POLISI NA WANANCHI WAUA WATU WANAODAIWA KUWA MAJANGILI MKOANI DODOMA .

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna
Msaidizi (ACP), David Misiime (kushoto), akitoa
taarifa ya tukio la kuuawa kwa watu wanaodaiwa
kuwa ni majangili. Mbele ni pembe zilizokamatwa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna
Msaidizi (ACP), David Misiime, akionesha
pembe za ndovu zilizopatikana katika tukio hilo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna
Msaidizi (ACP), David Misiime (kushoto), akitoa
taarifa kwa waandishi wa habri kuhusu tukio la
vifo vya watu watatu wanaodhaniwa kuwa ni majangili
waliouawa na wananchi katika Kijiji cha Miganga
Mvumi Dodoma. Pembeni ni Gari aina ya Noah no
T 983 BZJ walilokuwa wakilitumia na meno
73 ya Tembo.
Miili ya majangili hao baada ya kuawa kwa kupigwa
na vitu vyenye ncha kali na kuchomwa moto ikiwa
Hospitali ya Misheni ya Mvumi mjini Dodoma.

Miili ya majangili hao baada ya kuawa.
Na John Banda, Dodoma

MAJANGILI watatu wa nyara za serekali wameuawa

kwa mishale yenye sumu na kisha miili yao kuchomwa
moto na wananchi katika purukushani na polisi walipokuwa wakijaribu kukimbia ili kutorosha meno ya tembo.

Tukio hilo lilitokea jioni ya alhamis wiki hii katika kijiji cha Miganga kata ya mvumi wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma ambapo miili yao ilikutwa ikiwa imehalibika kutokana na kuchomwa moto.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa polisi mkoa wa

Dodoma David Misime alisema majangili hayo yaliuawa na wanachi wenye hasira kali kwa zana mbalimbali
za kijadi walipokuwa wanakimbilia polini ili kujiokoa
na mkono wa polisi.

Misime alisema jeshi hilo lipokea taarifa kutoka kwa

wananchi wema kuwa kulikuwa na Gali likitokea Manda likiwa na Meno ya Tembo na kisha kuweka mtego katika kijiji cha mwitikila ambapo waliona gali aina ya NOAH T 983 BZJ na kulisimamisha na Dereva wa Gali hilo alifanya kama anapunguza mwendo na kisha kuondoka kwa mwendo wa kasi.

‘’Polisi wakishirikiana na wananchi walianza kulifukuza walipofika kijiji cha Miganga Mvumi polisi walifanikiwa kupiga Risasi tairi moja ya kushoto na hivyo watu watatu waliokuwemo ndani gari hilo waliruka na kutawanyika, wananchi waliojichukulia sheria mkononi waliwashambulia kuasi cha kupoteza maisha yao’’, alisema

Aidha kamanda Misime alisema baada ya kulipekua

Gari hilo walikutaMeno 73 ya Tembo yenye uzito wa
kilo 255.9 yakiwa na thamani ya zaidi ya sh. 225 milion
pamoja na hati ya mashitaka (CHARGE SHEET)
ambayo ni kesi ya kuhujumu uchumi namba 4/2012
iliyokuwa imefunguliwa katika mahama ya Mpanda Mkoa wa Katavi na Leseni ya Udereva na 4000692535
Aboubakar Peter huku wakihisi ni mmoja ya
waliouawa.

Alisema walikuwa wameshitakiwa kwa kosa la

kupatikana
na Meno 3 ya Tembo Tarehe 17.06.2012 na maafisa
wanyama pori katika eneo la Msaginya Wilaya ya
Mlele mkoa wa katavi majina ya walikuwa
wameshatakiwa ni Joseph Marius (Ngondo) 59
mkazi wa maili mbili Dodoma, Aboubakar Mhina 25,
mkazi wa Mkuhungu Dodoma, Msafiri Milawa 36,
mkazi wa Nkuhungu Dodoma na Petro Mtipula 55,
mkazi wa mpanda.

Kamanda alitoa wito kwa wananchi wasijichukulie

Sheria mikononi kwani kwa kufanya hivyo ni kupoteza
ushahidi na inawawia vigumu polisi kupata mtandao
inayohusika na matukio kama hayo.


0 comments: