RAIS KIKWETE NA WENZAKE 14 KUPANGA MBINU ZA KUPAMBANA NA UGAIDI BARANI AFRIKA.
RAIS Jakaya Kikwete leo anatarajiwa kuungana na marais wengine 14 wa Afrika, kujadili mbinu za kupambana na ugaidi na matukio mengine kuhifadhi raia wa Nepal yanayotishia hali ya usalama barani Afrika.
Marais hao wanakutana jijini hapa katika mkutano wa siku moja wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Kenyatta (KICC).
Mbali ya marais hao na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama kutoka nchi wanachama wa baraza hilo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, pia anatarajiwa kuhudhuria.
Akizungumza jana jijini hapa, Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia yaliko makao makuu ya AU, Naimi Aziz alisema Afrika imechoshwa na matishio ya kiusalama barani Afrika, hivyo imeonekana kuna kila sababu ya kuchukua hatua dhidi ya ugaidi.
"Kwa kuwa kasi na vitendo vya kigaidi vinaongezeka, Baraza la Amani na Usalama la AU limeona kuna ulazima wa kuchukua hatua.
"Hivyo wakuu wa nchi wanachama wa Baraza la Usalama wameona kuna haja ya kutafuta njia za uhakika za kukabili ugaidi Afrika. Tunatarajia katika mkutano huu wa siku moja, kikao kitakuja na maamuzi mazuri ya kukabiliana na ugaidi," alisema Aziz ambaye pia ni mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Afrika.
Mkutano huo wa marais kutoka nchi wanachama wa Baraza la Amani na Usalama wa AU, unafanyika baada ya wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi hizo kukutana kwa wiki moja mjini Mombasa, kujadili jinsi ya kukabiliana na ugaidi.
Mbali ya Tanzania ambayo Rais Kikwete na ujumbe wake uliwasili Nairobi jana jioni, nchi nyingine zenye wajumbe wa baraza hilo ni Nigeria, Uganda na Chad ambayo kwa sasa ndiyo Mwenyekiti wa baraza hilo. Nyingine ni Equatorial Guinea, Gambia, Burundi, Ethiopia, Algeria, Namibia, Msumbiji, Afrika Kusini, Niger na Rwanda.
Aidha, Balozi Aziz alisema kutokana na uzito wa matukio ya kigaidi, marais wa Somalia na Djibout wamealikwa kutokana na nchi zao kuwa na mazingira magumu ya kiusalama, kutokana na kuwapo kwa makundi ya kigaidi katika nch
0 comments: