| |
WAAJIRI WATAKIWA KUWAPA WAFANYAKAZI WAO FURSA YA KUJIFUNZA ILI KUWAJENGA KIUWEZO
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 8:18 PM
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili
kwenye Ukumbi wakati wa utoaji wa tuzo ya mwajiri bora wa mwaka 2016 hafla iliyofanyika jana usiku Jijini Dar es salaam, Kushoto ni Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na kazi, Ajira, Vijana na
Wenye Uleamavu, Jenista Mhagama na Naibu wake waziri, Abdallah Possi.
Tuzo mbalimbali zikiwa zimeandaliwa kwa ajili ya kupatiw amakampuni yaliyoshiriki mwaka 2016.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewataka
waajiri kuendelea kuwapa fursa wafanyakazi wao kwa kwenda kupata ujuzi
wa aina mbalimbali kwani serikali imeadhimia kutoa mafunzo mahsusi kwa
lengo la kuwajenga uwezo waajiriwa.
Majaliwa
amesema hayo wakati wa utoaji wa tuzo za mwajiri bora wa mwaka
iliyoandaliwa na Association of Tanzania Employer (ATE) zilizofanyika
jana usiku na kuhudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,
Bunge na kazi, Ajira, Vijana na Wenye Uleamavu Jenista Mhagama na Naibu
wake waziri Abdallah Possi.,
Katika
utoaji wa tuzo hizo, Majaliwa amesema kuwa waajiri wanakabiliwa na
changamoto mbalimbali ikiwemo ugumu wa upatikanaji wamitaji, tozo ya
kuendeleza ujuzi na utiriri wa tozo mbalimbali ambapo huwa inawapa ugumu
kuweza kuwapa stahiki waajiriwa na kwa wakati.
Naye
Mwenyekiti wa ATE, Almas Maige amesema kuwa bado wanakabiliwa na
changamoto nyingi ila wanaimani kuwa kutokana na ushirikiano wanaoupata
sasa hivi kutoka kwa serikali ya awamu ya tano wana uhakika wa kuweza
kutimiza malengo ya waajiriwa ili kupata haki zao.
Maige
amesema kuwa bado wataendelea kuandaa tuzo hizi na zaidi Ubalozi wa
Norway umeonesha nia nzuri ya kushirikiana nasi kuweza kuona tunafikia
makengo mazuri.
Mkampuni
na mashirika mbalimbali waliweza kushiriki na kufanikisha hafla hiyo
ikiwemo, NSSF, PPF, NHC, SSRA, Geita Gold Mine, Coca Cola, MeTL, ACACIA
na mengine pia.
Mshindi
wa kwanza wa tuzo ya mwajiri bora ni Kampuni ya Bia ya Tanzania
Breweries Limited (TBL) wakifuatiwa na Coca Cola Kwanza na mshindi wa
tatu ni Geita Gold Mine.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo
ya mwajiri bora mwaka 2016 iliyoandaliwa na Association of Tanzania
Employer (ATE).
Mwenyekiti
wa Association of Tanzania Employer (ATE), Almas Maige akizungumza
wakati wa hafla ua utoaji wa tuzo ya mwajiri bora mwaka 2016
iliyofanyika jana usiku Jijini Dar es salaam.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akimpatia tuzo ya mshindi wa kwanza ya tuo ya
mwajiri bora mwaka 2016 Afisa Mwajiri Mkuu wa Tanzania Breweries Limited
(LTD) David Magese jana Jijini Dar es salaam.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akimpatia tuzo ya mshindi wa pili ya Tuzo ya
mwajiri bora wa mwaka 2016 Meneja Mwajiri Coca Cola Kwanza Sigifrid
Faustine jana Jijini Dar es salaam.
Waziri
Mkuu Kassim M. Majaliwa akitoa tuzo kwa washindi mbalimbali wa shindano
la mwajiri bora lililoandaliwa na Association of Tanzania Employers
(ATE) lililofanyika jana Jijini Dar es salaam
Waziri
Mkuu Kassim M. Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi
kutoka makampuni mbalimbali na washindi wa tuzo ya mwajiri bora kwa
mwaka 2016 katika vuipengele tofauti.
Wageni mbalimbali wakiwa katika hafla hiyo.
Picha zote na Zainab Nyamka
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: