Rais wa zamani wa Marekani Bw Bill Clinton Atua Dar Kiaina
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 9:37 AM
Rais
wa zamani wa Marekani Bw Bill Clinton pia alitembelea moja ya saluni ya
kutengenezea nywele ya Bi Zainabu Rashidi (kulia) ambaye ni mmoja wa
wanakikundi cha Upendo Hisa Group cha Vingunguti Mtambani, DSM jana.
Rais wa
zamani wa Marekani Bw Bill Clinton akizungumza na wanachama wa Upendo
Hisa Group alipotembelea kikundi hicho kilichopo Vingunguti jijini Dar
es Salaam jana. Kulia kwake ni Meneja Miradi wa Shirika la kimataifa la Plan
International Bw Paul Lusato na Catherine French Mkuu wa wafanyakazi
ofisi ya Mtendaji Mkuu wa Barclays.
Rais
wa zamani wa Marekani Bw Bill Clinton akipanda gari muda mfupi baada
ya kumaliza mazungumzo yake na Rais Jakaya Kikwete IKULU Jijini Dar es
Salaam Jana.Picha na Shabani Tolle na Mwananchi
----
Rais wa Mstaafu wa Marekani, Bill Clinton jana alifanya ziara
katika makazi ya watu duni eneo la Vingunguti, wilayani Ilala Dar es
Salaam, ambapo alikagua miradi midogomidogo ya wananchi inayofadhiliwa
na mfuko wake (Bill Clinton Foundation).
Clinton alitembelea eneo hilo akitokea moja kwa
moja Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam
(JNIA), alipowasili akiwa katika ziara ya nchi mbalimbali za Afrika
kukagua miradi inayoendeshwa na mfuko wake.
Katika eneo hilo rais huyo mstaafu alipokewa kwa
shamrashamra mbalimbali ikiwamo ngoma za kiasili huku baadhi ya wananchi
wakipigwa butwaa na kutoamini macho yao kwa kiongozi huyo kutembelea
makazi yao.Kwa habari zaidi Bofya na Endelea......>>>>
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: