LUTENI MLIMA WA JWTZ ALIYEUAAWA DRC CONGO AZIKWA DAR

 Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), wakishusha kwenye gari jeneza lenye mwili wa  askari mwenzao, marehemu Luteni Rajab Mlima wakati wa maziko yaliyofanyika jana katika makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam jioni hii. Mlima ambaye alikuwa katika Jeshi la Umoja wa Mataifa la Kulinda Amani DRC Congo aliuawa akiwa kazini katika Mlima Gavana eneo la Goma. (PICHA NA KHAMISI MUSSA)Mmiliki wa www.ujijirahaa.blogspot.com.
 Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), wakiwa wameinamia kwa huzuni  jeneza lenye mwili wa  askari mwenzao, marehemu Luteni Rajabu Mlima wakati wa maziko yaliyofanyika leo katika makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam jioni hii. Mlima ambaye alikuwa katika Jeshi la Umoja wa Mataifa la Kulinda Amani DRC Congo aliuawa akiwa kazini katika Mlima Gavana eneo la Goma. (PICHA NA KHAMIS MUSSA)
 Waombolezaji wakijiandaa kufanya maziko
 Waombolezaji wakifanya maziko

 Askari wa JWTZ wakitoa heshima wakati wa maziko
 Meja Leonidas Luangisa akisoma wasifu wa marehemu Luteni Mlima.
Msemaji Mkuu wa Familia ya Mlima, Balozi Alhaji Saleh Tambwe akisoma salamu za familia na kuwashukuru watu wote walioshiriki kwenye mazishi hayo.

0 comments:

DIWANI MALEMBEKA AIPIGA TAFU TIMU YA SOKA YA UHURU FM

 Diwani wa Kata ya Msongola, Ukonga, Dar es Salaam, Angel Malembeka (kulia) ameipiga tafu timu ya soka ya Uhuru FM, kwa kuipatia jozi mbili za jezi na mipira miwili ikiwa ni sehemu ya kuimarisha ushirikiano baina ya timu hiyo na kata yake. Pichani, Diwani huyo akikabidhi vifaa kwa uongozi wa timu hiyo, Angel Alikimali na Furaha Luhende, katika hafla fupi iliyofanyika nje ya Jengo la CCM mkoa wa Dar es Salaam, leo. Wakati Luhende ni Mwenyekiti wa timu hiyo,  Akilimali ambaye ni Kaimu Mkurugebzi Mtendaji wa Uhuru FM ni mlezi wa timu hiyo.
 Akilimali akimshukuru Masala Mabula ambaye ni mchezaji aliyeibuliwa kipaji chake katika michuano ya Malembeka Cup iliyomalizika hivi karibuni ambaye sasa anajiandaa kwenda Msumbiji kucheza soka la kulipwa. Masala alifuatrana na Diwani huyo (kulia)
Luhende na Akilimali wakifurahia vifaa hivyo baada ya kukabidhiwa na diwani
 Diwani na Akilimali wakiwa na baadhi ya waandishi na watangazaji wa Uhuru baada ya makabidhiano hayo.
Mtangazaji wa Uhuru FM, Mhina Dungumalo akimhoji diwani huyo baada ya makabidhiano Imetayarishwa na theNkoromo Blog

0 comments:

Tamasha la Krismas kufanyika Uwanja wa Taifa desemba 25.


WAANDAAJI wa Tamasha la Krismas wametangaza kuwa tamasha hilo litafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Desemba 25 mwaka huu.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ilieleza kuwa awali mikoa sita iliomba kuwa mwenyeji wa tamasha hilo, lakini kamati yake imeteua Mkoa wa Dar es Salaam uwe wa kwanza. “Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Krismas imeamua lifanyike Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, halafu Desemba 26 tutatizama mkoa mwingine. Tunaomba mashabiki wetu waendelee kutuunga mkono,” alisema Msama.
Alisema awali walipokea maombi kutoka kwa wadau mbalimbali wa muziki wa Injili nchini wakiomba lifanyike katika mikoa yao, ambayo ilikuwa ni Mbeya, Mwanza, Arusha, Dodoma, Dar es Salaam na Shinyanga.
Tamasha la Krismas linaandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion ya jijini Dar es Salaam, ambayo pia huandaa Tamasha la Pasaka kila mwaka.  Kwa mujibu wa Msama wanataka Tamasha la Krismas liwe bora zaidi kuliko la Pasaka kwa kualika wasanii maarufu kutoka nje na ndani ya Tanzania.
Alisema hilo litakuwa tamasha kubwa la nyimbo za kumsifu Mungu na litakuwa na tofauti kubwa iilinganisha na matamasha mengine yaliyowahi kuandaliwa na kampuni yake.

0 comments:

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA SERIKALI ZA MITAA KUJADILI MABADILIKO YA TABIANCHI.

01Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua rasmi kongamano la Kimataifa la Serikali za Mitaa la kujadili Mabadiliko ya Tabianchi, lililoanza leo kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam. Picha na OMR 02Sehemu ya washiriki wa Kongamano hilo, wakimsikiliza Makamu wa Rais, wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi huo, kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam, leo. Picha na OMR 03.Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais, Richard Muyungi, akizungumza kutoa mada yake wakati wa kongamano la Kimataifa la Serikali za Mitaa la kujadili Mabadiliko ya Tabianchi, lililoanza leo kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam, lililofunguliwa na Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal. Picha na OMR
05Sehemu ya washiriki wa Kongamano hilo, wakimsikiliza Makamu wa Rais, wakati akisoma hotuba yake ya ufunguzi huo, kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam, leo. Picha na OMR 06Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano la Kimataifa la Serikali za Mitaa la kujadili Mabadiliko ya Tabianchi, lililoanza leo kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam, baada ya kufungua rasmi Kongamano hilo. Picha na OMR 07Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano la Kimataifa la Serikali za Mitaa la kujadili Mabadiliko ya Tabianchi, lililoanza leo kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam, baada ya kufungua rasmi Kongamano hilo. Picha na OMR 08Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea katika moja ya Banda la maonyesho baada ya kufungua rasmi kongamano la Kimataifa la Serikali za Mitaa la kujadili Mabadiliko ya Tabianchi, lililoanza leo kwenye Hoteli ya Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

0 comments:

Yanga yakung'uta Mgambo Shooting mabao 3-0


Mashabiki wa Yanga wakifuatilia mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom kati ya timu yao hiyo na Mgambo Shooting, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Peter Mwalanzi wa Mgambo Shooting, akimtoka Simon Msuva wa Yanga, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Peter Mwalanzi wa Mgambo Shooting, akimtoka Simon Msuva wa Yanga, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Peter Mwalanzi wa Mgambo Shooting, akimtoka Simon Msuva wa Yanga, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Mrisho Ngassa wa Yanga, akijaribu kumtoka Peter Mwalanzi wa Mgambo Shooting katika mchezo huo.
Mrisho Ngassa wa Yanga na Peter Mwalanzi wa Mgambo Shooting wakikimbilia mpira, wakati wa mchezo huo.
Mrisho Ngassa wa Yanga na Peter Mwalanzi wa Mgambo Shooting wakikimbilia mpira, wakati wa mchezo huo.
Simon Msuva wa Yanga na Peter Mwalanzi wa Mgambo Shooting wakiwania mpira, wakati wa mchezo huo.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao lao la kwanza lililofungwa na Mbuyu Twite, wakati ilipopambana na Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Wachezaji wa Yanga wakipongezana na kushangilia bao lao la kwanza lililofungwa na Mbuyu Twite.
Wachezaji wa Yanga wakipongezana na kushangilia bao lao la kwanza lililofungwa na Mbuyu Twite.
Wachezaji wa Yanga wakipongezana na kushangilia bao lao la kwanza lililofungwa na Mbuyu Twite.
Mrisho Ngassa wa Yanga, akijaribu kuwatoka Bashiru Chanache (katikati) na Daud Salum wa Mgambo Shooting wakati wa mchezo huo.
Rajab Zahir wa Yanga, akiudhibiti mpira huku akifuatwa na Bakari Mtama wa Ruvu Shooting.
Rajab Zahir wa Yanga na Bakari Mtama wa Ruvu Shooting, wakipambana kuuwania mpira.
Rajab Zahir wa Yanga akiudhibiti mpira huku akifuatwa na Bakari Mtama wa Ruvu Shooting.
Simon Msuva wa Yanga akifuatwa na Bakari Mtama na Bashiru Chanache wote wa Ruvu Shooting. Mpaka mwisho wa mchezo huo, Yanga ilishinda mabao 3-0

0 comments:

KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI, CHAFUNGULIWA JIJINI MBEYA LEO


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kushoto) akimpokea Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Mariam Ntunguja ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi cha siku tatu kinachofanyika katika Hoteli ya Paradise jijini Mbeya. Katika Hotuba yake ya ufunguzi, Ntunguja aliwaomba watendaji wakuu wa wizara hiyo washirikiane vizuri na watumishi wao ili kuleta mafanikio zaidi ndani ya wizara hiyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Mariam Ntunguja ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi akizungumza na wajumbe wa baraza hilo kabla ya kufungua kikao cha siku tatu kinaofanyika katika Hoteli ya Paradise jijini Mbeya. Wa pili kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mwamini Malemi. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Edson Nyinyimbe. Wa pili kushoto ni Venance Ntiyalundura, Katibu wa tawi hilo. Katika kikao hicho Ntunguja aliwaomba watendaji wakuu wa wizara hiyo washirikiane vizuri na watumishi wao ili kuleta mafanikio zaidi ndani ya wizara hiyo. 
Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Mariam Ntunguja (hayupo pichani) wakati alipokuwa anatoa hotuba ya kufungua mkutano wa wafanyakazi wa siku tatu unaofanyika katika Hoteli ya Paradise jijini Mbeya. 
Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakiimba nyimbo ya mshikamo daima kabla ya mgeni rasmi, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Mariam Ntunguja (hayupo pichani) kufungua kikao cha baraza hilo kinachofanyika katika Hoteli ya Paradise, jijini Mbeya. 
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Mariam Ntunguja (wa tano kutoka kushoto waliokaa), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (wa tano kulia waliokaa), Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mwamini Malemi (wanne kulia waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa idara wa wizara hiyo na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi baada ya Kikao cha siku tatu cha baraza hilo kufunguliwa katika Hoteli ya Paradise, jijini Mbeya leo.
 Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

0 comments:

WAFANYAKAZI WA KIWANDA CHA KONYAGI (TDL) WALIOKWENDA KUONA MECHI YA BARCELONA NA REAL MADRID,HISPANIA WAREJEA WAKIWA NA BASHASHA TELE

Mfanyakazi wa Kiwanda cha Konyagi cha Tanzania Distilleries Limited (TDL), Khadija Madawili ambaye alikuwa kiongozi wa msafara wa wafanyakazi wa TDL waliokwenda kushuhudia pambano la Ligi ya La Liga ya Hispania kati ya Barcelona na Rael Madrid, akirejea jana kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam. Wafanyakazi watano wa TDL, waliteuliwa baada ya kampuni hiyo kushinda  Tuzo ya SABMILLER AFRICA MB COMPLEMENTARY BEVERAGE CATEGORY AWARD FOR F 13)
 Joseph Chibehe (kushoto) akilakiwa na mkewe baada ya kuwasili
                                             Chibehe akiwa na furaha baada ya kulakiwa na mkewe
 Bavon Ndumbati (kushoto), akilakiwa na ndugu yake. Katikati ni Michael Mrema
                                                              Bavon akiwa na furaha
                                                                 Mwesiga Mchuruza.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Konyagi ya Tanzania Distilleries Limited (TDL), David Mgwassa (katikati), akiwa na mabosi wa kampuni mama ya SABMILLER AFRICA.wakiwa wameshikilia tuzo hiyo ya  MB COMPLEMENTARY BEVERAGE CATEGORY AWARD FOR (F 13).

KAMPUNI ya Tanzania Distilleries Ltd, (KONYAGI) ambayo ni miongoni mwa kampuni tanzu za Kampuni ya Sabmiller South Africa, imeshinda tuzo ya utendaji bora wa bidhaa (SABMILLER AFRICA MB COMPLEMENTARY BEVERAGE CATEGORY AWARD FOR F 13). Sabmiller inamiliki zaidi ya viwanda 60 vya bia na vinywaji vingine duniani.

Baada ya ushindi huo, Mkurugenzi Mkuu wa TDL, Mgwassa ambaye alipambana mpaka kupata ushindi huo, aliamua kuwazawadia baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo, kwenda Hispania kushuhudia pambano la timu kubwa za Barcelona na Real Madrid lililofanyika mwishoni mwa wiki.

Wafanyakazi waliokwenda Hispania  na kurejea jana usiku kwa ndege ya Afrika Kusini ni; Joseph Chibehe, Khadija Madawili, Bavon Ndumbati, Michael Mrema na Mwesiga Mchuruza.

Wafanyakazi hao, walipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, walionekana kuwa na bashaha na kupokelewa na ndugu zao pamoja na baadhi ya wafanyakazi wenzao.

Akizungumza kwa niaba ya wenzie,Michael Mrema wa Kanda ya Kaskazini, alisema kuwa wanashukuru uongozi kuwapa zawadi hiyo, ambayo imewafanya kuwa na morari mpya wa kazi.

Pia anaseama walifurahi sana kushuhudia mechi hiyo kubwa ya timu za Barcelona na Real Madrid ambapo timu ya Barcelona waliyokuwa wanaishabikia kushinda mabao 2-1.

0 comments: