Jiwe linalotumiwa na kabila la Wasafwa linalopatikana mkoani Mbeya kwaajili ya kusaga nafaka mbalimbali lililopo katika nyumba ya kabila hiyo katika kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam.
WASAFWA KUNOGESHA KIJIJI CHA MAKUMBUSHO JIJINI DAR ES SALAAM
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 12:37 PM Akina
mama wa Kabila la Wasafwa wakiwa katika maandalizi ya utengenezaji wa pombe ya
asili ijulikanayo kwa jina la idadu itakayotumika katika tamasha la utamaduni
wa kabila hilo utakaofanyika katika kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam
kuanzia tarehe 22 hadi 24 mwezi huu. Wakwanza kushoto ni Katibu wa Wasanii wa
Kabila kundi la Mbeta Rose Alufani na kulia ni Kristina Mwaniengu ambaye
ametumwa na Machifu kwenda kuandaa nyumba za Asili za kabila hiyo kwaajili ya uzinduzi utakaofanyika kesho. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
Mtaalam
wa ujenzi wa nyumba za asili za kabila la wasafwa Helena Mwamengo akiendelea na
ujenzi ikiwa ni maandalizi ya uzinduzi wa tamasha la siku tatu la utamaduni wa
kabila hilo utakaofanyika kesho katika kijiji cha Makumbusho kilichopo jijini
Dar es Salaam.
Wakina
mama wa Kabila la Wasafwa wakiwa katika maandalizi ya utengenezaji wa pombe ya
asili ijulikanayo kwa jina la idadu itakayotumika katika tamasha la utamaduni
wa kabila hilo utakaofanyika katika kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam
kuanzia tarehe 22 hadi 24 mwezi huu. Wakwanza kushoto ni Katibu wa Wasanii wa
Kabila kundi la Mbeta Rose Alufani na kulia ni Kristina Mwaniengu ambaye
ametumwa na Machifu kwenda kuandaa nyumba za Asili za kabila hiyo kwaajili ya uzinduzi utakaofanyika kesho.
Sehemu ya kuishi kaya moja ya kabila la wasafwa ambayo
ina nyumba tatu tofauti yenye sehemu ya
kuishi familia, kufua chuma, kihenge cha vya kuhifadhia nafaka , boma la
ng’ombe na eneo la kufanyia tambiko iliyojengwa katika kijiji cha Makumbusho
kilichopo jijini Dar es Salaam.
Wasanii
wa kundi la Kabila la Wasafwa kutoka
mkoani Mbeya wakiwasili katika viwanja vya kijiji cha Makumbusho kilichopo
jijini Dar es Salaam kwaajili ya kushiriki tamasha la utamaduni wa kabila hilo
litakalofanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia tarehe 22 hadi 24 mwezi huu.
Wasanii
wa kundi la Kabila la Wasafwa kutoka
mkoani Mbeya wakiwasili katika viwanja vya kijiji cha Makumbusho kilichopo
jijini Dar es Salaam kwaajili ya kushiriki tamasha la utamaduni wa kabila hilo
litakalofanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia tarehe 22 hadi 24 mwezi huu. Mhamasishaji wa tamasha la utamaduni wa kabila la wasafwa kutoka
mkoani Mbeya Reddy Makuba (Kushoto) na Katibu wa Tamasha hilo Bahati Mbwete wakionyesha ghala la asili (kihenge) la
kuhifadhia nafaka linalotumiwa na kabila hilo linalopatikana mkoani Mbeya.
Mhamasishaji
wa tamasha la utamaduni wa kabila la
wasafwa kutoka mkoani Mbeya Reddy Makuba akionyesha kamba zinazotumika kufunga
mzinga wa kuhifadhia chakula unaotumiwa na
kabila hilo linalopatikana mkoani
Mbeya.Jiwe linalotumiwa na kabila la Wasafwa linalopatikana mkoani Mbeya kwaajili ya kusaga nafaka mbalimbali lililopo katika nyumba ya kabila hiyo katika kijiji cha Makumbusho jijini Dar es Salaam.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments: