DAWA YA JINO SI KUNG'OA , ONANA NA MTAALAMU WA AFYA YA KINYWA NA MENO

Na Khamisi Mussa – Dar es Salaam

Imebainishwa kuwa dawa ya jino bovu si kuling’oa bali ni kufika hospitalini kuonana na wataalamu wa afya ya Kinywa Na meno, Kwa uchunguzi zaidi, ambao watasaidia kutibu na kuwaepusha na Madhara yakudumu ( Mapengo)

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Msaidizi wa huduma za afya, kinywa na meno kutoka Wizara ya Afya Dkt. Baraka Nzobo wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa watu wengi wamekuwa wakichukua hatua za kung'oa meno yao bila kufuata utaratibu wa matibabu jambo ambalo ni hatari kwa afya ya kiywa na meno na Mstakabali mzima wa afya zao.

Dkt. Nzobo alisema asilimia kubwa ya watanzania wanasumbuliwa na changamoto za meno, hasa meno kuoza kwa muda mrefu lakini hawafiki hospitali ili kupata matibabu, inapofikia wanapata maumivu makali ndio wanaenda hospitali hivyo kuishia kwenye kung’olewa jino/ meno.

“Dawa ya jino lenye hitilafu sio kulin’goa ni kulitibia, Pia dhana ya kutokufika hospitali kufanya uchunguzi, hupelekea jamii kuchukua maamuzi ya kung’oa meno pale yanapouma”, kwa sababu ya uchelewaji.

Dkt. Nzobo alibainisha kuwa zipo taratibu za kiafya ambazo zikichukuliwa zinaweza kusaidia kuimarisha afya ya meno badala ya kung’oa.

“Unatakiwa kufika hospitali na kufanyiwa vipimo kama x-ray ya jino ili kubaini uharibifu umefikia hatua gani, ambapo wataalamu wa afya watakupa ushauri wa nini kifanyike kama ni kuliziba au kutumia dawa ili uweze kukaa sawa”, alisema Dkt. Nzoba.  

Zaidi ya asilimia 80% ya watanzania ambao wanachangamoto ya meno kuoza yanaweza yakazibwa vizuri na kupona kabisa na tukabaki na asilimia 10 hadi 20 wale ambao wamechelewa kufika hospitali ndio wanaweza kuishia kwenye kung’olewa meno.

0 comments: