Maamuzi Gani Nichukue Dhidi ya Ndoa Yangu?
Mimi ni
mama wa
watoto wawili, nimefunga ndoa miaka saba iliyopita, mwanzo kabisa maisha
yangu ya mahusiano hayakuwa mazuri hata kidogo, first of all niliwahi
kubakwa nikiwa na umri wa miaka 15, baada ya hapo niliishi maisha ya
tabu sana mpaka nilipokuwa mkubwa na kuweza kujitambua.
Nillianza maisha ya mahusiano nikiwa na miaka 21 na mwanaume
niliyetokea kumpenda na kuamini yeye ndio atakayenifuta machozi na
huzuni zangu.
Mambo hayakuwa hivyo kwani miaka miatatu ya mahusiano yetu alienda
oversizi na kuniacha na pia kuamua kukata mawasiliano kabisa. Nilibaki
na kovu na maumivu niliyokosa tiba. Nilimtafuta bila mafanikio na kuamua
kumove on na maisha yangu,ingawa ilikuwa ni ngumu sana.
Baada ya hapo nilikutana na mwamaume ambaye sikujua kama ni kweli
nampenda kwani siku zote nilipokuwa nae nilikuwa namuwaza X wangu
aliyeniacha bila kusema neno lolote.
Mwanaume huyu mwanzo sikumuelewa kabisa kwanza alikuwa mgomvi na
mkorofi kwa watu dakika mbili alishabadirika haeleweki kama kinyonga ,police kwake ilikuwa ni kama nyumbani.
Nyimbo zake mara
nyingi zilikuwa ni za kina Tupac ,Snopy D na wale aina ya magang star
Ingawa alikuwa msomi na kazi nzuri,na maisha yake mpaka sasa bado miziki
yake ndio hiyo ,starehe kwake hataki kuacha wala kupunguza.
Niliamini atabadilika ingawa nilikuwa nakwazika sana kuwa nae
alinifundisha kunywa Pombe ,Ok nikawa mnywaji mzuri na ili niwe nae
Kimapenzi niliona ninywe kwanza ndio nakuwa huru na hayo ndio yakawa
maisha yangu..Tuliendelea na mahusiano ya muda mrefu hatimaye nilianza
kumzoealakini si kumpenda ,
Tukiwa tayari ndani ya mahusiano nilishika mimba na tukakubaliana
kuanza kukaa pamoja ,taratibu za mahali zilifanyika na nikahama rasmi
lakini kwa sababu jamaa alikuwa mtu wa starehe alikuwa akiniacha na
kurudi usiku wa manane amelewa mara anitukane na sikuona kama alikuwa
ananithamini na hali yangu ya ujauzito chuki moyoni ikawa inazidi siku
hadi siku.
Ingawa kuna wakati nilikuwa naona kama ananipenda .Baada ya
kujifungua tulianza taratibu za ndoa lakini moyoni mwangu nikijua kabisa
mwanaume huyu sina mapenzi nae hata kidogo.Na nilikuwa najiuliza kwanini nafunga ndoa?
Ingawa kuna vitu vingine vilikuwa kama najifosi kufanya. Tulifunga
ndoa takatifu nakuanza kuishi kama mke na mme ,na mungu akatujaalia
kuongeza mtoto mwingine wa kiume lakini system yangu ni mpaka ninywe
ndio nakuwa na hisia za kuwa na mme wangu.
Ndani ya ndoa yangu nimekuwa nikiishi kwa kujifanya nampenda mme
wangu ingawa hizo hisia sijawahi kuzipata hata kidogo ,nimekuwa nikilia
na kujutia maamuzi yangu sina furaha ,ni mnyonge ,for the sake of my
kids ndio napata faraja kidogo.
Kila siku zinavyoenda nazidi kuchanganyikiwa mwenzenu nitaishi hivi
mpaka lini nifanye nini ili nipate amani ya roho,? maana hii pretend sasa imenichosha. Nakosa usingizi usiku kucha.
Ni mengi ya kuelezea lakini kwa hapa moyo wangu unazidi kuwa mnyonge
Nisaidieni juu ya hili
By Ndoa Yangu
0 comments: