![]() |
| Wadau wakiwa wa Mali Hai Arusha wakiwa katika picha ya pamoja |
MAANDAMANO MAKUBWA ARUSHA YA KUPINGA UJANGILI,BALOZI KAGASHEKI ASEMA MWISHO WA MAJANGILI UMEFIKA
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 2:31 AM
Mkurugenzi
mkuu wa Hifadhi za Taifa nchini(TANAPA)Bw.Allan Kijazi(T shirt
nyeupe)akisalimiana na maafisa wa Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa ya
Ngorongoro leo kwenye uwanja wa ndege wa Arusha wakati wakimsubiri
Waziri wa Maliasili na Utalii,Balozi Khamis Kagasheki kuongoza
maandamano ua kupiga vita ujangili wa Tembo nchini
Na Mwandishi Wetu,Arusha
Waziri wa
Maliasili na Utalii,Balozi Khamis Kagasheki amesema serikali ya Rais
Jakaya Kikwete haitakubali utalii ufie mikononi mwake kwa kuwaacha
majangili kutamba kwa kuwaua hovyo wanyama mbalimbali hasa Tembo kwenye
Hifadhi za taifa nchini.
Balozi
Kagasheki leo ameongoza maandamano makubwa ya wadau wanaopinga vitendo
nya ujangili vinavyohatarisha uwepo wa Tembo kwa mika 15 ijayo kama
hatua mahususi hazitachukuliawa.
"Sasa
hakutakuwa na suala la wanaharakati kutaka kesi ziharakishwe mahakamani
kwasababu maafisa wetu wakikutana na majangili huko porini mambo
yatakua yanaishia huko huko,"alisema Kagasheki
Akizungumza
katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye viwanja vya AICC Kijenge
,Mwenyekiti wa taasisi iliyoandaa maandamano hayo ya Tanzania
Association of Tour Operetors(TATO)Willy Chambuso alisema kuna kila
sababu ya serikali ya Tanzania kuzungumza na serikali ya China ambako
kumeonakana ni soko la pembe za Ndovu.Picha na Habari na
www.rweyemamuinfo.blogspot.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)












0 comments: