Naibu
Waziri Selemani Jafo akiwa na mtoto wa baba wa Taifa Madaraka Nyerere
pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Edo Mapunda, nyumbani kwa Baba
wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere Butiama.
Naibu Waziri Selemani Jafo akikagua ujenzi wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Mara mjini Musoma
Naibu Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo akikagua mradi wa Maji Katika wilaya ya Mbogwe mkoani Geita.
Naibu
waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(Tamisemi), Selemani Jafo amefanya ziara katika Mkoa wa Kigoma huku
akimuagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma kuunda timu ya uchunguzi juu
ya malalamiko ya wananchi kuhusu tuhuma za wizi wa madawa na ujenzi wa
wodi ya kina Mama ya Buhando na ujenzi ulio fanyika Katika zahanati
zingine ndani ya Manispaa ya kigoma
Hatua
hiyo ya Jafo ilitokana na kutoridhishwa na utendaji wa mkuu wa idara ya
Afya ya Manispaa ya Kigoma, John Maganga kutokana na usimamizi mbovu
wa miradi hiyo katika idara yake sambamba na kuwepo kwa malalamiko mengi
ya ubadhilifu wa madawa ndani ya Manispaa hiyo.
Jafo
alitembelea jengo la wazazi la Zahanati ya Buhanda ambapo hakuridhishwa
kabisa na maelezo ya ubora wa jengo hilo na mganga mkuu huyo kushindwa
kumpa Naibu Waziri maelezo ya kuridhishwa juu ya gharama za ujenzi wa
jengo hilo ambalo limejengwa chini ya kiwango na kuwepo mashaka makubwa
ya upotevu wa fedha nyingi katika ujenzi wa jengo hilo lililo zinduliwa
kinyemela na DMO huyo.
Kutokana
na simtofahamu hiyo Naibu Waziri amemtaka Katibu Tawala wa Mkoa wa
Kigoma kuunda timu ya uchunguzi na kwamba lengo la ziara hiyo ni kuleta
ufanisi katika kuwahudumia wananchi ndani ya halmashauri mbalimbali hapa
nchini.
Jafo
katika Mikoa minne ya Mara, Simiyu, Geita na Kigoma ambapo alizifikia
Halmashauri 19 na kuongea na watumishi zaidi ya 6000 pamoja na kukagua
miradi mbalimbali 25 ya barabara, maji, afya, elimu na ujasiliamali
imeleta tija sana kwa kuinua hamasa ya utendaji kazi kwa watumishi wa
halmashauri za wilaya.
Ziara
hiyo aliifanya baada ya kufunga Mkutano Mkuu wa 32 wa Jumuiya ya
Taasisi za Serikali za Mitaa (ALAT) uliofungwa rasmi tarehe 24 September
2016 mjini Musoma Mkoani Mara.
Ziara ya Naibu Waziri huyo ilianza tarehe 25 September hadi 30 September 2016 ambapo alikagua miradi na kuongea na watumishi.
Jambo
kubwa lililo sisitizwa Katika ziara hiyo ni umuhimu wa watumishi wa
halmashauri kufanya kazi kwa kuzingatia taaluma zao pamoja na kuweka
maslahi ya Taifa mbele.
Aliwataka
wakurugenzi kuwekeana malengo ya utekelezaji na wakuu wao wa Idara, na
wakuu wa idara kuwekeana malengo na watendaji wao wa chini wanao
waongoza.
Kadhalika,
Aliwataka watendaji wa halmashauri wabadilike katika utendaji wao.
Amewataka wakuu wa idara kutowabagua baadhi ya watumishi katika idara
zao.(P.T)
0 comments: