MWILI WA MAREHEMU ALBERT MANGWEA WAWASILI NCHINI TAYARI KWA MAZISHI
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 7:34 AM
Waombolezaji wakibeba mwili wa Msanii wa muziki wa kizazi kipya Marehemu Albert Mangwea aka Ngwair wakati alipowasili leo alasiri kwenye uwanjua wa ndege wa Mawlimu JK Nyerere kwa ndege ya shirika la ndege la South Africa Airways kutoka nchini Africa Kusini alikokuwa akiishi, Albert Mangwea alifariki hivi karibuni nchini humo ambapo habari zisizo rasmi inadaiwa zinadai alikula chakula chenye sumu. Umati wa waombolezaji ukijaribu kulikaribia jeneza la msanii huyo huku watu wngine wakijaribu kupiga picha wakati mwili wake ulipowasili kwenye uwanja wa JK Nyerere leo. Ukiingizwa kwenye gari. Wapiga picha wakipiga picha. Wadogo zake na marehemu wakilia kwa uchungu. Waombolezaji mbalimbali wakiwa kwenye uwanja wa ndege wa JK Nyerere kuupokea mwili wa marehemu Albert Mangwea. Waombelezaji wengine walivalia fulana zenye picha ya marehemu huku wakionekana kuwa na majonzi P. Funk na wasanii wengine wakiwasili kwenye uwanja wa ndege wa JK Nyerere Mwanamuziki Lady Jay Dee akiwasili katika eneo hilo la mapokezi Ndugu na jamaaa wakiwa na majonzi huku wengine wakilia kwa uchungu. Hapa ni vilio tu wakimlilia Albert Mangwea Tipo na Bazo nao wameshiriki katika kuupokea mwili wa marehemu Albert Mangwea Edwin Temba na Abraham Mosi nao walijumuika katika mapokezi hayo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: