Rais
Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mkewe, Mama Salma, Mwenyekiti
wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) jana, wakati alipowasili
katika viwanja vya mahafali katika mahafali ya Kwanza ya Shule ya
Sekondari ya WAMA Nakayama, yaliyofanyika shuleni katika Kijiji cha
Nyamisati, Wilaya ya Rufiji, mkoani Pwani jana. Zaidi ya wanafunzi 60
walitunukiwa vyeti vya kumaliza kidato cha nne na zawadi mbalimbali
zilitolewa kwa wahitimu wakati wa mahafali hiyo, ambayo yalihudhuriwa
pia na viongozi na watu mashuhuri, akiwemo Balozi wa Japan na
wafanyabiashara, ambapo Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi aliahidi
kuisadia shule hiyo, shilingi milioni 200 kila mwaka kwa miaka mitano
mbazo ni kiasi cha shilingi bilioni moja kwa miaka hiyo mitano. (Picha
zote kwa hisani ya Fullshangwe)

Rais Jakaya Kikwete akizungumza na wageni waaikwa na wahitimu wakati wa mahafali hayo jana huko Nyamisati Rufiji.

Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkuu wa shule ya WAMA Nakayama Suma Mensa na viongozi mbalimbali wakati aliowasili shuleni hapo.

Watu mashuhuri na viongozi mbalimbali wakiwa katika mahafali hayo.

Mama Salma Kikwete akiwasili katika eneo la tukio. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Shule hiyo Dk. Ramadhan Dau.

Wahitimu wakiingia katika eneo la tukio.

Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akicheza na wanawake wenzake wake wa viongozi.

Rais
Jakaya Kikwete wa nne kutoka kulia akiwa na viongozi mbalimbali katika
meza kuu wakiimba wimbo wa taifa uliooongozwa na wanafunzi wa shule ya
WAMA Nakayama kutoka kulia ni Balozi anzania Mhe.Masaki
Okada Mkuu wa mkoa wa Pwani Ndugu Mwantumu Mahiza, Mama Salma Kikwetena
kutoka kushoto ni Dr. Ramadhan Dau Mwenyekiti wa bodi ya shule ya Wama
Nakayama na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dr. Shukuru Kawambwa.

Baadhi wa walimu wa shule hiyo.

Baadhi ya wanakamati kutoka kulia ni Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage, Daudi Nasibu Katibu Mkuu wa Taaisis ya WAMA na Dan Kiondo.

Baadhi ya wananfunzi wa shule ya WAMA Nakayama.

Mbunge Vick Kamata akiongoza wanafunzi wa Wama Nakayama kuimba wimbo maalum kwa wahitimu katika mahafali hayo.

Viongozi mbalimbali wakicheza muziki wakati wa mahafali hayo.

Dk. Ramadhan Dau, Mwenyekiti wa bodi ya shule ya Wama Nakayama akizungumza katika mahafali hayo

Mama Salma Kikwete akikaribisha wageni mbalimbali katika mahafali hayo.

Mkuu wa shule ya WAMA Nakayama Suma Mensa aakitoa historia ya shule hiyo

Mmoja
wa wasanii wa kundi la Mjomba Band linaloongozwa na msanii Mrisho Mpoto
akiigaiiza katika igizo maalum lililokuwa likitafsiri changamoto
zinazomkabili mtoto wa kike yatima na anayeishi kwenye mazingira magumu
katika suala zima la kupata elimu.

Mkuu wa Wilaya ya Kionondoni, Jordan Rugimbana pamoja na waalikwa wengine (katikati), akiwa katika hafla hiyo.

Wahitimu wakiimba wimbo maalum wa kumshukuru Mwenyekiti wa WAMA mama Salma Kikwete.

Nyoka alikuwa ni moja ya burudani katika mahafali hayo.

Mwenyekiti
wa Makampuni ya IPP Regnald Mengi akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Mwantumu Mahiza. Kulia ni mke wa Makamu wa Rais, Mama Aisha Bilal.

Baadhi ya majengo ya shule hiyo.
Mdau Seraphina kutoka Serena Hotel alihudhuria pia
Mama Salma Kikwete katikati akiimbiwa wimbo maalum na wahitimu

Rais Jakaya Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete akicheza wimbo maalum ulioimbwa na wanafuzni wahitimu katika mahafali hayo

Rais Jakaya Kikwete na Mkewe mama Salma Kikwete wakiongoza viongozi mbalimbali kucheza wimbo huo



0 comments: