RC MTAKA AWATAKA WANANCHI, VIONGOZI SIMIYU KUTOA USHIRIKIANO UTAFITI WA MAPATO NA MATUMIZI YA KAYA
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 7:58 AM
Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka ametoa wito kwa wananchi na
Viongozi Mkoani humo kutoa ushirikiano kwa wadadisi na wataalam wa
Takwimu katika utafiti wa mapato na matumizi ya kaya binafsi unaoendelea
hapa nchini ili kuwezesha upatikanaji wa takwimu halisi na sahihi
Mkoani humo.
Mtaka
ameyasema hayo katika Mkutano wake na waandishi wa habari, wataalam
wa Takwimu na Viongozi wa madhehebu ya dini uliofanyika Februari 28
Mjini Bariadi.
Amesema
Utafiti huo utatoa makadirio ya uchumi jumla(macroeconomic), hususani
matumizi ya kaya kwa ajili ya Pato la Taifa (Gross Domestic
Product-GDP), kupata mwenendo wa matumizi ya moja kwa moja ya kaya ili
kuwezesha uchambuzi wa hali ya soko na kupata taarifa za umilikaji wa
vifaa vya kudumu pamoja na nyenzo za uzalishaji wa kipato.
Amesema
kwa mujibu wa sheria namba 9 ya mwaka 2015 kila mwananchi anawajibika
kushiriki katika utafiti kwa kutoa taarifa sahihi na kwa wakati ili
kuiwezesha Serikali kupata takwimu rasmi ambazo zitatumika kupanga na
kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo.
“
Lengo mama la utafiti huu ni kujua hali ya kipato kwa kaya zetu asije
mtu akapotosha kuwa watafiti wana agenda nyingine, ndiyo maana nimeona
viongozi wa Dini nao walifahamu hili ili wasaidie kuwaeleza kwa ufasaha
waumini wao; Serikali inahitaji takwimu sahihi ili ipange bajeti na
kuweka mipango ya maendeleo, niwaombe wananchi na viongozi tutoe
ushirikiano” alisema Mtaka.
Aidha,
amemuagiza Meneja wa Takwimu mkoani humo kuendelea kutoa elimu kwa
wananchi juu ushiriki wao katika utafiti huu hususani kaya
zilizochaguliwa na akamtaka yeye na wataalam wa Takwimu wa Mkoa huo
kufanya mikutano katika minada na magulio pamoja na maeneo ya yenye
idadi kubwa ya watu yakiwemo ya Makao Makuu ya Wilaya na miji
midogo(centers) ili kujenga uelewa kwa wananchi.
Meneja
wa Takwimu Mkoa wa Simiyu, Nestory Mazinza amesema tangu utafiti huu
uanzae Desemba Mosi 2017 jumla ya kaya 102 zimeshafanyiwa utafiti kati
ya 408 zinazotarajiwa kufikiwa mpaka kumalizika kwa zoezi hilo mwezi
Novemba 2018.
Naye
Bi.Joyce Luhende Mdadisi kutoka Wilaya ya Meatu amesema wanapofanya
utafiti huu wanakutana na changamoto mbalimbali na kubwa ikiwa ni baadhi
ya wanakaya kuogopa kutoa taarifa zinazohitajika wakati wakihojiwa hali
inayopelekea kukosekana kwa taarifa sahihi.
Akizungumza
kwa niaba ya viongozi wa Dini, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikiristo
Tanzania(CCT) Mkoa wa Simiyu, Mchungaji Martine Samson Nketo amesema
kupitia ibada watasaidia kuwahamasisha wananchi kushiriki katika
utafiti huu na kuwaeleza umuhimu wake katika mipango ya maendeleo
inayopangwa na Serikali.
Kaya zilizochaguliwa k kufanyiwa utafiti huu zinatoka katika maeneo 34
(Vijiji/Mitaa) kwenye Wilaya zote tano za Mkoa wa Simiyu yaliyopo katika
kata za Nkindwabiye, Nyangokolwa, Sakwe, Nyakabindi, Dutwa,
Matongo,Gilya, Sima,Mwamtani, Mwaswale, Mwamapalala, Nhobora, Zagayu,
Kinang’eli, Mwanhuzi, Mwandoya, Sakasaka, Mwabuma, Lubiga, Ng’oboko,
Busilili, Seng’wa, Masela, Mwamashimba, Buchambi, Badi, Nyalikungu,
Kiloleli,Kalemela, Mkula na Ngasamo.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na waandishi wa
Habari, Viongozi wa Madhebu ya Dini na Wataalam wa Takwimu (hawapo
pichani) katika kikao kilichofanyika Ofisini kwake Mjini Bariadi.
Kaimu
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Donatus Weginah akifafanua jambo
katika kikao cha Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka na waandishi wa
Habari, Viongozi wa Madhebu ya Dini na Wataalam wa Takwimu
kilichofanyika Mjini Bariadi.
Meneja
wa Takwimu, Mkoa wa Simiyu, Ndg.Nestory Mazinza akifanyiwa mahojiano na
waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Mkuu wa Mkoa
huo, Mhe.Anthony Mtaka na waandishi wa Habari, Viongozi wa Madhebu ya
Dini na Wataalam wa Takwimu kilichofanyika Mjini Bariadi.
Baadhi
ya Viongozi wa Madhehebu ya Dini wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) katika kikao kati yake na waandishi
wa Habari, Viongozi wa Madhebu ya Dini na Wataalam wa Takwimu katika
kikao kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mmoja
wa Wadadisi akifanyiwa mahojiano na waandishi wa habari mara baada ya
kumalizika kwa kikao cha Mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka na
waandishi wa Habari, Viongozi wa Madhebu ya Dini na Wataalam wa Takwimu
kilichofanyika Mjini Bariadi.
Baadhi
ya Wadadisi na Waandishi wa habari wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka (hayupo pichani) katika kikao kati yake na
waandishi wa Habari, Viongozi wa Madhebu ya Dini na Wataalam wa Takwimu
katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (wa tatu kulia) akiwa katika picha
ya pamoja na Meneja wa Takwimu, Mkoa wa Simiyu, Ndg.Nestory Mazinza(wa
pili kulia) na baadhi ya Viongozi wa Madhehebu ya Dini mara baada ya
kumalizika kwa kikao kati yake na waandishi wa Habari, Viongozi wa
Madhebu ya Dini na Wataalam wa Takwimu kilichofanyika Mjini Bariadi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: