ANGALIA PICHA WAPIGANA MAPANGA MCHANA DAR

 Kijana aliyekatwa na sime kichwani.
 Timbwili lenye ujazo mkubwa limeibuka baa ambapo jamaa mmoja muokota chupa za maji ambaye jina lake halikupatikana, anadaiwa kukatwa sime kichwani na mwenye gari baada ya kukutwa amekaa karibu na gari hilo.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, tukio hilo la kuumiza lilijiri wikiendi iliyopita mishale ya asubuhi kwenye baa mpya iitwayo Kangaroo iliyopo eneo la Afrika Sana jijini Dar.Ilielezwa kwamba kijana huyo alikuwa amekaa pembeni ya gari hilo huku akisoma Gazeti Pendwa la Amani ambalo ni ndugu na hili, mara ghafla alikuja mtu akitokea ndani ya baa kisha akaingia kwenye gari lake aina ya Toyota Noah akatoka na sime na kuanza kumshambulia jamaa huyo kichwani.

Aliyemkata mwenzie na sime (kushoto) maeneo ya baa mpya iitwayo Kangaroo iliyopo eneo la Afrika Sana jijini Dar es Salaam.
 Kufuatia tukio hilo, watu walijaa na kufunga mtaa wakishangaa kilichotokea huku aliyefanya kitendo hicho akikimbilia ndani ya baa kujinusuru na raia wenye hasira kali waliotaka kumlipizia kwa kumuua baada ya kugundua kuwa kijana huyo aliyeshambuliwa hakuwa mwizi.
Polisi akiingia eneo la tukio kutuliza ugomvi uliojitokeza.
 “Mimi siyo mwizi, nilikuwa nimepumzika baada ya kuzunguka sana, nikaamua kutulia na kusoma gazeti, nimeonewa mimi ni muokota chupa za maji tu,” alisema kijana huyo kwa uchungu huku akitoa tafsiri ya namna wenye nazo wanavyowanyanyasa maskini.
Wanawake wakishudia mkasa huo.
 Baada ya kujielezea, watu waliamua kumfuatilia mwenye gari na kuanza kumpiga wakitaka awaambie sababu za kumkata kijana huyo.Hali ilipokuwa tete, uongozi wa baa hiyo ulitoa taarifa kwenye Kituo cha Polisi cha Kijitonyama a.k.a Mabatini, Dar ambapo askari walitinga katika eneo hilo ndani ya dakika sifuri wakiwa tayari kwa lolote.
Raia walikuwa eneo la tukio.
 Askari hao waliokoa jahazi kwa kuwatuliza raia hao na kuwachukua wahusika wote na kuondoka nao kwa ajili ya kutoa maelezo kituoni ili sheria ichukue mkondo wake. - See more at: http://jocyberspace.blogspot.com/2014/08/timbwili-zito-la-aina-yake-laibuka.html#sthash.Cj8sCrco.dpuf

0 comments: