Posted by
khamisimussa77@gmail.com
at
6:00 AM
Watu
wanadhaniwa kuwa ni majambazi wamemuua kinyama kwa kupiga risasi
moja ya kichwani mwenyekiti wa chama cha mapinduzi kata ya Busambala
wilayani Butiama mkoani Mara Bw Willison Opio mwenye umri wa miaka 6o
huku kichwa chake kikisambaratishwa kabisa na risasi hiyo.
Mauaji hayo
ya kinyama yamefanyika saa saba usiku wa kuamkia leo,baada ya majambazi
hayo kuvunja milango ya nyumba aliyokuwa amelala kiongozi huyo na
familia yake katika kijiji cha Kwikuba kabla ya kumshambulia kwa bapa
za panga mke wamarehemu Bi Agness Wambura ambaye alilazimika kuwapa
kiasi cha shilingi laki nne ambazo alizikopa kutoka katika taasisi
moja ya fedha.
Afisa
upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa Mara Acp Rogati
Mlashan,akizungumza na ITV akiwa eneo la tukio, amesema baada ya
majambazi hayo kuvunja milango miwili ya nyumba hiyo, walipiga risasi
tatu na moja kumpata kichwani kiongozi huyo wa CCM na kufariki dunia
papo hapo na kusema kuwa jeshi la polisi litafanya kila liwezavyo
ili kuhakikisha wote walihusika kufanya uhalifu huo wanakamatwa na
kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Kwa
upande wao baadhi ya viongozi serikali katika kata ya
Busambala,wakizungumzia tukio hilo pamoja na kuonyesha masikitiko yao
baada ya kupata taarifa za kifo cha kiongozi huyo wa CCM,wameliomba
jeshi la polisi kuendesha msako mkali ambao utawesha kukamatwa kwa
wahusika,hatua ambayo wamesema itasaidia kuondolea wananchi hofu kubwa
waliyonayo sasa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: