TUKIO LA UFOO SARO, BADO YU CHUMBA CHA DHARULA


 Mwandishi wa habari wa Kituo cha ITV na Redio One, Ufoo Saro, hadi sasa bado yupo katika Chumba cha Dharula katika Hospitali ya Muhimbili, akiendelea kupatiwa matibabu kufuatia tukio la kupigwa risasi na mtu anayedaiwa kuwa Mchumba wake alfajiri ya leo huko maeneo ya Kibamba, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. 
 Kamanda Suleiman Kova, akizungumza na waandishi wa habari wakati akiwa eneo la Hospitali ya Muhimbili leo mchana alipofika kujua kinachoendelea juu ya tukio hilo na maendeleo ya mgonjwa. 
 Baadhi ya waandishi wa habari waliofika Hospitalini hapo leo kwa ajili ya kujaribu kumuona, lakini haikuwezekana kuruhusiwa kutokana na mgonjwa huyo kuendelea na matibabu katika chumba cha dharula.
 Baadhi ya wafanyakazi wenzake wa Redio One na ITV, wakiwa Hospitalini hapo wakisubiri kumuona mgonjwa.
 Pia waandishi wa habari kutoka vyombo tofauti walikuwapo hospitalini hapo.
  Baadhi ya wafanyakazi wenzake wa Redio One na ITV, wakiwa Hospitalini hapo wakisubiri kumuona mgonjwa.
  Baadhi ya wafanyakazi wenzake wa Redio One na ITV, wakiwa Hospitalini hapo wakisubiri kumuona mgonjwa.
 Wengine walianza kukata tamaa wakianza kutawanyika angalau kutafuta chochote...
 Wapigapicha nao walipozi katika anlge ya peke yao wakivizia kunasa picha ya mgonjwa huyo wakati akitolewa katika chumba cha Dharula.
Kama Windo la Chui.........

*UFOO SARO WA ITV NA REDIO ONE, AJERUHIWA KWA RISASI, MAMA YAKE AFARIKI DUNIA, MUUAJI AJIUA



Habari zilizoufikia mtandao huu, zinasema kuwa, Mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha ITV na Redio One, Ufoo Saro pichani, amejeruhiwa kwa risasi na mtu anayedaiwa kuwa mchumba wake, ambaye hakuweza kufahamika jina lake mara moja, ambaye pia amejiua kwa kijipiga risasi baada ya kudhani kuwa tayari alikwisha muua mwandishi huyo.

Aidha habari zinasema kuwa katika tukio hilo, pia Mama yake mzazi na Ufoo Saro, amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na Jamaa huyo, katika tukio hilo lililotokea alfajiri ya leo nyumbani kwa mama mzazi wa Ufoo maeneo ya Kibamba.  Habari zinasema kuwa jamaa huyo aliwasili nchini jana na  kufikia nyumbani kwa Mchumba wake huyo, 'Ufoo' na alfajiri ya leo majira ya saa 11, waliondoka wawili hao na kwenda nyumbani kwa Mama mzazi wa Ufoo huko maeneo ya Kibamba, ambapo imeelezwa kuwa huenda wawili hao walifunga safari hiyo kwa kutafuta suluhisho la kutoelewana kwao.   Akizungumza na Radio one Kamanda wa Polisi wa mkoa wa kipolisi wa Kinondoni kamanda Wambura alithibitisha kutokea kwa tukio hilo alfajiri ya leo na kuongeza kuwa muuaji huyo amegundulika kuwa ni mfanyakazi katika Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) huko Sudani ila bado haijafahamika kwamba anafanyia kitengo gani.  
Imeelezwa kuwa hali ya mwandishi huyo inaendelea vizuri akiwa amelazwa ICU katika Hospitali ya Muhimbili, akiendelea kupatiwa matibabu.  Aidha imeelezwa kuwa Ufoo amejeruhiwa maeneo ya tumboni, ambapo inadaiwa ndipo alipopigwa risasi nyingi zaidi, begani na mguuni.

0 comments: