FLORA MBASHA, ROSE MUHANDO,SHUSHO NDANI YA KANISA LA GWAJIMA
Christina Shusho na Flora Mbasha wakiimba sambamba na waumini wengine waliohudhuria misa hiyo.

Flora Mbasha akiimba katika kanisa la Gwajima.
Halima Mdee akisisitiza jambo alipokuwa akiwahutubia waumini wa kanisa hilo.
Mchungaji Gwajima akicheza kwa shangwe.
Rose Mhando akicheza kwa hisia na shangwe kubwa.
Umati wa watu waliohudhuria misa hiyo wakifuatilia kwa makini.
Upendo Nkone akiimba kwa hisia kali.
Gwajima (kushoto) akicheza pamoja na Christina (Kulia).WAUMINI wa Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Mchungaji Josephat Gwajima leo wamefanya ibada ya shukrani kwa kupata helikopta. 
Kanisa hilo lililopo maeneo ya Kawe jijini Dar limetoa shukrani zake za dhati kwa Mwenyezi Mungu kuwawezesha kumiliki helikopta hiyo ambayo itatumika zaidi kutoa huduma  sehemu mbalimbali za Tanzania na duniani kote.
Helkopta hiyo inakadiriwa kugharimu shilingi bilioni 7.5.
Misa hiyo iliyoanza majira ya asubuhi mpaka jioni ilifanyika kwenye Uwanja wa Tanganyika Packers ambapo ilihudhuriwa na waimba injili maarufu nchini wakiwemo; Rose Mhando, Upendo Nkone, Christina Shusho, Flora Mbasha, John Lissu, Boniface Mwaitege, Munishi na wengineo.
Picha/Stori na Gabriel Ng’osha na Shani Ramadhani/GPL

0 comments: