MAMA SALMA KIKWETE AKUTANA NA WANAWAKE WATANZANIA WAJASIRIAMALI WAISHIO WASHINGTON

IMG_0015 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea shada la maua kutoka kwa Ndugu Juster Mutakyawa mara baada ya kuwasili kwenye ofisi ya ubalozi wa Tanzania nchini Marekani iliyoko Washington tarehe 3.8.2014.
IMG_0019Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akipokewa na Mwenyekiti wa kikundi cha wanawake wajasiriamali cha Watanzania wanaoishi Washington kiitwacho TANO Ladies Ndugu Asha Hariz wakati alipotembelea ofisi ya ubalozi wa Tanzania nchini Marekani tarehe 3.8.2014

IMG_0035Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea kipeperushi kutoka kwa Rais na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya  Help for Underserved Communities  (HUC) ya nchini Marekani Ndugu Zawadi Sakapalla baada ya kupata taarifa ya huduma mbalimbali zitolewazo na kampuni hiyo. Kampuni hiyo husaidia familia maskini kwa kuwapatia huduma ya maji safi na salama kwa kuwachimbia visima pamoja na kutoa vifaa vya elimu kwa wanafunzi.
IMG_0122Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza na akina mama wa kitanzania wajasiriamali wanaoishi nchini Marekani kwenye ukumbi wa ofisi ya ubalozi wetu mjini Washington tarehe 3.8.2014.
IMG_0170 Baadhi ya wanawake wajasiriamali na wafanyakazi wa ubalozi wa Tanzania nchini Marekani wakisikiliza kwa makini hotuba iliyokuwa ikitolewa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.

PICHA NA JOHN LUKUWI.

0 comments: