KILA LA KHERI SIMBA SC KATIKA UCHAGUZI WENU....WANACHAMA MSIFANYE MAKOSA, SAFARI NI NDEFU!

http://www.eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/field/image/simbaz.jpg?itok=iAv7P-nO 

Safari ya miaka minne ya mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage inafikia kikomo leo
SIMBA SC wapo katika  mkutano  mkuu wa Uchaguzi unaoendelea muda huu katika Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Uchaguzi huo unashirikisha jumla ya wagombea 27 ambapo nafasi ya juu kabisa, Urais, inawaniwa na wagombea wawili Evans Elieza Aveva na Andrew Peter Tupa.
Nafasi ya Urais inawaniwa na Swedi Mkwabi, Bundala Kabulwa ,
Geofrey Nyange `Kuburu`  na  Jamhuri  Musa Kihwelo `Julio`.
Wanaowania ujumbe wa kamati ya utendaji  ni Said Tulliy,  Yasini Mwete, Ally Suru,  Rodney Chiduo,  Said Pamba, Ally Chaurembo , Abdulhamid Mshangama , Chano Almasi,  Damian Manembe,  Ibrahim Masoud, Kajuna Noor,  Hamisi Mkoma, Alfred Elia na Saidi Kubenea.
Wagombea wengine ni Idd Mkamballah, Juma Mussa, Maulid Abdallah na Collin Frisch. Wagombea.
kwa upande wa wanawake ni Asha Muhaji, Amina Poyo na Jasmine Badour.
Mchakato huu wa uchaguzi umefika hapa ulipo baada ya kugubikwa na mizengwe kadhaa.
Inafahamika kuwa matatizo yalianza siku alipoenguliwa mgombea wa nafasi ya Urais Michael Richard Wambura.
Wambura alienguliwa na kamati ya uchaguzi ya Simba sc, chini ya mwenyekiti wake, Wakili Dkt. Damas Daniel Ndumbaro kwa sababu ya kuipeleka Simba mahakamani na kusimamishwa uanachama mwaka 2010.
Lakini `kidume` alikata rufaa katika kamati ya rufani ya uchaguzi ya TFF chini ya mwenyekiti wake, Jaji Julius Mutabazi Lugaziya.
Kamati ya jaji Lugaziya alimrejesha Wambura kuendelea na mchakato wa uchaguzi baada ya kubainika kulikuwa na makosa yaliyofanywa na Simba kwa kumuacha Wambura aendelee kufanya shughuli za klabu kama mwanachama akiwemo kulipa ada wakati walimsimamisha.
 http://shaffihdauda.com/wp-content/uploads/2014/06/simba-mkutano6.jpg
Lakini kamati ya Ndumbaro alimuengua kwa mara ya pili kwa sababu ya kupiga kampeni kabla ya muda. Wambura alikata rufaa tena katika kamati ya uchaguzi ya TFF, lakini rufani yake ilikataliwa, hivyo kutoka rasmi kwenye mchakato wa uchaguzi wa Simba sc.
Baada ya tukio hilo, baadhi ya wanachama wa Simba walienda kufungua kesi mahakama kuu wakitaka mahakama isimamishe uchaguzi kwasababu Wambura hakutendewa haki.
Mahakama Kuu ilikataa kusimamisha uchaguzi huo, na hatimaye leo hii rais mpya, makamu wa rais na wajumbe wa kamati ya utendaji wanapatikana.
Ilikuwa safari ndefu na wengine waliamini isingetimia, lakini hatimaye kitendawili kimeteguliwa.
Kazi kwenu wanachama wa Simba. Kwa muda sasa mmesikiliza kampeni za wagombea wote. Kinachotakiwa ni kutuliza akili kwenye maboksi ya kura ili wapatikane viongozi sahihi.
Inafahamika wapo ambao wanaumia kwasababu wagombea wanaowaunga mkono walienguliwa hususani Wambura, lakini yameshatokea na mwisho wa siku Simba ni yenu na mnatakiwa kushirikiana kupata viongozi wapya.
Simba inahitaji mabadiliko makubwa, na kwa kuanza, leo ni siku muhimu kwa wanasimba wote.
Zaidi mtandao huu na timu yake unawatakia kila la heri katika uchaguzi wenu unaofanyika leo.

0 comments: