VIONGOZI WA DINI WASISITIZA UMUHIMU WA KULINDA AMANI YA TAIFA
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 6:57 AM
BENY Israel Mwaisaka, mchungaji wa kanisa la FPCT Komwale lililopo nje kidogo ya mji wa Handeni mkoani Tanga
Na Mwandishi wetu
BENY
Israel Mwaisaka, mchungaji wa kanisa la FPCT Komwale lililopo nje
kidogo ya mji wa Handeni, wilaya ya Handeni mkoani Tanga anasema kuwa
ninatambua na kuthamini Amani ambayo imekwepo tangu nchi ipate uhuru
imekuwa msingi mkubwa wa maendeleo limewezesha wananchi kuishi kwa
utulivu na kufanya shughuli zao bila hofu.
Kupitia
amani hii,
Watanzania wameweza kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii
na kiuchumi kwa uhuru mkubwa. Michezo, biashara, elimu na ibada
vimekuwa vikifanyika kwa utulivu mkubwa,vilevile Vijana wamepata nafasi
ya kusoma na kujiendeleza, huku watu wa dini mbalimbali wakifanya ibada
zao kwa uhuru.
Haya
yote ni matokeo ya juhudi za waasisi wa taifa letu ambao waliweka msingi
wa umoja, mshikamano na upendo miongoni mwa Watanzania.
Mch.Mwaisaka
anasema Amani ikikosekana hali hiyo huleta hofu kwa wananchi na
kuhatarisha maendeleo katika sekta mbalimbali kama vile elimu, uchumi na
hata uhuru wa kuabudu hivyo Ni muhimu kutambua kuwa amani si jambo la
kudumu bila jitihada, bali inahitaji kulindwa na kila mmoja wetu kwa
nguvu zote.
Katika
mazungumzo mbalimbali ya kijamii, ndugu Hendry Lema, ambaye ni mzee
mstaafu wa kanisa la KKKT Usharika wa Engarenaro Arusha, amekuwa
akisisitiza umuhimu wa amani kwa maendeleo ya taifa. Anasema kuwa amani
ndiyo nguzo kuu inayowezesha jamii kustawi, na bila amani hakuna
maendeleo ya kweli yanayoweza kupatikana.
"Mimi
ni baba na Kichwa cha familia pia ni mlezi wa kiroho na mshauri wa
jamii, nahimiza watu kurejea katika misingi ya upendo, heshima na
kuvumiliana,
Ni wajibu
wa kila Mtanzania kuhakikisha kuwa tunadumisha misingi hii ya upendo na
mshikamano. Kama alivyotuasa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,
upendo ni silaha kubwa inayoweza kuondoa chuki, ubaguzi na migogoro.
Tukizingatia
hilo, tutaweza kujenga taifa lenye umoja na lenye kuheshimiana kati ya
wananchi na viongozi wao, tutangulize utu ili kuepusha migongano isiyo
ya lazima.
Mwisho,
nitoe wito kwa Watanzania wote bila kujali dini au imani zao, kuendelea
kuliombea taifa letu na kumtanguliza Mungu katika kila jambo. Tukiwa na
moyo wa toba na unyenyekevu,
Mungu
atatusaidia kulinda amani yetu na kutujalia haki ya kweli. Kama
ilivyoandikwa katika Mithali 14:34, “Haki huinua taifa; bali dhambi ni
aibu ya watu wote.” Mungu ibariki Tanzania, Mungu tubariki Watanzania.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

0 comments: