DIDA WA TIMES FM AONESHA JEURI NYINGINE YA PESA

 Hadija Shaibu ‘Dida’ akiikagua gari yake.

Zimemtembelea! Prizenta wa Kipindi cha Mitikisiko ya Pwani kinachorushwa na Radio Times FM, Hadija Shaibu ‘Dida’ ameonesha jeuri nyingine ya fedha baada ya kununua magari mengine mawili kwa mpigo.Dida amefanya kufuru hiyo ikiwa imepita miezi kadhaa tangu atangaze kuwa ana nyumba mbili maeneo ya Goba na Kigamboni pamoja na kuyaanika magari manne anayomiliki (Toyota Verossa mbili, Toyota Noah nyeusi na Toyota Vitz.) 
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, rafiki wa karibu wa Dida aliyeomba hifadhi ya jina alisema ameshtushwa na kitendo cha shosti wake huyo kununua magari mawili kwa mpigo kiasi cha kumfanya ahisi kuna biashara nyingine anaifanya tofauti na utangazaji.

Prizenta wa Kipindi cha Mitikisiko ya Pwani, Hadija Shaibu ‘Dida’ akipozi kwenye gari yake mpya.

 “Kanunua magari mawili, Toyota Noah na Toyota Brevis New Model. Yaani hata sisi mashosti zake anatufanya tuhisi labda anafanya ile biashara ya unga kama watu wanavyohisi.
 “Ni kweli anafanya biashara zake lakini ndiyo apate fedha za kuonesha jeuri hiyo? Ila kama ni kupambana na maisha, sasa hivi anapambana kikwelikweli, hata akijiita Boss Lady ni sahihi kabisa,” alisema mtoa habari huyo.

Gari jingine la ‘Dida’ aina ya Toyota Noah.

 Baada ya kupata taarifa hizo, mwandishi wetu alimtafuta Dida ili kujua ukweli wa magari hayo, alipopatikana alifunguka:
 “Siwezi kujiita Boss Lady kimdomomdomo tu, huwa napenda kufanya kitu watu ndiyo waseme, nimeongeza magari mengine mawili. Moja ni Noah kwa ajili ya biashara zangu na lingine ni Toyota Brevis la kutembelea,” alisema Dida aliyetengana na mumewe, Ezden Jumanne siku chache zilizopita.

0 comments: