo kama inavyoonekana .
Mbunge
wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akiendesha gari hilo la wagonjwa
lililotolewa na na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli kwa ajili ya kubebea wagonjwa katika hospitali ya Wilaya
ya Chalinze.
Gari
jipya la Wagonjwa lililotolewa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya Hospitali ya Wilaya ya
Chalinze kama linavyoonekana kwa nyuma.
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akifurahia mara baada ya kukabidhiwa Gari hilo la Wagonjwa.
Mbunge
wa Chalinze Ridhiwani Kikwete akishukuru mara baada ya kukabidhiwa gari
na Katibu Mkuu Ikulu Peter Ilomo kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es
Salaam. Wengine katika picha ni Afisa Usafirishaji wa Ikulu Athuman
Natepe wakwanza kushoto, Mwenyekiti wa Wilaya ya Chalinze Said Omar
Zikatimu wapili kutoka kulia na Dkt. Nasoro Ally Matuzya wakwanza kulia.
Picha na IKULU
Rais
wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli
amekabidhi gari la kubebea wagonjwa kwa hosipitali ya wilaya ya
Chalinze, Ikiwa ni utekelezaji wa ilani na ahadi ya uchaguzi ya Chama
Cha Mapinduzi CCM kwa wananchi ikiwa ni pamoja na wa jimbo la Chalinze.
Gari hilo la kubebea wagonjwa limekabidhiwa kwa niaba ya Rais, na Katibu
Mkuu Ikulu Peter Ilomo kwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mheshimiwa
Ridhiwani Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi gari hilo, Katibu Mkuu Ikulu Ndugu
Peter Ilomo amesema gari hilo limetolewa na Mheshimiwa Rais kwa
hosipitali hiyo ikiwa ni kuitikia wito na utekelezaji wa ilani na ahadi
ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi CCM ya kuboresha huduma ya afya kwa
wananchi wake kote nchini. Aidha, Ndugu Ilomo amewaomba viongozi wa
jimbo la Chalinze kulitumia gari hilo kwa matumizi yaliyokusudiwa ya
kuwahudumia wananchi wa eneo hilo.
Akipokea gari hilo kwa niaba ya wananchi wa jimbo na Wilaya ya
Chalinze, Mbunge wa jimbo la Chalinze Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete
amemshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa msaada huo
na kuahidi kulitumia gari hilo kwa malengo yaliyokusudiwa, na kusema
kuwa, utendaji kazi wa Rais Magufuli umekuwa ukiungwa mkono na wananchi
wa kada mbalimbali na kuwaomba watanzania kuzidi kumuombea kwa Mungu.
Kwa upande wake Dakta Nasoro Ally Matuzya, amesema gari hilo limekuja
kwa wakati muafaka kwa kuwa umezingatia utekelezaji wa malengo ya
Milenia hususan lengo namba nne linalosisitiza kupunguza vifo vya mama
wajawazito na watoto chini ya miaka mitano
Naye Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Chalinze Ndugu Saidi Omar
Zikatimu amesema gari hilo la kubebea wagonjwa litakuwa msaada mkubwa
kwa wananchi wa jimbo hilo la Chalinze hususan katika kusaidia kutoa
wagonjwa ambao wako katika maeneo ya vijijini wilayani humo na
kuwafikisha katika hospitali ya Chalinze na hivyo kunusuru maisha yao
kwa kupata huduma za afya kwa haraka.
Mbali na Wilaya ya Chalinze kupata msaada wa gari hilo la kubebea
wagonjwa, tayari magari mengine mawili ya kubebea wagonjwa
yameshakabidhiwa katika vituo vya afya vya Kiroka na Kisemu mkoani
Morogoro.
Hospitali mpya ya Wilaya ya Chalinze imepanda hadhi kutoka kituo cha
Msoga ambayo ilikuwa haina gari la kubebea wagonjwa na hivyo kufanya
usafirishaji wa wagonjwa kutoka hospitali hiyo hadi hospitali ya rufaa
ya Mkoa wa Pwani ya Tumbi au kutoka maeneo ya vijijini kuwa mgumu.
18 Machi 2016.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: