![]() |
| Washiriki wa mkutano wakifuatilia kwa makini |
MAALIM SEIF "ASHITAKI" DEMOKRASI KUVURUGWA ZANZIBAR; NI KWENYE MKUTANO HUKO WASHINGTON DC
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 8:29 AM
Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza kwenye mkutano maalum ulioandaliwa na Taasisi ya Kimarekani ya Centre for Strategic and International Studies (CSIS), Juni 13, 2016 kwenye makao makuu ya taasisi hiyo mjini Washington DC, nchini Marekani kujadli hali ya Zanzibar
Aliyekuwa Balozi wa Marekani nchiniTanzania, Mark Green ambaye kwa sasa ni Rais wa Taasisi ya International Republican Institute (IRI), akizungumza kwenye mkutano huo
Mkurugenzi wa Afrika katika Taasisi ya Centre for Strategic and International Studies (CSIS), Jennifer Cooke
Oktoba 25, Zanzibar na Tanzania kwa ujumla wake, walishiriki kwa uaminifu mkubwa kwenye uchaguzi mkuu ambao waangalizi wote wa uchaguzi kutoka SADC, AU, EAC, EU, Marekanina Uingereza, waliupongeza kuwa ulikuwa huru na wa haki.
“Matokeo kutoka vituo mbalimbali vya kupigia kura yalionyesha chama chetu (CUF), kiempata ushindi mkubwa, hata hivyo wakati tunasubiri mamlaka zitutangaze washindi, vikosi vya usalama viliizunguka hoteli ambayo ilikuwa ndio kituo cha kujumlisha kura za zoezi la kuhakiki na kujumlisha kura lilikuwa likiendelea.” Alisema Maalim Seif kwenye mkutano huo.
Alisema jambo la kustaajabisha zaidi, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, (ZEC), ambaye ni mteule wa CCM, alitangaza kufuta uchaguzi wote. Maalim Seif ameuambia mkutano huo kuwa CUF iko wazi na iko tayari kwa serkali ya umoja wa kitaifa ambayo inaweza kuundwa kwa sababu ya dharura iliyopo na kujiandaa kwenda kwenye uchaguzi chini ya taasisi huru ya kimataifa.
Baadhi ya waliohudhuria mkutano huo
Naibu Mkurugenzi anayeshughulika na Afrika Mashariki na Kusini wa Taasisi ya National Democratic Institute (NDI), Mercedeh Momeni
Subscribe to:
Post Comments (Atom)







0 comments: