Tunakiwa kumaliza mechi Dar es Salaam
Mimi ni mshambulizi wa kati
Timu
ya Soka ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars itacheza na ile ya Msumbiji,
Black Mambas mwishoni mwa wiki ijayo katika uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Stars
chini ya Mwalimu,Martin Nooij tayari imeingia kambini,Tukuyu Mbeya,
mwanzoni mwa wiki hii ikitokea nchini Botswana ilipokuwa na kambi ya
mafunzo ya wiki mbili.
Mchezo
huo wa kwanza wa mtoano kuwania nafasi ya kufuzu katika hatua ya
makundi kuwania tiketi ya kucheza michuano ya Mataifa Afrika, AFCON
2015, nchini Morocco unataraji kuwa mgumu kwa kila upande.
Msumbiji
iliifunga Stars katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi kuwania
nafasi ya kufuzu kwa fainali za Afrika mwaka 2008 nchini Ghana.
Stars
ililazwa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza wa mashindano katika uwanja wa
Taifa, septemba, 2007, bao maridadi la mpira wa kichwa lililofungwa na
aliyekuwa nahodha wa Msumbiji, Tico Tico.
Miaka
miwili iliyopita timu hizo zilikutana katika michezo ya mtoano kuwania
kufuzu kwa fainali zilizofanyika nchini Afrika Kusini,2013 na Stars
iliondolewa kwa changamoto ya mikwaju ya penalti.
“
Mechi ya wiki ijayo itakuwa ngumu, naamini Msumbiji nao watakuja wakiwa
wamejipanga kuhakikisha hatupati ushindi katika uwanja wa nyumbani”
anasema mshambulizi, Mbwana Samatta ambaye alipoteza mkwaju wa mwisho wa
penalti na kuitupa nje Stars.
Msumbiji
walilazimisha sare ya bao 1-1 katika uwanja wa Taifa,wiki mbili
baadaye, Stars iliyokuwa chini ya Kim Poulsen ilipata matokeo kama hayo
kabla ya kuchapwa katika mipigo ya penalti.
Samatta,
mfungaji bora wa kombe la Shirikisho barani Afrika 2013 akiwa na klabu
yake ya TPMazembe ya DRC, amekuwa na uzoefu wa kutosha sasa kuhusiana na
michezo ya kimataifa ya mtoano bila shaka mshambulizi huyu anaweza
kuisaidia zaidi Tanzania katika mchezo ujao kutokana na mafanikio ambayo
tayari yameonekana wakati akiwa katika uwakilishi wa klabu yake.
“
Muhimu siyo kutazama mchezaji mmoja mmoja au timu inacheza kwa kiwango
gani, ndiyo wakati mwingine mashabiki wanakuwa wakifurahia mpira
tunaocheza, lakini kitu muhimu zaidi ni kufunga mabao ya kutosha”
anasema, Samatta wakati alipofanya mahojiano na mtandao huu.
Kila
mtu anafahamu kuwa mchezo huo utakuwa mgumu, lakini umefikia wakati
ambao Stars inatakiwa kufuzu kwa michuano CAN, katika miaka minne
iliyopita timu imeshindwa kufikia lengo hilo katika michuano mitatu
tofauti, kuna kitu chochote kimepatikana kutoka kwa wachezaji? Wachezaji
wamejifunza nini kutoka katika michuano iliyopita?
“
Kuna kitu kimeongezeka kwa timu na kwa mchezaji mmoja mmoja, hivi sasa
wachezaji wa Taifa Stars wanajiamini sana wanapokuwa mchezoni, pasi ni
nzuri na unakutana hata katika eneo letu la ulinzi wachezaji wanakuwa na
utulivu, wanapasiana bila hofu yoyote".
"Tunacheza
vizuri nyumbani na huwa tunafanya hivyo katika michezo ya ugenini”
anasema mshambulizi huyu namba moja wa TP Mazembe. Na kuongeza ;”
Kinachotakiwa ni ‘Kutwist’ vichwa vya wachezaji ili waelewe majukumu
yao na kuifahamu vizuri timu pinzani, hili ni jukumu ambalo linatakiwa
kufanywa na waandishi wa habari pia. Inasaidia kuwafanya wachezaji
waelewe mchezo ulio mbele yao”
Tanzania
ilitolewa na Msumbiji miaka miwili iliyopita katika michuano kama hii,
ili kufuzu kwa fainali za Morocco,Stars inalazimika kuitoa kwanza ,Black
Mambas ili kuungana na timu za Zambia, Niger na Cape Verde kuwania
tiketi mbili za kundi hilo ambazo zinaweza kupatikana, lakini kwa kulipa
kisasi cha timu hiyo ya Kusini mwa Afrika
“
Kwanza ni lazima tumalize mechi Dar es Salaam,hatutakiwi kufanya kama
wakati ule tuliposhindwa kupata ushindi katika uwanja wa nyumbani”
anasema Samatta ambaye amekuwa akipangwa katika nafasi ya mshambulizi wa
pembeni au mshambulizi wa pili katika timu ya Taifa.
Samatta
amefunga mabao sita katika michezo17 inayotambulika na FIFA kuanzia
mwaka 2011 alipoitwa kwa mara ya kwanza na kocha Jan Poulsen.
Poulsen
alimuingiza kikosini akiwa na miaka 18 na haraka akamuamini kama
mshambulizi wa kwanza katika kikosi chake. Alifunga mabao manne ndani ya
mwaka mmoja aliofanya kazi na Jan lakini tangu timu hiyo ikinolewa na
Kim Poulsen, Samatta amekuwa ‘butu’ katika ufungaji japokuwa amekuwa
mfungaji wa kutegemewa sana katika klabu yake ya TP Mazembe.
“
Nachoweza kusema nimekuwa makini na mtulivu, na wakati mwingine huwa
nasema ni bahati kutoka kwa Mungu. Mimi ni ‘ mwanajeshi wa mbele’
mshambulizi wa kwanza kabisa, hivyo ndivyo ninavyotumika katika klabu
yangu na nimekuwa nifunga mabao ya kutosha kutokana na kupangwa katika
nafasi hiyo nayoipenda. Mchezaji huwezi kujichagulia nafasi ya kucheza
katika timu, mahitaji ya Mwalimu ndiyo jambo la msingi"
"
Napenda kucheza katika nafasi yoyote nayopangwa Stars kutokana na mfumo
wa kocha anavyotaka” anasema Samatta amekuwa akipangwa nyuma ya
mshambulizi, John Bocco katika timu ya Taifa.
“
Siwezi kusema kama huwa nina furaha au laa!, naweza kufurahia kama
nikipangwa katika wingi ya kushoto, au mshambulizi wa kwanza na si nyuma
ya mshambuliaji wa kwanza kwa sababu nakosa nafasi ya kuuchezea mpira”
Naweza kufurahi km nikicheza km winga ya kushoto au streka sio nyuma ya streka.
Mechi
17 za Fifa, mabao sita inamaanisha nini kwa mshambulizi huyu
unayependwa nchini Tanzania. “ Bado sijafanya nachopenda kufanya, lakini
inatokana na ufinyu wa michezo, bado nina imani wakati upo wa kufanya
mambo makubwa kwa Taifa langu, kufunga mabao kadri inavyowezekana ili
kukaribiana idadi ya michezo”anasema mchezaji huyo anayedai anafunga
mabao mengi katika klabu yake kutokana na kuzungukwa na wachezaji wengi
wa kulipwa, kitu ambacho hakipo kwa Stars.
Samatta
ametoa wito kwa mashabiki wa soka nchini kuwapa sapoti wachezaji wao
katika muda wote wa mchezo na kuwafanya wageni wao kuingia mchecheto.
Hivyo ndivyo mazingira ya uwanja yanavyokuwa katika uwanja Stade de TP
Mazembe wakati timu ngeni zinapokuwa zikitembelea katika uwanja huo.
“
Mashabiki wana mchango mkubwa sana katika mchezo kama huo,wanatakiwa
kuinuka katika viti vyao na kuimba wimbo wa Taifa pamoja na wachezaji.
Kuishangilia timu muda wote ili kuwafanya Msumbiji wajione wapo ugenini
hasa. Waje kwa wingi uwanjani siku ya mchezo kuipa sapoti timu”
0714 08 43 08
Chanzo:shaffihdauda.com
0 comments: