KUWAT YAANDA FUTARI KATIKA WILAYA YA KIGAMBONI

 Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Al-Najem na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Hashim Mgandilwa wameshiriki katika futari iliyoandaliwa na Ubalozi wa Kuwait kwa ajili ya wananchi wa wilaya hiyo. Futari hiyo ilifanyika katika msikiti wa Daaru Salaam Kigamboni na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kidini na wananchi, na kuwajumuisha wanafunzi na mayatima wanaofadhiliwa na jumuiya za misaada za Kuwait zilizopo nchini.
Pembezoni mwa futari hiyo iliyotumbuizwa na kasida kutoka kwa watoto, Al-Najem alimkabidhi Mkuu wa Wilaya wa Kigamboni Hashim Mgandilwa zawadi.
Yafaa kueleza kuwa Ubalozi  wa Kuwait nchini utaendelea na program yake ya kufuturisha katika kipindi chote cha mwezi mtukufu wa  Ramadhan katika maeneo mbalimbali nchini.a






0 comments: