Posted by
khamisimussa77@gmail.com
at
1:08 PM
Na Stori: Mayasa Mariwata na Shani Ramadhani
Mganga aliyejita-mbulisha
kwa jina moja la Kimweri ameibuka na madai mazito kuwa ndiye
aliyemng’arisha staa wa kike wa Bongo Fleva, Meninah Abdukareem ‘Meninah
La diva’ hivyo kutoa siri nzito ambayo wengi hawakuijua.
Staa wa kike wa Bongo Fleva, Meninah Abdukareem ‘Meninah La diva’.
Kwa
mujibu wa chanzo makini, mganga huyo amekuwa akimfanyia ndumba msanii
huyo ili arudiane na aliyekuwa mwandani wake, Nasibu Abdul ‘Diamond
Platinum’.
Kwa
mujibu wa chanzo hicho, mganga huyo amekuwa akidai kwamba, huwa msanii
huyo anatinga nyumbani kwake maeneo ya Mwananyamala-Komakoma jijini Dar
kisha kumlilia shida yake akimtaka afanye juu chini kuhakikisha
anamrudisha Diamond mikononi mwake.
Meninah Abdukareem ‘Meninah La diva’ akipozi.
Baada
ya kukisikia chanzo hicho, waandishi wetu walikwenda nyumbani kwa
mganga huyo na walipomuuliza ishu hiyo alikiri Meninah kufika kwake ili
kufanyiwa ndumba arudiane na Diamond.
“Yule
msanii anayeitwa Meninah ambaye habari zilivuma kuwa anatoka na Diamond
na kukanusha, huwa anakuja hapa kufuata tiba na kikubwa anachokitaka
anataka nimvute Diamond ili warudiane,” alisema.
Meninah alipoulizwa kuhusu madai hayo aliruka kimanga na kudai hakuwahi kuwa na uhusiano na Diamond na wala hamjui mganga huyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: