CHADEMA KUJADILI MASUALA MAZITO IKIWEMO MISUKOSUKO KATIKA KIKAO CHA KAMATI KUU JIJINI DAR ES SALAAM.
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 6:08 AM
Mkurugenzi wa
Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika PICHA|MAKTABA.
Taarifa
iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika
ilisema kikao hicho kitakachofanyika Dar es Salaam kitapokea, kujadili na
kufanya uamuzi wa masuala mbalimbali ikiwamo hali ya siasa na ripoti ya
fedha.
“Suala
mojawapo litakuwa kujadili mihutasari ya mikutano iliyopita na yatokanayo na
mikutano hiyo, taarifa ya hali ya siasa na ripoti ya fedha,” ilisema taarifa
hiyo ya Mnyika, ambaye yuko ziara ya kikazi huko Uturuki.
Pia
utajadili mchakato na maudhui ya mabadiliko ya katiba, taarifa ya utekelezaji wa
Programu ya Chadema ni Msingi na shughuli za kanda na taarifa ya utekelezaji wa
Mpango Mkakati kuhusu maboresho.
Chadema katika mawimbi
makali
Miongoni
mwa mambo ambayo yanatarajiwa kujadiliwa katika kikao hicho ni mustakabali wake
katika kipindi hiki ambacho kinapita katika mawimbi makali kutokana na kuibuka
kwa malumbano ya waziwazi baina ya viongozi wake waandamizi na pia kusimamishwa
kwa baadhi ya viongozi wa mikoani.
Matukio ya
karibuni yanajumuisha malumbano kati ya Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe na Mbunge
wa Arusha Mjini, Godbless Lema kuhusiana na masuala ya posho, kusimamishwa kwa
Mwenyekiti wa Chadema wa Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba, kuvunjwa kwa uongozi
wa Mkoa wa Mara na pia kuondolewa kikaoni kwa Mbunge wa Maswa Magharibi, John
Shibuda.
Wafuatiliaji wa mambo ya siasa watakuwa
wanakitazama kikao hiki kama fursa ya kuweka sawa mambo ili kiendelee kutoa
ushindani kwa chama tawala.
Alipoulizwa
kama matukio ya hivi karibuni yatajadiliwa katika kikao hicho, Mnyika alikataa
kuingia kwa undani na badala yake alisema taarifa zitatolewa baada ya
kikao.
“Niko nje
ya nchi, mengine utapewa majibu kesho (leo) kwa yale ambayo yatakuwepo katika
taarifa zitakazowasilishwa. Yale ambayo hayatakuwepo utajulishwa pia iwapo
hayatajadiliwa,” alisema Mnyika.
Zitto na
Lema
Zitto na
Lema waliingia katika vita ya maneno mwanzoni mwa Novemba kuhusiana na masuala
ya posho ya vikao.MWANANCHI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: