Posted by
khamisimussa77@gmail.com
at
7:44 AM
Tabasamu
'bab kubwa': Ashley Young akiungana na wachezaji wenzake Wayne Rooney
na Danny Welbeck kwenye mazoezi ya Manchester United.
LOUIS
van Gaal atawachana macho kwa macho wachezaji wake ambao wataachwa na
Manchester United baada ya kumaliza ziara ya Marekani ambapo amewapa
nafasi ya kumuonesha viwango vyao.
Anderson,
Nani, Javier Hernandez, Shinji Kagawa na Marouane Fellaini ni miongoni
mwa majina makubwa yaliyopo katika mstari mwekundu kabla ya kufungwa kwa
dirisha la usajili.
Lakini inafahamika kuwa Van Gaal hatakuwa na huruma kabisa ingawa hajafanya maamuzi ya hadharani.
'Nitafikia maamuzi baada ya ziara hii,' alisema. Nimewapa nafasi ya kucheza wachezaji wote na najua zaidi hata kabla ya ziara.
Louis van Gaal atawaambia wachezaji asiowahitaji kuwa wapo tayari kutafuta timu nyingine.
'Kwa
sasa nimefikia maamuzi kidogo, lakini kwenye mpira wa miguu lazima
uamue. Unatakiwa kuwapa nafasi wachezaji kufanya usajili pale unapoona
hawana nafasi ya kucheza kwenye kikosi chako.
'Unatakiwa
kusema mapema kwasababu ni mbali sana baada ya Agosti 31. Nitawaambia
wachezaji baada ya ziara hii, lakini nitawaambia wao na sio ninyi.'
Van
Gaal aliyasema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari mjini Miami
jana kuelekea mechi ya fainali ya leo usiku ya kombe la kimataifa nchini
Marekani dhidi ya mahasimu wao wakubwa England, klabu ya Liverpool.
CHANZO MPENJA BLOG
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: