BALOZI WA KUWAIT AZINDU KISIMA CHA MAJI CHA 61WILAYNI KIMBONI

Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Al-Najem azindua kisima cha maji cha 61 Wilayani Kigamboni, Dar es salaam kwa ajili ya Shule ya Msingi ya GEZAULOLE yenye wanafunzi 868 na Shule ya Sekondari ya Ibnu Rushdy yenye wanafunzi 250 ikiwa ni mwendelezo wa utekelezezaji wa mradi wa '' KISIMA CHA MAJI KATIKA KILA SHULE'' ulioanzishwa na Ubalozi wa Kuwait mwanzoni mwa mwaka 2017. Hafla ya uzinduzi wa kisima hicho ilihudhuriwa pia na Diwani wa Sumangila Francis M. Chichi, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Maziku Luhemega, Mwenyekiti wa CCM Gezaulole Masiku Lupa, Mwalimu Mkuu Maryam Shaaban pamoja na wakaazi, walimu na wanafunzi wa Shule hiyo.

0 comments: