WANAUME MUWAKIMBIA WAKEZAO MARAWANAPO ZA MTOTO MWENYE ULEMAVU.

Usimwache mkeo kwa
kumzaa mlemavu - MOI

Na Nyendo Mohamed

Taasisi ya Tiba na Mifupa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Kitengo cha Mifupa (MOI) imewataka Wanaume kuacha kuwatelekeza wake zao baada ya kujifungua watoto walio na ulemavu wa vichwa kujaa maji.

Akizungumza na Jambo Leo baada ya kufika katika Hospitali hiyo ili kufahamu ukubwa wa tatizo hilo Meneja Uhusiano na Ustawi Taasisi ya Tiba na Mifupa Jumaa Almasi alisema kuwa tatizo hilo ni kubwa ambapo wanaume wengi wamekuwa wakiwakimbia wake zao baada ya kujifungua watoto wenye Vichwa Maji.

Alisema watoto 1000 huzaliwa wakiwa hai ambapo asilimia 3.02 kati yao sawa na watoto 4485 huzaliwa wakiwa na ulemavu huo na watoto 200 hufikishwa katika MOI kupata matibabu.

Almasi alisema kumekuwa kuna idadi kubwa ya watoto wenye tatizo hilo kutofikishwa hospitali kutokana na wanaume kuwatelekeza wake zao ambapo hukosa msaada kwa ajili ya matibabu.

Aliongeza kuwa kuna changamoto kubwa ambayo inachangia kwa watoto hao kukosa matibabu ya haraka ikiwemo umbali wa vituo vya tiba na watoto hao wanapofkishwa hospitalini wamekuwa wakigundulika kuwa na magonjwa mengine kama utapiamlo hivyo hulazimika kutibiwa magonjwa mengine ili waweze kuwafanyia upasuaji.

Alisema hadi sasa kuna watoto 20wanaohitaji matibabu

0 comments: