VIBINTI HIVI VINADAIWA KUBAKWA KWA ZAMU NA MCHUNGAJI WA KANISA LA PENTEKOSTE |
Baadhi ya walimu wa shule ya Msingi Maendeleo wakizungumza kwa hisia tukio hilo la ubakaji lililofanywa na Mchungaji |
Kanisa linaloendeshwa na Mchungaji Bryson Mwaikambo |
Shule ya Msingi Maendeleo ambako wanasoma wasichana wanaodaiwa kubakwa na Mchungaji kwa zamu |
Wazazi wa watoto wanaodaiwa kubakwa na Mchungaji wakiwa katika sura ya huzuni |
Nyumba anayoishi Mchungaji Mwaikambo ikiwa imepigwa kufuri huku mwenyewe akiwa ''amelala mbele!! baada ya kufanya unyama wake |
Kufuri!!! Ngaaa!!!! mchungaji huyooo kasepa |
Nyumba anayoishi Mchungaji Mwaikambo |
Diwani wa Kata ya Nsalala Mashauri Mbembela akitoa msimamo wake juu ya vitendo vya kinyama walivyofanyiwa mabinti hao |
Ripota Wetu
MCHUNGAJI wa kanisa la
Pentekostal aliyefahamika kwa jina la Bryson Mwaikambo(55) anadaiwa kuwabaka na
kuwaambukiza ugonjwa wa zinaa wanafunzi wawili wa kike wanaosoma katika shule ya
msingi ya Maendeleo wa
kata ya Nsalala wilaya ya Mbeya vijiji mkoani Mbeya.
Wanafunzi hao (majina
yanahifadhiwa) wenye umri kati ya miaka 11 na 13 wanaosoma darasa la nne na
darasa la sita walifanyiwa unyama huo kuanzia mwaka 2012 ambapo alianza kujenga
mazoea na watoto hao wadogo kwa kuwapa peremende pamoja na fedha.
Imeelezwa kuwa mchungaji huyo
ambaye anaendesha ibada katika kanisa hilo dogo lenye waumini wachache lililopo
kitongoji cha kanani kijiji cha ‘Tunduma Road’alikuwa akiwavizia watoto hao kwa
muda mrefu kila walipokuwa wanapita kuelekea shuleni.
Katika jitihada zake za kuwanasa
watoto hao wa kike alimdanganya mmoja wa wazazi wa watoto aliyefahamika kwa jina
la Bw.John Mussa(38) na kumuomba binti yake awe anamsaidia kazi za nyumbani
nyakati za jioni kutokana na kuwa mke wa mchungaji kuwepo
safarini.
Kwa kuamini kuwa mchungaji huyo
alikuwa ni mtumishi wa Mungu, Bw. Mussa aliridhia mwanaye aende kuishi na
Mtumishi huyo wa Mungu bila kujua hatima ya kile ambacho kimemtokea binti yake
kwa sasa.
Kwa mujibu wa maelezo kutoka kwa
wazazi na walimu wa shule ya Msingi Maendeleo ni kwamba mabinti hao walikuwa
wakifanya ngono na mchungaji huyo kwa zamu na kwamba walianza kujua tatizo hilo
baada ya kutokea mgongano baina ya wasichana hao wawili .
‘’Tumejua tukio hili baada ya kutokea
ugomvi baina yao wa kugombania maji na hivyo kuanza kurushiana maneno, mmoja wa
watoto hao alikuja ofisini kushitaki kuhusu ugomvi wao ndipo mmoja akasema kuwa
mwenzie anatembea na Mchungaji Mwaikambo’’alisema Mwalimu mkuu msaidizi Bi. Lucy
Kamongile.
Alifafanua kuwa, baada ya tukio hilo
walimu kwa pamoja walilazimika kuwauliza zaidi ndipo walipoanza kujieleza kuwa
wamekuwa wakilala na Mchungaji huyo kwa muda mrefu na kwamba mwanzo alikuwa
akiwapa peremende na baadaye akaanza kuwapa fedha.
Alisema kuwa walilazimika kuitisha
kikao cha dharura baina ya wazazi wa watoto hao na walimu ambapo walieleza tukio
zima la kuingiliwa kimwili na Mchungaji huyo tangu mwaka jana.
‘’Nililazimika kuwaita wazazi pamoja
na wanafunzi tulikaa katika ofisi ya walimu, watoto walieleza tukio zima mbele
ya wazazi wao juu ya vitendo walivyokuwa wakifanyiwa na Mchungaji
huyo.
Alisema kuwa mara baada ya kikao
hicho cha wazazi waliwapeleka watoto hao katika kituo kidogo cha Polisi
kilichopo katika mji mdogo wa Mbalizi ambako walipewa Fomu ya Polisi Na.
3,(PF3) kwa ajili ya kuepelekwa hospitali ili wapatiwe matibabu.
Mwalimu Kamongile ambaye alikuwa na
walimu wenzie katika ofisi ya Mwalimu mkuu wa shule hiyo wakati akitoa taarifa
hizi mbele ya Ripota Wetu kuwa wanafunzi hao walipatiwa matibabu katika
hospitali Teule ya Ifisi ambapo kwa mujibu wa taarifa za mganga aliyewachunguza
watoto hao ni kwamba mbali na kufanyiwa ubakaji wote wawili walikuwa
wameambukizwa ugonjwa wa zinaa wa kaswende.
‘’Tukio hili limetufedhehesha sana
tulikuwa tunatafakari wapi tutaenda,tunaomba kilio chetu kifike chama cha
Waandishi wa Habari wanawake TAMWA kitoe taarifa hizi kwa undani waone namna
ambavyo jamii ya pembezoni inavyokosa msaada na haki za kisheria,’’alisema
Mwalimu Kamongile.
Mwalimu huyo alisema kuwa wanatambua
juhudi za chama cha waandishi wa habari wanawake TAMWA ambazo wamekuwa
wakizifanya hivyo wanaimani chama hicho kikisikia suala kitalifanyia kazi kwa
kina zaidi kuisaidia jamii ambayo aina mahali pa kusemea.
Kwa upande wa watoto hao ambao
walikuwa wakizungumza kwa kupokezana juu ya kadhia iliyowakuta walisema kuwa
Mchungaji huyo alianza kufanya nao vitendo vya ngono tangu mwaka 2012 kwa
kuwadanganya kwa fedha na peremende na baadaye wakazoea kwenda kwa Mchungaji
huyo mara kwa mara.
Mwanafunzi anayesoma darasa la nne
alisema kuwa alianza kutembea na Mchungaji huyo wakati akimpitia mwenzie
aliyekuwa akiishi nyumbani kwa mchungaji ambapo siku hiyo alimuita chumbani
kwake na kumlazimisha kulala kitandani ambapo alianza kumuingiza vidole katika
sehemu zake za siri.
“Siku ya kwanza nililia sana wakati
mwenzangu yupo pembeni akishuhudia mchungaji akinifanya na ndipo mwenzangu
alisema jikaze rafiki yangu”alisema Mtoto huyo.
Alisema kuwa mara baada ya kumuingiza
vidole alivua nguo zake na kumbaka huku akilia wakati msichana mwenzie (alimtaja
jina) akiwa amekaa pembeni ya kitanda akimweleza kuwa aache kulia kwa kuwa baada
ya kumaliza watapewa fedha za kutumia shuleni.
Binti huyo aliendelea kusema kuwa
alipata maumivu makali wakati Mchungaji huyo akitekeleza ubakaji wake ambapo
mara baada ya kumaliza` alimpa sh.500 na peremende na baadaye alimwita mwenzie
kitandani na kufanya naye ngono huku akishuhudia kwa macho yake.
Alisema mara baada ya kumaliza
kufanya na mwenzie Mchungaji Mwaikambo aliwaonya wasiseme kwa wazazi wao kisha
akawapa fedha na kuwaonya wasiseme jambo hilo kwa mtu yoyote.
Akizungumza sababu za kutosema kwa walimu au
wazazi wake binti mwingine anayesoma darasa la sita alisema kuwa Mchungaji huyo
aliwatishia kuwachinja na kuwafukia kwenye shimo iwapo atasikia wamesema tukio
hilo kwa wazazi ama walimu wao.
Alisema kuwa Mchungaji aliwaomba
wazazi wake ili aende kuishi nyumbani kwake kumsaidia kazi kutokana na mama
Mchungaji ‘’Mke wa Mchungaji’’ kuwa safarini na kwamba katika siku hizo ndipo
Mchungaji huyo alipoanza kulala naye mahusiano taratibu.
Alisema kwa siku za mwanzo alikuwa
akimuingiza vidole katika sehemu zake za siri na baadaye akaanza kumbaka ambapo
alijisikia maumivu makali lakini alimbembeleza kwa kumpa sh.1000 ambayo alikuwa
akitumia shuleni kwa kununua chipsi.
‘’Alikuwa akiniingiza vidole huku
chini(akionyesha sehemu za siri) akanibaka, sikuweza kumwambia baba niliogopa
atanichinja..mwenzangu alipokuwa anakuja kunipitia kwenda shuleni naye alianza
kumuingiza vidole akambaka!!, alilia sana, nikamwambia asilie atatupa
hela,’’alisema.
Alisema kuwa wamebakwa na Mchungaji
huyo zaidi ya mara nne na kila alipokuwa akiwabaka alikuwa anawapa hela za
kutumia shuleni.
Kwa upande wazazi wa watoto hao
Bw.Suveli Harrison na Bw. John Mussa walikiri kuitwa shuleni na kupata taarifa
za kubakwa kwa watoto wao walipoitwa shuleni ambapo watoto walijieleza
walichokuwa wakifanyiwa na Mchungaji Mwaikambo mbele ya walimu.
‘’Jambo hili lilitushitua sana,
machozi yalitulenga, hatukutegemea kusikia Mchungaji anaweza kuwabaka watoto
ambao ni sawa na wajukuu zake, tulienda polisi walitupa karatasi tukaenda
Hospitali ya Ifisi, watoto walikutwa na maambukizi ya ugonjwa wa zinaa,’’alisema
Bw. John Mussa.
Alisema kuwa yeye aliridhia mwanaye
kuishi na Mchungaji huyo baada ya kuombwa kutokana na mchungaji huyo kuishi na
mtoto mdogo wakati mkewe akiwa safarini.
Bw. Mussa alisema kuwa hakujua kuwa kama kuna
siku mwanaye atadhurika kwa kufanyiwa kitendo cha unyanyasaji na ukatili wa
kijinsia kama walivyofanyiwa watoto hao na kwamba hata hivyo hadi sasa hakuna
jitihada zozote za jeshi la polisi zilizofanikisha kumnasa Mchungaji
huyo.
Alisema kuwa kwa sasa watoto hao
wamekuwa wakitishiwa na Mchungaji kutokana na kufahamika kuwa yeye aliwabaka na
kwamba anaomba msaada wa kisheria kusimamia haki ili sheria iifuatwe dhidi ya
mtuhumiwa wa ubakaji.
Naye mzazi mwingine Bw.Suvile
Harrison alisema kuwa hakujua chochote juu ya vitendo alivyofanyiwa mwanaye na
Mchungaji huyo na kwamba alifahamu tukio hilo baada ya kuitwa shuleni ambako
walimu waliwaita watoto wao na kueleza tukio zima walilokuwa wakifanyiwa na
Mchungaji.
Alisema kuwa hakubaini mabadiliko
yoyote kwa mwanaye juu ya vitendo alivyofanyiwa na wala hajawahi kuhisi lolote
hadi hapo alipoitwa shuleni na walimu.
Baada ya taarifa hizo waandishi wa
habari wa gazeti hili walifunga safari hadi katika nyumba ambayo inasadikiwa
kuwa ndipo anapoishi Mchungaji huyo na kukuta mlango ukiwa umefungwa lakini
alijitokeza jamaa ambaye alijitambulisha kuwa ni mmiliki wa nyumba hiyo Bw.
Zacharia Gambi.
Bw.Gambi alisema kuwa anamfahamu
mpangaji wake kwa jina moja la Mchungaji Mwaikambo na kwamba mbali ya kuwa ni
Mchungaji wa Kanisa la Kipentekoste ni Balozi wa nyumba kumi wa mtaa wa
Kanani.
Bw.Gambi alisema kuwa Mchungaji huyo
hajaonekana muda mrefu na kwamba mkewe amekuwa na desturi ya kuondoka alfajiri
kuelekea shambani na kurudi usiku.
Kadhalika imeelezwa na baadhi ya watu
ambao hawakupenda kutajwa majina yao gazetini kuwa kitendo cha Mchungaji huyo
kuwabaka mabinti wadogo kimetokana na imani za nguvu za giza kwamba kwa kufanya
hivyo kitamuongezea waumini katika kanisa lake dogo lililopo katika mtaa wa
Kanani.
Mama mzazi wa mmoja wa watoto
waliobakwa aliyejitambulisha kwa jina la Jane John(35) alisema kuwa awali yeye
alikuwa ni mmoja wa waumini katika kanisa hilo lakini baadaye walihamia kanisa
jingine baada ya kuona mienendo ya mchungaji huyo kutofanana na kazi ya huduma
za kiroho.
Alisema waumini wengi wamehama katika kanisa
hilo wakiwemo watoto wake wakubwa wa kike ambao walieleza waziwazi tabia ya
ukware ya Mchungaji huyo ya kuwafuatilia mabinti wadogo kwa ajili ya kufanya nao
vitendo vya ngono.
Diwani wa Kata ya Nsalala iliyopo Mbeya
vijijini Bw.Mashauri Mbembela alipozungumza na waandishi wa gazeti hili alisema
kuwa anashangazwa tukio hilo kutoshughulikiwa kwa kipindi chote huku taarifa
zikiwa zimefikishwa kituo cha polisi.
Alisema kuwa tukio hilo ni la
unyanyasaji ambalo lilipaswa kushughulikiwa kwa nguvu zote na kwamba kuna haja
ya kuweka sheria ngumu itakayokomesha vitendo vya ubakaji kwa watoto wa
kike.
Bw.Mbembela alisema kuwa ili
kukomesha tabia za ubakaji, itungwe sheria ya kuwahasi wabakaji badala ya
kuwafunga jela miaka 30 ambako wanaenda kula chakula kinachotokana na kodi za
wananchi.
‘’Wabakaji wanafungwa jela, wakimaliza
vifungo vyao hurejea uraiani ambako wanaweza kuendeleza vitendo hivyo, njia
pekee ya kukomesha ubakaji ni kuwahasi, wakirudi uraiani wataendeleza kujenga
Taifa,’’alisema Bw. Mbembela.
Ripota wetu alifanya jitihada za kutafuta
namba za simu za mchungaji huyo ambaye mara baada ya kupokea na kuulizwa juu ya
tuhuma hizo alikanusha na kusema kuwa huu ni uzushi na uongo uliolenga kumpaka
matope ili kuchafua huduma zake anazotoa kwa waumini .
Alidai kuwa kanisa lake la Pentecostal
Holiness lenye jumla waumini nane linatoa huduma za uhakika kijijini hapo hivyo
baadhi ya wafuasi wa shetani wanalipiga vita ili lisiendelee kukua ili kuwafikia
wanakondoo wengi.
“Wananipakazia tu unaweza kuingiwa na ibilisi
na hivi ulivyonipigia nafikiria kuchukua maamuzi magumu na mwili wangu hamtauona
kamwe bora uliwe na ndege na wanyama wa porini niende jehanamu kuliko
kuchafuliwa huku”alisema Mchungaji huyo.
Alisema kuwa tuhuma hizo zimeelekezwa kwake
baada ya kumdai fedha mmoja wa wazazi wa watoto hao ambaye alikuwa akifanya
kibarua cha kujenga ofisi ya kata ambapo mama huyo alimkopesha fedha sh.5000 na
alipoanza kudai ndipo akaanza kuzushiwa tuhuma hizo.
Hata hivyo alisema Jumanne iliyopita
alifuatwa na askari mgambo sita wenye virungu ambao walitaka kumkamata lakini
kwa nguvu za yesu walishindwa na kuondoka zao.
“Mimi naishi kwa nguvu za Yesu mtu yeyote
mwenye nia mbaya na mimi hawezi kunipata nataka niwe kama mfalme aliyejitoa
mhanga nijiue mwili wangu usionekane duniani”alisisitiza na kukata simu.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya
Bw.Diwani Athumani alisema kuwa amepata taarifa hizo za ubakaji ambapo
amemuagiza Ofisa Upelelezi wa Mkoa Bw.Mtatiro Nyamuhanga ambaye atalifuatilia
kwa karibu tukio hilo na kwamba hata hivyo mtuhumiwa bado hajatiwa
mbaroni.
0 comments: