MSIMAMO WA RAIS KIKWETE KWA RAIS KAGAME WA RWANDA WAUNGWA MKONO KWA ASILIMIA 100 NA WASOMI HAPA NCHIN
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 7:47 AM
WASOMI
na baadhi ya wanasiasa wazalendo nchini wameunga mkono msimamo wa
Tanzania uliotolewa na Rais Jakaya Kikwete kuhusiana na chokochoko
zinazoanzishwa na Rwanda na wamemtaka Rais wa nchi hiyo, Paul
Kagame, kukaa meza ya mazungumzo na waasi wa nchi hiyo walioko Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kwani amani haiwezi kutafutwa kwa njia
ya mtutu wa bunduki.
Akizungumza
na MAJIRA kwa njia ya simu jana Mhadhiri wa Chuo cha St. Agustino,
katika kitivo cha sayansi ya siasa, Prof. Mwesiga Baregu, alisema
ushauri alioutoa Rais Kikwete kwa Rais Kagame ni mzuri, hauwezi kuleta
athari zozote tofauti na kutumia mtutu wa bunduki kukabili waasi.
"Mimi
nikiwa kama mtaalam wa kutatua migogoro suala la mazungumzo ni njia
moja ambayo huwa inatumika mara kwa mara na inasaidia kuleta
amani," alisema na kuongeza;
"Kutumia mtutu wa bunduki haileti tija kwa mataifa yote mawawili, hivyo ni busara itumike njia ya mazungumzo."
Alitoa mwito kwa nchi jirani kushirikiana kutatua mgogoro uliopo kwa njia ya mazungumzo baina ya Rwanda na DRC.
Kwa
upande wake Mkuu wa Kitivo cha Elimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM), Dkt. Kitila Mkumbo, alisema anakubaliana na kauli ya Rais
Kikwete na anashangazwa na Rais Kagame ni kwa nini anachukizwa kuambiwa
azungumze na waasi.
"Maana
yake inaonekana hataki kushauriwa...ushauri huo ni kitu kizuri kinaweza
kuleta maelewano," alisema Dkt. Mkumbo. Alisema Rais Kagame, anaonekana
kama dikteta kutokana na kukataa kuambiwa ukweli na viongozi wenzake.
Alisema
kauli ya Rais Kikwete, aliyoitoa kwenye hotuba yake ya mwisho wa mwezi
wa saba hakugusia masuala ya vita na anaamini kwamba kwa karne hii sio
mwafaka nchi kuingia kwenye vita kwani nchi zina matatizo mengi ambayo
yanahitajika kupatiwa ufumbuzi.
"Alichoongea
Rais Kikwete, ni msimamo unaotakiwa kuungwa mkono na Watanzania kwani
yeye ndiye Amiri Jeshi Mkuu na hiyo ndiyo kauli ya nchi...hivyo
alichosema ni sawa," alisema Dkt. Mkumbo.
Mwenyekiti
wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda, alisema ameridhishwa na kauli
ya Rais Kikwete, kwani ametumia lugha sahihi katika kueleza hali halisi,
hivyo Watanzania wote wanatakiwa kumuunga mkono.
Alisema kwa hali ilivyo ni lazima Watanzania waungane katika masuala kama hayo ili kuleta mshikamano wa nchi.
Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP) Augustino Mrema, alisema anamuunga mkono Rais Kikwete, kwa kauli yake hiyo.
Alisema
Rais Kagame ameanza chokochoko dhidi ya Tanzania na kwamba hivyo,
ndivyo alivyoanza hata Idd Amin. "Siungi mkono vita vitokee, lakini kama
atatuchokoza basi tuwe wa mwisho kujibu mapigo," alisema Mrema.
Aliyekuwa
Mhadhiri UDSM, Dkt. Azaveri Lweitama, amezitaka nchi za Afrika
Mashariki kukaa chini ili kuangalia jinsi ya kutatua mgogoro huo.
Alisema
kuipiga Rwanda ni kazi ndogo sana, lakini hauwezi kumaliza tatizo kwa
kutumia bunduki na badala yake ni vyema nchi hizo zikaangalia namna ya
kumaliza mgogoro.
"Unajua
mnaweza kuingia katika vita mkamuondoa Rias wa Rwanda, lakini bado
mkatengeneza matatizo mengine kwa rais ajaye," alisema.
Alisema
Kongo kuna waasi wa Rwanda na hata Rwanda pia kuna waasi wa kutoka
Kongo, hivyo ni lazima kutafuta njia nzuri ya kutatua tatizo hilo.
Kwa
upande mwingine, Dkt. Lweitama, alivitaka vyombo vya habari kutopotosha
taarifa zinazozungumzia vita vikitokea hakuna mtu atakayebaki salama.
"Vyombo
vya habari vijitahidi kuandika habari zisizo za uchochoezi, kwani hata
ninyi pia ni Watanzania, naamini vita ikitokea hakuna mhariri wala
mwandishi atakayebaki salama," alisema.
Alisema
vyombo vya habari pia vina nafasi ya kukaa chini na kutafakari namna ya
kumaliza mgogoro kwa kuwa vina nafasi kubwa kwa mustakabali wa taifa.
Uhusiano
wa Tanzania na Rwanda unaelekea kupata mtikisiko baada ya Rais Kikwete
kutoa ushauri kwa Serikali ya Rwanda kuzungumza na mahasimu wao.
Rais
Kikwete alitoa ushauri huo kwa nia njema kwa kuwa bado anaamini kuwa
kama jambo linaweza kumalizwa kwa njia ya mazungumzo njia hiyo ni vyema
itumike.
Ushauri
ule aliutoa pia kwa Serikali ya Kongo na kwa Serikali ya Uganda. ambapo
katika mkutano ule Rais Yoweri Museveni wa Uganda aliunga mkono kauli
hiyo.
Tangu
atoe ushauri huo viongozi wa Rwanga wamekuwa wakitoa kauli za kejeli
dhidi ya Tanzania na Rais Jakaya Kikwete. Katika hotuba yake Rais
Kikwete, alisema uhusiano wa Tanzania na Rwanda unapitia katika kipindi
kigumu
-MAJIRA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: