Posted by
khamisimussa77@gmail.com
at
1:05 PM
Ni
moja ya taarifa ambazo nimezisikia sana kwa wiki hii hapa Nairobi
inayosema kuhusu Mchungaji mmoja maarufu kwenye mji huu kwa jina la
Geofrey Maingi wa kanisa la Redeemed Gospel alikutwa amefariki kwenye
chumba cha kulala cha mama ambae ni muumini wake huko Buruburu.
Vyombo mbalimbali vya
Kenya vimeripoti kwamba kwamba marehemu aliekua na umri wa miaka 70,
alikua amekwenda nyumbani kwa mama ambae ni muumini wake kwa lengo la
kumfanyia maombi lakini akafariki wakati maombi yakiendele
Mwili wa mchungaji ukiwa unatolewa kweye chumba alichofia.
Mama huyu ambae amesema
ana umri wa miaka 40, amewaambia Polisi kwamba Marehemu alizirai wakati
wakiwa kwenye maombi na kwamba hawakuwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi
japo majirani wanasema wawili hawa walikua wapenzi.
Baadhi ya mashuhuda
wanasema Mchungaji huyu amekua na kawaida ya kwenda kwenye nyumba ya
huyu mama kila weekend, na mara nyingi amekua akienda Jumamosi na
kuondoka Jumatatu. Mke wa Marehemu alizimia baada ya kupata taarifa za
kifo cha mume wake ambacho kimetokea wiki mbili baada ya mchungaji
mwingine wa Embu kufumaniwa na mke wa mtu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: