Posted by
khamisimussa77@gmail.com
at
5:51 AM
Mkazi
huyo wa Mtaa wa Kigera Kibini, Kata ya Kigera, Manispaa ya Musoma
mkoani Mara, anasimlia historia ya maisha yake hadi kuzaa mtoto huyo wa
mwisho nje ya ndoa baada ya mumewe kufariki, lakini hatima imekuwa
kugeuzwa mke mwenza.
Mwita
anasita kuendelea na simlizi kabla binti yake aliyefanyiwa unyama na
baba yake, hajasimulia masaibu yake: “Matatizo niliyonayo ni mengi,
Mungu pekee ndiye anayefahamu, bado naongezewa msalaba mzito kama huu.”
Ghafla
anapaza sauti anaita jina la binti yake aliyefanyiwa ukatili, aliyekuwa
chumba kingine na kumtaka aeleze yote yaliyomsibu ili ulimwengu
utambue.
Anatokea
binti mrembo ila sura yake inaonyesha unyonge, mrefu, mwembamba
anasalimia kwa sauti ya upole huku akielekea kwenye kiti kuketi, afya
yake siyo ya kuridhisha.
Bila
kupoteza muda, binti huyo anadai alianza kuishi na baba yake mwaka
2002 akiwa anaingia darasa la tatu, baada ya mama yake kupata kibarua
kwenye nyumba ya watawa.
Anasema
baba yake alikuwa akiishi na kaka zake wawili wakubwa ambao walikuwa
wamemaliza shule na wakati huo walikuwa wakijihusisha na kazi za
vibarua.
Anasimulia
kuwa alipofika darasa la tano, baba yake alikuwa akimfuata chumbani
kabla ya kaka zake hawajarudi nyumbani na kumtaka afanye naye ngono.
Binti huyo anasema kwamba wakati huo alikuwa hafahamu chochote kuhusu
mapenzi.
“Nilipoona
baba ananipiga kila siku, nilikubali, akawa anakuja chumbani kwangu na
wakati mwingine ananiita kwake, tukishamaliza ananiambia niende kwangu
kulala, hivyo nikaona kama jambo la kawaida,” anasimulia binti huyo.
Anaendelea
kusema kuwa baada ya kumaliza shule ya msingi mwaka 2009, alibaki na
jukumu la kumhudumia baba yake kama mume wake, jambo ambalo anadai
lilikuwa likimuumiza, hivyo akaamua kuwa wazi ili apate msaada.
Baada
ya kumweleza dada yake, alimpa mbinu za kutoroka ili amsaidie
kumfikisha kwa mama yao aliyekuwa amehamia Kijiji cha Kabasa, Wilaya ya
Bunda.
Bhoke
anasema baada ya mumewe wa ndoa kufariki mwaka 1989, alianza uhusiano
na mwanamume huyo (anamtaja) alipata mimba na kujifungua binti huyo
Septemba 3, 1994.
“Nilipojifungua
mwanamume huyo alinitunza vizuri, alimpenda mwanawe hivyo sikuhangaika
kumlea ingawa alikuwa mume wa mtu, kwa sababu alikuwa na familia yake,”
anasimlia Bhoke.
Anasema
kuwa mwaka 2003 alipata kibarua cha upishi nyumba ya watawa wa Shirika
la Utawa mjini hapa, huku akitakiwa kuishi kwenye nyumba hiyo hivyo
ilimlazimu kumtafutia mtoto wake sehemu ya kuishi kutokana na nyumbani
kwake kutokuwapo mtu.
Mama
huyo anadai baada ya mwanamume kupata taarifa kuwa mtoto amepelekwa
kuishi kwa babu yake, alimfuata na kumwomba ampe mwanaee akamlee.
“Sikuwa
na sababu za kumnyima mtoto, kwani ni wake, hivyo nilimkabidhi. Hata
hivyo, nyumbani kwake hapakuwa mbali na nilipokuwa naishi,” anasema
Bhoke na kuongeza:
“Kipindi
anamchukua alikuwa anaingia darasa la tatu, hivyo alikuwa na akili ya
kutambua zuri na baya, niliamini kama ataona anateseka atarudi hapa kwa
dada zake.”
Anasema
yeye aliendelea kufanya kazi nyumba ya watawa kwa miaka miwili, kisha
akarejea nyumbani na kuamua kwenda kijijini kulima.
Bhoke
anadai kabla hajaenda kijijini alikuwa akisikia maneno kwa majirani
kuwa, mzazi mwenzike ana uhusiano wa kimapenzi na binti yake, lakini
hakuamini, huku akimtaka binti yake mmoja kufuatilia ukweli wa tetesi
hizo.
Anadai
mwaka 2007, binti yake alianza kutaja maovu ya baba yake kwa dada yake,
lakini akimtaka asimweleze mama yake, ingawa alimwambia licha ya kusema
kuwa baba yake akimtaka kimapenzi, hakutamka iwapo wanajamiiana.
“Baada
ya kupata taarifa hizo nilianza kuhisi kitu ila sikuwa na la kufanya,
kwa sababu mtoto mwenyewe hana ushirikiano wa kutosha,” anadai Bhoke.
Mwaka 2007, binti alimaliza elimu yake ya msingi Shule ya Kamnyonge lakini alishindwa kuendelea na sekondari.
Anadai
baada kushindwa, baba yake alimpeleka Shule ya Msingi Nyasho kurudia
darasa la sita, hivyo alimaliza tena darasa la saba mwaka 2009 lakini
hakufaulu.
Dada
yake binti huyo anadai baada ya mdogo wake kukiri baba yake anajamiiana
naye kwa lazima, alimhurumia na kumsihi atoroke na kwamba atampa nauli
aende kwa mama yake kijijini. Anasema alipofika kwa mama yake
alitafutiwa shule akarudia darasa la saba Shule ya Msingi Kung’ombe,
Wilaya ya Bunda mwaka 2011, alifaulu na kujiunga na Sekondari ya Wariku
mwaka 2012.
Ads by OffersWizardAd Options
Anadai
baada ya kufunga shule Juni akiwa kidato cha pili, alimlazimisha mama
yake ampe nauli ili aende Musoma kumsalimia baba yake. Anadai alipofika
kwa baba yake hakurejea tena Bunda, zaidi ya baba yake kumpigia simu
mama yake kuwa mtoto wake anateseka hivyo anamchukulia uhamisho asomee
Musoma Mjini.
Anadai
mdogo wake alihamia Sekondari ya Nyasho mjini hapa, ambako alisoma
miezi miwili na kuachishwa na baba yake na kumpeleka Kijiji cha
Sirorisimba, wilayani Serengeti kufanya kazi za hotelini.
Hata
hivyo, anadai siri ilifichuka baadaye kwamba mdogo wake alitoroshwa
kutokana na ujauzito, hivyo baada ya mimba kukua alishindwa kuendelea na
kazi ili apate nauli ya kurejea kwa mama yake Bunda.
Baada
ya kufika kwa mama yake, alimpeleka kupima ingawa binti huyo alikataa
kuwa siyo mjamzito lakini vipimo vilionyesha ana ujauzito.
Mama
yake alimpa nauli ya kurudi kwa baba yake kwa sababu alimchukua kwa
madai ya kumsomesha, hivyo hakuona umuhimu wa kumpokea akiwa na hali
hiyo.
Dada
yake anaendelea kusema, siku moja alikwenda kumsalimia mdogo wake na
kumkuta akiwa na hali mbaya, hatua iliyomshtua na kumpigia simu mama
yao na ndugu zake wengine ili kumpa msaada wa kumpeleka hospitali.
“Nilimkuta
mdogo wangu akiwa na hali ambayo siyo nzuri kwa kweli, alikuwa kavimba
mwili mzima, halafu amejisaidia haja kubwa na ndogo hapohapo kitandani
hakuna msaada, niliumia sana!”
Baada
ya kumpeleka hospitali vipimo vilionyesha ana maambukizi ya virusi vya
Ukimwi, walimpa ushauri nasaha na kumwanzishia dawa za kuzuia maambukizi
ya mama kwenda kwa mtoto.
Anasema
binti alikaa nyumbani wiki moja tu na kujifungua mtoto akiwa amekufa,
kufuatia hali hiyo taarifa zililifikia Dawati la Jinsia la Polisi na
kumtia mbaroni mtuhumiwa.
Awali,
binti huyo alikuwa akipewa msaada na Shirika lisilo la Serikali la
Watoto Wapinge Ukimwi (WWU) mjini hapa kama mtoto anayeishi katika
mazingira magumu, walimsaidia akiwa darasa la kwanza hadi la saba, baada
kuhitimu elimu ya msingi hawakuendelea naye.
Mkurugenzi
wa shirika hilo, Sista Marion Haqhes anasema hawezi kumzungumzia mtoto
huyo kwa sababu shirika lake na sheria ya mtoto haimruhusu ingawa tukio
hilo ni kweli.
Kaimu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Paul Kasabago anathibitisha kuwapo
taarifa za ubakaji na kwamba, mtuhumiwa amekuwa akimbaka binti yake muda
mrefu.
Kasabango
anasema licha ya mtuhumiwa kumbaka binti yake mara kwa mara,
amemsababishia ujauzito aliojifungua mtoto aliyekufa na vipimo
vimeonyesha amemwambukiza Ukimwi.
Anasema kwa sasa mtuhumiwa yupo rumande kwa mahojiano zaidi na kwamba, atafikishwa mahakamani muda wowote.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: