Posted by
khamisimussa77@gmail.com
at
8:48 AM
Mbunge wa Kawe na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Halima Mdee.
Mbunge wa
Kawe, Halima Mdee na wenzake 8 leo wamepata dhamana katika Mahakama ya
Kisutu, Dar. Kesi yao kutajwa tena Oktoba 21, 2014.
Siku ya
jana washtakiwa hao walipanda kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi Kaluyenda
na kusomewa mashtaka mawili na Wakili wa Serikali Mkuu, Kangola
aliwataja washtakiwa kuwa ni Mbunge wa Kawe, Mdee, Rose Moshi, Penina
Peter, Anna Linjewile, Mwanne Kassim, Sophia Fanuel, Edward Julius,
Martha Mtiko na Beatus Mmari.
Mdee na
wenzake hao wanashitakiwa kwa makosa mawili la kwanza washtakiwa wote
wanadaiwa Oktoba 4 mwaka huu, Mtaa wa Ufipa wilayani Kinondoni,
walikaidi amri ya Ofisa wa Polisi SP Emmanuel Tillf iliyowataka
watawanyike.
Shtaka la
pili washtakiwa wote wanadaiwa Oktoba, mwaka huu, maeneo ya mtaa wa
ufipa jijini Dar es Salaam wakiwa na lengo moja walikusanyika kinyume na
sheria wakitaka kwenda ofisi ya rais
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments: