Posted by
khamisimussa77@gmail.com
at
8:50 PM
Dereva
wa bodaboda mjini Moshi amepata fursa ya kukutana na msanii wa
kimataifa siku ya fainali za Serengeti fiesta zitakazo fanyika Oktoba 18
mwaka huu jijini Dar es Salaam baada ya kushinda katika shindano la “ni
sheedah moment”linalofanyika katika mitandao ya kijamii ya Facebook na
twitter.
Akizungumzia
kushiriki kwake katika shindano hilo ambapo mshiriki hutuma picha
katika uwanja wa twitter na facebook, Bwana Nikolaus alisema kwamba
baada ya kusikia tangazo redioni, alitumia fursa hiyo kutuma picha yake
akifurahia bia ya Serengeti Premium lager na kuituma katika twitter.
Masaa
kadhaa baadae alipigiwa simu na wahusika kutoka Serengeti breweries na
kumtangaza kama mshindi. “Sikuamini…nilishangilia kwa furaha sana hasa
ukuzingatia kwamba imekuwa ndoto yangu ya muda mrefu kukutana na msaanii
toka nje ya nchi…ninatamani siku ifike mapema,” alisema Nikolaus.
“Hii
ni mara yangu ya kwanza kushiriki shindano hili, na ninaishukuru sana
kampuni ya Serengeti kwa kunipa fursa ya kwenda Dar es saaam kushuhudia
fainali za Serengeti Fiesta 2014 ” aliongeza Bwana Nikolaus.
Mshindi
huyo alitoa wito kwa vijana wenzake kushiriki katika shindano hili ili
nao wapate fursa ya kwenda kushuhudia fainali za Serengeti fiesta.
Shindano
la ni sheedah moment linaendeshwa na kampuni ya Push Mobile Media
Limited katika mitandao ya kijamii facebook na twitter, ambapo kwenye
Facebook mshiriki atumie link hapa chini kuweza kujisajli kwenye
shindanohttps://www.facebook.com/serengetipremiumlager/app_739696419428430 na kwa wale wa twitter mshiriki atume picha kwenye ukurasa wake yenye hashtag #nisheedahmoment
Washindi
watazawadiwa zawadi mbalimbali ikiwemo bidhaaa mbalimbali za Serengeti,
baadhi ya washindi hawa pia watapata fursa ya kushinda tiketi ya
kuhudhuria fainali za Serengeti fiesta mjini Dar-es salaam ambapo msanii
wa kimataifa atatumbuiza.
Baada
ya Moshi, joto la Serengeti fiesta linaendelea kusambaa katika mikoa
mbalimbali hapa nchini na baadae kumalizia jijini Dar es salaam.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: