Posted by
khamisimussa77@gmail.com
at
7:43 AM
MABINGWA
wa Ulaya, Real Madrid wamemsajili mlinda mlango na shujaa wa Costa Rica
katika fainali za kombe la dunia majira ya kiangazi mwaka huu nchini
Brazil, Keylor Navas.
Navas
amekubali kusaini mkataba wa miaka sita na sasa anaingia katika
ushindani na kipa Iker Casillas kwasababu kuna dalili kuwa kipa mwingine
Diego Lopez anasepa zake.
Taarifa
iliyochapishwa kwenye mtandao rasmi wa klabu ya Real Madrid jana jioni
inasomeka: "Real Madrid CF na Levante UD zimefikia makubaliano juu ya
uhamisho wa Keylor Navas, ambaye atajifunga klabuni kwa misimu sita
ijayo""Mchezaji
atatambulishwa jumanne, Agosti 5, saa 7:00 mchana (saa za Hispania)
kwenye uwanja wa Bernabeu, baada ya kuchukuliwa vipimo vya afya
NA BARAKA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: