Gari lenye namba za usajili T 709 AYW likiwa limeegeshwa pembezoni mwa Bahari ya Hindi baada ya kutofuata sheria za vivuko, gari hilo likiwa limesheheni barafu ambapo haikufahamika mara moja ilikuwa ikipelekwa wapi. Inakadiriwa mnamo majira ya saa 11: 25 alfajiri, gari hilo likiingia katika kivuko cha MV Lami mapema leo hii lilinasa kwenye mlango wa kivuko hicho kwa kile kinachodaiwa ni kuzidisha mzigo mkubwa na kusababisha kunasa katika mlango huo na kusababisha MV Lami kusukumwa na gari hilo na ikabidi barafu hiyo kupakuliwa kisha gari hilo kuvutwa na na gari lingine lenye namba za usajili T 661 AXB na kupelekwa Kituo cha Polisi cha Kigamboni Jijini Dar es Salaam (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI, WCF WAENDELEA NA KAMPENI YA KUELIMISHA MADAKTARI KUHUSU FIDIA KWA WAFANYAKAZI WAPATAPO MADHARA KATIKA KAZI
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 10:51 AM
NA K-VIS
MEDIA/Khalfan Said
Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), umeendelea na
kampeni yake ya kutoa mafunzo kwa madaktari ili kujenga uelewa wa kufanya tathmini ya ajali na magonjwa ayapatayo mfanyakazi yanayotokana
na kazi safari hii ikihusisha madaktari kutoka mikoa mitano ya ambayo ni Arusha
Tanga, Manyara, Kilimanjaro na Singida.
Mafunzo
hayo yaliyofunguliwa Mei 30, 2016 na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira,
Vijana na Watu Wenye Ulemavu. Anthony Mavunde, huko jijini Arusha, ni
muendelezo wa mafunzo mengine kama hayo yaliyotolewa wiki mbili zilizopita
jijini Dar es Salaam, ambapo madaktari kutoka mikoa ya Dares Salaam, Pwani, Morogoro,
Dodoma, lindi na mtwara walihudhuria.
WCF
imechukua hatua hiyo ili kujiandaa na UTOAJI WA Mafao kwa mara ya kwanza tangu
uanzishwe ifikapo Julai mwaka huu wa 2016.
DIWANI WA KATA YA MABATINI JIJINI MWANZA AZINDUA KIKUNDI CHA USHIRIKIANO
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 10:46 AM
Diwani wa Kata ya Mabatini Jijini Mwanza, Deus Mbehe (Chadema) akikata utepe kama ishara ya Uzinduzi wa Kikundi cha Kusaidiana cha USHIRIKIANO PEOPLE'S kinachoundwa na Wanachama zaidi wa 100 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Kata ya Mabatini.
Na BMG
Kikundi hicho kiliundwa baada ya kuibuka stofahamu ya wananchi kusaidiana katika masuala mbalimbali ikiwemo misiba, baada ya baadhi ya wanachama wa chadema kutengwa katika shughuli za misiba katika Kata ya Mabatini.
Uzinduzi wa Kikundi hicho ulifanyika katika Ukumbi wa Kilimanjaro uliopo Mabatini Stand huku ukiambatana na harambee kwa ajili ya kukiimarisha kikundi ambapo diwani wa Kata ya Mabatini ambae alimwakilisha diwani wa Kata ya Butimba, akichangia shilingi Laki Tano huku wageni wengine waalikwa wakifanikisha harambee hiyo kufikisha shilingi Milioni Moja, laki moja na elfu sabini.
Wanachama nao waliahidi kila mmoja kuchangia shilingi elfu kumi, pesa ambazo kwa ujumla zitasaidia kukabiliana na mapungufu yanayokikabili kikundi hicho. Mapungufu hayo ni pamoja na viti 120, sufuria nne, turubai mbili pamoja na sahani 200 lengo likiwa ni kujiimarisha katika mahitaji mbalimbali yanayohitajika katika shughuli mbalimbali.
Mwenyekiti wa Kikundi hicho chenye wanachama 103 hadi sasa, Salma Ibrahim, amewasihi wananchi wengine kujiunga na kikundi ili kuongeza nguvu ya kusaidiana katika masuala mbalimbali ikiwemo sherehe, misiba na kuinuana kiuchumi bila kujali itikadi zao za kisiasa.
MADAKTARI WAPATA MAFUNZO YA KUREKEBISHA MIGUU ILIYOPINDA
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 10:44 AM
Daktari
Bingwa wa Upasuaji wa Mifupa Dk.Richald Gellman kutoka Califonia - San
Fransisco Marekani (kushoto), akiwaonesha kifaa Chuma, maalumu kinacho
tumika kufanya marekebisho ya mifupa iliyo pinda baada ya kuunga vibaya
au kutounga kabisa, madaktari mbalimbali kutoka nchi mbalimbali ,
Kenya, Burundi, Rwanda, Zambia, DRC Congo, Nigeri, Zimbabwe na wenyeji
wao Madaktari wa Taasisi hiyo wamehudhuria Mkutano huo utakaomalizika
Juni 3, 2016 , unaendelea katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Upasuaji wa
Ubongo na Mifupa ya Fahamu Muhimbili (MOI)
Dar es Salaam leo. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
Pichani ni baadhi ni vifaa
Madaktari Bingwa wakiwa katika chumba cha mikutano katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Moi
Mmoja wa Maktari Bingwa wa Taasisi hiyo mwenye miwani mbele Dk. Moonlight Mnyenye akiandika jambo wakati wa mkutano huo
MKE WA RAIS MAMA JANETH AWATAKA WATANZANIA KUWASAIDIA WAZEE NA WATU WENYE ULEMAVU
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 9:52 AM
Mke wa
Rais Mama Janeth Magufuli akimkaribisha Mke wa Waziri Mkuu Mama Marry
Majaliwa Ofisini kwake Magogoni jijini Dar es Salaam. Mama Majaliwa
alifika Ofisini hapo ili kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na
mke wa Rais.

Mke wa
Waziri Mkuu Mama Marry Majaliwa akisaini kitabu cha wageni mara baada ya
kuwasili katika Ofisi ya Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli Magogoni
jijini Dar es Salaam.

Mke wa
Rais Mama Janeth Magufuli akimuonesha Mke wa Waziri Mkuu Mama Marry
Majaliwa mafuta maalumu yanayotumiwa watu wenye ulemavu wa ngozi Albino
ambayo atayagawa hivi karibuni kwa baadhi walemavu wa ngozi katika
maeneo mbalimbali nchini. Pia Mke wa Rais mama Janeth amewaomba
watanzania kuwajali Wazee na watu wenye ulemavu wa ngozi. PICHA NA IKULU
SERIKALI KUANZISHA BENKI YA MAENDELEO YA VIWANDA NCHINI
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 9:39 AM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizindua nembo mpya ya Tuzo za Rais kwa Wazalishaji bora wa Viwanda PMAYA The President’s Manufacure of the Year pamoja na Mwenyekiti wa Wenyeviwanda Tanzania CTI Dkt. Samwel Nyantahe katika Ukumbi wa Serena Jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU / HASSAN SILAYO-MAELEZO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wadau mbalimbali wa CTI na kutoka Sekta ya Viwanda nchini kabla ya kutoa Tuzo za Rais kwa viwanda vilivyofanya vizuri kwa mwaka 2015 katika Ukumbi wa Serena Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la wenye Viwanda nchini Leodgar Tenga mara baada ya kumalizika kwa hafla hio ya utoaji Tuzo za Rais.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na baadhi ya Wadau wa Viwanda nchi mara baada ya kumalizika kwa hafla hio ya utoaji Tuzo za Rais.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimia na Waziri wa Nishati na Madini wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam.(P.T)

Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembelea
baadhi ya mabanda ya bidhaa zinazotoka viwandani wakati wa hafla ya
utoaji tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo
Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa
Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akiongea na wadau
wa sekta ya Viwanda wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa
wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 na kuwataka kuunganisha
nguvu katika uanzishaji na uendelezaji wa viwanda nchini ili kuongeza
upatikanaji wa bidhaa nchini hali itakayopelekea kukuza uchumi wa nchi
na kuongeza ajira kwa watanzania.

Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizindua nembo
ya shirikisho la viwanda nchini wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais
kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es
Salaam kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles
Mwijage, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda
Tanzania (CTI) Leodger Tenga na wa pili ni Mwenyekiti wa Shirikisho la
Wamiliki wa Viwanda nchini Tanzania (CTI)Dr.Samuel Nyantahe.

Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na
wadau wa sekta ya viwanda nchini(hawapo pichani) na kuwaahidi kuwaunga
mkono katika harakati za kuendeleza sekta ya viwanda ikiwamo kuanzisha
banki ya maendeleo ya viwanda nchini itakayosaidia kutoa mikopo yenye
riba nafuu kwa wale wenye nia ya kuanzisha viwanda.

Wadau wa
Sekta ya Viwanda nchini wakimsilkiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais
kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es
Salaam.

Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa tuzo kwa
washindi wa tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka
2015 leo Jijini Dar es Salaam.

Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa tuzo kwa
washindi wa tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka
2015 leo Jijini Dar es Salaam.

Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika
picha ya pamoja na washindi wa tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa
Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam.

Raila Odinga
Rais wa
Kenya Uhuru Kenyatta anafanya mazungumzo na kiongozi wa upinzani nchini
humo Raila Odinga ili kuondoa wasiwasi wakati ambapo taifa hlo
linajiandaa kwa uchaguzi mwaka mkuu ujao.
Bw Odinga
alikatiza ziara yake ya kushiriki katika mazishi kusini magharibi mwa
eneo la Natol ili kuhudhuria mkutano huo wa Uhuru Kenyatta katika mji
mkuu wa Nairobi.
''Nilipokea
simu kutoka ikulu ya mkutano na rais Uhuru Kenyatta.Naomba ruhusa yenu
watu wa Narok nielekee kuzungumza naye,alinukuliwa na gazeti la Daily
Nation akiwaambia waombolezaji.Nitatangaza kwa Wakenya iwapo
tumekubaliana na iwapo hatujakubaliana pia nitawaelezea'', aliongezea bw
Odinga.

Uhuru Kenyatta
Muungano
wa upinzani nchini Kenya Cord umeapa kuhudhuria mkutano jijni Nairobi
hapo kesho,licha ya kwamba serikali ilitangaza kupigwa marufuku.
Watu kadhaa wameuawa katika ghasia kati ya polisi na wafuasi wa upinzani wanaopigania mabadiliko ya sheria ya kupiga kura. BBC
NAIBU SPIKA DKT. TULIA ACKSON AKUTANA NA WAANGALIZI WA UCHAGUZI KUTOKA JUMUIYA YA ULAYA
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 9:19 AM
Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Dkt. Tulia Ackson
(kulia) akizungumza jambo na Waangalizi wa Uchaguzi uliofanyika Oktoba 25, mwaka jana (2015), kutoka Umoja wa Ulaya.
Judith Sargentini (kushoto) na Balozi wa Umoja huo . Roeland Van De
Geer (katikati) waliofika Ofisini kwake Dodoma leo Mei 31, 2016.

Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson
akiwasikiliza waangalizi wa Uchaguzi Mkuu kutoka Umoja wa Nchi za Ulaya (EU)
waliofika Ofisini kwake kuwasilisha Taarifa ya Umoja huo kuhusu Uchaguzi Mkuu
uliofanyika nchini Oktoba 25, 2015.

Waangalizi
wa Uchaguzi Mkuu kutoka Umoja wa Nchi za Ulaya (EU) wakizungumza na Naibu Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson (hayupo pichani)
ofisini kwake Dodoma.

Balozi
wa Umoja wa Ulaya Mhe. Roeland Van De Geer (kulia) akimkabidhi Naibu Spika wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Tulia Ackson Taarifa ya
miradi inayotekelezwa na Umoja wa Ulaya nchini Tanzania.

Naibu
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Tulia Ackson
(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Waangalizi wa Uchaguzi kutoka
Umoja wa Nchi za Ulaya (EU) waliomtembelea Ofisini kwake leo mjini Dodoma. (PICHA NA ARON MSIGWA NA FATMA SALUM-MAELEZO).
![]() |
| Tanzania President, Dr. John Pombe Magufuli |
From Freddy Maro
Tanzania Embassy Addis Ababa Ethiopia.
TANZANIA has been elected a Chair of the Governing Council
of African Minerals and Geosciences Center (AMGC) during its 36th
annual meeting held at United Nations Economic Commission for Africa (UNECA)
conference Centre in Addis Ababa, Ethiopia over the weekend.
Tanzania was represented by The Permanent Representative of Tanzania to
the United Nations Economic Commission for Africa (UNECA) and Ambassador of
Tanzania to Ethiopia H.E. Naimi Hamza Aziz who read the Member country’s
statement on behalf of Minister for Minerals and Energy Prof. Sospeter Muhongo.
In her speech, ambassador Naimi urged Member
States to consider the development of other strategic minerals such as graphite;
lithium and Rare Earth Elements (REEs) which she said were not only
economically viable but also important.
“The mining sector is seriously affected by the
drop of mineral prices in the global market especially for precious and base
metals which are mostly mined by our countries. The decline of mineral price
has resulted to low exploration activities to Member States especially my
country, which has led to the decline of income to the centre (AMGC),” she
said.
The Tanzania Permanent Rep. further advised the
African Minerals and Geo-Sciences Center(AMGC) to be more creative and
diversify its economic activities for its future and sustainability.
In order for Member States to catch up with
fast growing technologies, the Ambassador said it was high time for AMGC to
invest in Research and Development (R&D), in which the findings would be
shared with Member States for optimal utilization of mineral rich resources
found in the continent.
She said
that Member States should endeavor to make AMGC a truly Pan African Center of
Excellence and to achieve this more needs be done in terms of marketing, which
would increase the center’s visibility and capability and promote the
tremendous work it does.
“It is therefore crucial that Member States pay
their respective annual contributions to the center, in order to allow it to
operate more efficiently and effectively and successfully implement its
programs and activities,” She emphasized.
Ambassador Naimi said Tanzania was very proud
to host the AMGC and stands committed to continue to honor and fulfill its
obligation which aims inter alia, to facilitate and ensure that the center
fulfills its mission and mandate to serve all African countries.
In his opening speech the outgoing AMGC
chairman who is also The Ethiopian Minister of Mines, Petroleum and Natural Gas
H.E. Tolesa Shagi said Ethiopia and many African countries were adopting
effective mineral management policies and strategies for the exploitation of
mineral resources which were vital in boosting economic growth.
“The Mining sector in Ethiopia is providing support
for the development of small and medium scale and artisanal mining enterprises
and encourage greater participation of women in mining activities as a strategy
for enhancing the development impact of mineral resources,” he said.
The Minister highlighted challenges facing
mining industry in Ethiopia and Africa in general including shortage of
capacity in negotiating, administering and monitoring the mining contracts as
well as lack of sufficient geo-science information.
He said for African countries to overcome the
challenges facing the mining industry they should opt for coordinated efforts
as envisaged in the Africa Mining Vision (AMV) that was adopted by African
Heads of States in February 2009, the long term goal of the vision is to create
a Transparent Equitable and optimal exploitation of mineral resources to
underpin broad-based sustainable growth and socio-economic development.
Speaking during the same occasion, the Deputy
Executive Secretary and Chief Economist of ECA said that the Economic
Commission for Africa(ECA) was acutely aware of the strategic importance of the
AMGC as a partner to African Countries to collectively implement a
transformative agenda for mineral resources development which would be
instrumental for sustainable development.
African Minerals and Geosciences Centre (AMGC)
formerly known as the Southern and Eastern African Mineral Centre (SEAMIC)
started as a sub-regional development Centre for Eastern and Southern African
nations namely, Angola, Comoros, Ethiopia, Mozambique, Tanzania and Uganda.
The Centre is located in Kunduchi Dar es Salaam
Region, Tanzania.
WAZIRI MKUU MAJALIWA ATUA ARUSHA KUFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA "AFRICA WORLD HERITAGE"
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 7:55 AM
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Maliasili
na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe (kulia) na Mkuu wa mkoa wa Arusha,
Felix Ntibenda Kijiko (katikati) baada ya kuwasili kwenye uwanja wa
ndege wa Arusha May
30, 2016 ambako May 31, 2016 anatarajiwa kufungua mkutano wa Kimataifa
wa
'Africa World Heritage' kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha
Arusha -AICC. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
RAIS MAGUFULI AMTEUA JAJI KIONGOZI SHAABAN LILA KUWA JAJI WA MAHAKAMA YA RUFANI, MAKINDA NAYE ATEULIWA KUWA MWENYEKITI WA BODI YA NHIF
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 7:53 AM
Jaji Kiongozi Shaaban Lila, sasa ateuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani nchini

Bi. Anna Semamba Makinda, Mwenyekiti mpya wa bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, NHIF

NAIBU KATIBU MKUU WA CCM-BARA, RAJABU LUHWAVI AENDELEA NA ZIARA YAKE YA KUHAMASISHA CHAMA, YUKO MKOANI MANYARA
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 7:35 AM
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akiagana na Afisa Tawala wa mkoa wa
Manyara Eliakim Maswi baada ya mazungumzo na mkuu wa mkoa huo Joel Bendera
(Katikati), alipoenda ofisini kwa mkuu huyo wa mkoa, mjini Babati leo Mei 30,
2016.
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi (kulia) akizungumza na Mkuu wa
mkoa wa Manyara Joel Bendera alipoenda ofisini kwa mkuu huyo wa mkoa,
mjini Babati leo Mei 30, 2016.
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM,-Bara, Rajab Luhwavi akisalimiana na Mwenyekiti wa
CCM mkoa wa Manyara, Luccas Ole Mukusu, alipowasili kwenye Ofisi ya CCM
mkoa huo, mjini Babati, leo Mei 30, 2016. Kushoto ni Katibu wa CCM mkoa
huo Ndegesu Ndekobali.
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM,-Bara, Rajab Luhwavi akisalimiana na baadhi ya
watumishi wa CCM mkoa wa Manyara, alipowasili kwenye Ofisi ya CCM mkoa
huo, mjini Babati, leo Mei 30, 2016. Kushoto ni Katibu wa CCM mkoa huo
Ndegesu Ndekobali.
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akisaini Kitabu cha wageni
katika Ofisi ya CCM mkoa wa Manyara, baada ya kuwasili mjini Babati leo
Mei 30, 2016. Kushoto ni Katibu wa CCM wa mkoa huo, Ndegesu Ndekobali.
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi akisaini Kitabu cha wageni
katika Ofisi ya CCM mkoa wa Manyara, baada ya kuwasili mjini Babati leo
Mei 30, 2016. Kushoto ni Katibu wa CCM wa mkoa huo, Ndegesu Ndekobali.
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rajab Luhwavi (kulia) akizungumza na Mkuu wa
mkoa wa Manyara Joel Bendera alipoenda ofisini kwa mkuu huyo wa mkoa,
mjini Babati leo Mei 30, 2016. Kushoto ni Afisa Tawala wa mkoa huo,
Eliakim Maswi.
Katibu wa CCM wa mkoa wa Manyara Ndekobali akishukuru baada ya mazungumzo hayo
wakiagana baada ya mazungumzo. (PICHA ZOTENA BASHIR NKOROMO WA CCM)
Subscribe to:
Posts (Atom)












0 comments: