Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Mhe. Glorious Luoga (wa tatu kushoto) akiongoza matembezi ya uhamasishaji wa Afya ya Kinywa na Meno kuelekea kilele cha maadhimisho hayo duniani yatakayofanyika Machi 20, 2018, kwenye viwanja vya Chuo cha Ualimu Tarime ambapo mgeni rasmi ni Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.
Suleimani Jaffo yatakayo fanyika katika viwanja hivyo yaliyotanguliwa na upimaji wa Afya
ya Kinywa na Meno na matibabu bure. kuanzia kushoto ni Afisa Afya wa Mkoa Mara
akimuwakilisha Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara, Rais wa Chama cha Madaktari
wa Kinywa na Meno Tanzania (TDA), Dokt. Ambege Mwakatobe, Rais
Mwandamizi wa Chama hicho, Dr. Deogratias Kilasara na Kaimu Ras Mkoa wa Mara Ndg, Emmanuel Kisongo . (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA) TARIME. Mmiliki wa ujijirahaa blog
Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Mhe. Glorious Luoga (wa pili kulia) akipokea matembezi hayo kwenye viwanja vya Chuo cha Ualimu Tarime
Matembezi ya uhamasishaji yakipita katika baadhi ya Barabara za wilaya ya Tarime .
Wananchi wajitokeza kwa wingi kujiandisha katika kiwanja cha Serengeti, wilayani Tarime, kushiriki matembezi ya uhamasishaji kuelekea kilele cha maadhimisho ya afya ya kinywa na meno Machi 20, 2018.
Profesa, Febronia Kahabuka (kushoto) akipokea karatasi zenye namba mara baada ya wananchi kujiandikisha kushiriki matembezi ya uhamasishaji ya maaaaadhimisho ya Afya ya Kinywa na Meno Duniani ambayo yanafanyika Kitaifa Tarime, Mkoani Mara Machi 20, 2018
Wanafunzi wa House of Hope wakitoa burudani katika kiwnja cha Serengeti kabla ya kuanza matembezi hayo
Madaktari wakiwapungia mikono wananchi waliojitokeza kushuhudia matembezi hayo, wa kwanza kulia katika msitari huo ni Daktari Bingwa wa kinywa na meno Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dakt, Gloria Leo na wapili ni Dr, Lorna Carneiro ambye ni Rais mstaafu wa chama cha madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania (TDA)
|
Meneja wa Hope Dental Mwanza Rock City Mall akishiriki matembezi hayo na akifatiwa na mfanyakazi mwenzake ambaye ni Muuguzi, Happy Barnabas |
Daktari wa Afya ya Kinywa na Meno Ofisi ya Rais TAMISEMI mbele akiwa katika matembezi hayo
Rais mstaafu wa Chama cha Madaktari
wa Kinywa na Meno Tanzania (TDA) Dokta, Lorna Carneiro akiwa katika matembezi hayo
wanafunzi wa Shule ya House of Hope iliyopo kijiji cha Ntagacha Wilaya ya Tarime wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kuhutubia mgeni rasmi katika viwanja vya Ualimu, Tarime
Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Mhe. Glorious Luoga (wa nne kushoto) akiimba wimbo wa Taifa pamoja na viongozi wengine katika viwanja vya Chuo cha Walimu kilichopo Tarime Mkoani Mara
Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Mhe. Glorious Luoga (wa pili kulia) akisalimia wananchi waliojitokeza viwanja vya Chuo cha Walimu wakati wa matembezi ya
uhamasishaji wa afya ya kinywa na meno kuelekea kilele cha maadhimisho
ya afya ya kinywa na meno duniani yatakayofanyika machi 20, 2018, ambapo
mgeni rasmi ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.
Suleimani Jaffo.kuanzia kushoto ni Daktari wa Afya ya Kinywa na Meno Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dr, James Kengia, Afisa Afya wa Mkoa Mara, Bumija Mhando akimuwakilisha Mganga Mkuu wa Mkoa huo, Rais wa Chama cha Madaktari
wa Kinywa na Meno Tanzania (TDA), Dokt. Ambege Mwakatobe na kushoto ni Kaimu Ras wa Mkoa huo, Emmanuel Kisongo
Profesa, Febronia Kahabuka akielekeza namna nzuri ya upigaji mswaki
Rais wa Chama cha Madaktari
wa Kinywa na Meno Tanzania (TDA), Dokt. Ambege Mwakatobe akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya matembezi hayo
Profesa, Febronia Kahabuka (wa pili kulia) katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya House of Hope iliyopo kijiji cha Ntagacha Wilaya ya Tarime
Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Mhe. Glorious Luoga (wa tano kushoto) katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi mbalimbali
Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Mhe. Glorious Luoga (katikati) akisalimiana na Daktari wa Meno Wilaya ya Ngara Mkoa wa Kagera, David Mapunda na kulia ni Rais wa Chama cha Madaktari
wa Kinywa na Meno Tanzania (TDA), Dokt. Ambege Mwakatobe
0 comments: