MAJAMBAZI WAUA MMOJA WAJERUHI WAWILI KWA RISASI WAPORA MAMILIONI YA SHILINGI ,IRINGA USIKU HUU
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 7:06 AM
Wananchi wa
Zizi la Ng'ombe mjini Iringa wakiwa kando ya gari ambalo marehemu alijificha
chini ya uvungu baada ya kupigwa risasi na majambazi hao
Mwili wa
marehemu huyo aliyetambulika kwa jina la baba Daudi ukiwa katika gari la
polisi
Huu ndio
mwili wa marehemu huyo baada ya kupigwa risasi na watu wanaosadikika kuwa
ni majambazi leo
Hapa penye damu
ndipo alipopigwa risasi
Askari polisi
wakiushusha mwili huo tayari kuuhifadhi chumba cha maiti Hospitali ya Rufaa ya
mkoa wa Iringa
Jeraha ambalo
kijana Patrick Vatung'a alilojeruhiwa kwa risasi
Majeruhi wa
risasi Dismas Nyaulingo kulia na Patrick Vatung'a wakiwa wodini
leo
.......................................................................................................................................
WAKATI kikao
cha wadau wa ulinzi kinataraji kufanyika kesho jumanne mkoani Iringa katika
ukumbi wa Siasa ni kilimo kikao kinacholenga kupambana na mtandao wa uharifu
mkoa ya kusini mwa Tanzania ,
Watu
wanaosadikika kuwa ni majambazi wakiwa na silaha wamevamia maduka eneo la
Zizi la Ng'ombe jirani na msikini mjini Iringa na kuua mtu mmoja na kujeruhi
wengine wawili kwa risasi kabla ya kupora fedha kiasi cha zaidi ya
shilingi milioni 2 .
Mashuhuda wa
tukio hilo wameueleza mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com na
mtandao wa www.matukiodaima.com baada ya kufika eneo la tukio kuwa majambazi
hao wakiwa zaidi ya wawili walivamia eneo hilo muda wa saa 1.30 usiku wa
leo .
Mashuhuda hao
walisema kuwa majambazi hao baada ya kufika katika eneo hilo la kibanda cha
M-Pesa kinachomilikiwa na Zamoyoni na kufanikiwa kumpora kiasi hicho cha
fedha kabla ya kuelekea katika duka moja wapo maarufu eneo hilo kwa lengo
la kuvamia na kupora.
Alisema Kevin
Kalinga kuwa chanzo cha kuuwawa kwa mwananchi huyo aliyetambuliwa kwa jina la
baba Daudi ni kutokana na kugoma kutii amri ya majambazi hao ambao walimkuta
akitoka dukani kununu sigara na kumtaka kukaa chini na baada ya marehemu
huyo kugoma kukaa chini ndipo walipomfyatulia risasi mwili jirani na pega na
kupelekea kutimua mbio na kujificha chini ya gari lililokuwa limeegeshwa
nje ya duka hilo gari aina ya Toyota Hilux lenye namba T 258 .
Hata hivyo
baada ya kupigwa risasi kwa mwananchi huyo wananchi waliokuwa karibu na eneo
hilo walianza kujikusanya kwa lengo la kuwavaa majambazi hao hali
iliyopelekea majambazi hao kuanza kufyatua risasi ovyo na kujeruhi
wananchi waliokuwa karibu na eneo hilo.
Kwa upande wao
majeruhi wa tukio hilo ambao wamelazwa wodi namba 5 katika Hospitali ya
Rufaa ya mkoa wa Iringa Dismas Nyaulingo ( 20) na Patrick Vatung'a(19)
walisema kuwa wao walikuwa wakiendelea kucheza Pool eneo hilo na baada ya
kusikia mlio kama wa baruti walianza kujihami kwa kukimbia na ndipo
walipokutwa na mkasa huo .
Nyaulingo
alisema chanzo cha majambazi hao kuanza kufyatua risasi onyo ovyo ni baada
ya wananchi kuanza kujikusanya kwa lengo la kupambana na majambazi hao
.
"Sisi tulikuwa
tukicheza mchezo wa Pool eneo hilo na baada ya hapo tulisikia mlio wa risasi
hewani na tukajua ni baruti na baada ya kusikia mlio wa pili ndipo tulipoanza
kutimua mbio kabla ya kupigwa risasi "
Nyaulingo yeye
amedai kujeruhiwa eneo la paja lake la mguu wa kushoto huku mwenzake
Vatung'a akijeruhiwa eneo la paja la mguu wa kulia.
Madaktari
waliowatibu majeruhi hao wamedai kuwa hali zao zinaendelea vizuri na
uwezekano wa kupona ni mkubwa zaidi.
Tukio hili
limetokea ikiwa ni siku chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kumpandisha
cheo aliyekuwa kamanda wa polisi mkoa wa Iringa (RPC) Michael Kamuhanda ambae
kutokana na kupanda kwake kwa cheo wakati wowote kuanzia wiki hii atauaga
rasmi mkoa wa Iringa na kwenda kuanza maisha mapya katika kiti cha enzi mpya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: