NA MAGRETH MAGOSSO,KIGOMA
SERIKALI imeshauriwa iangalie
upya viwango vya utozaji wa ushuru katika rasilimali za umma,ili kuondoa
urasimu unaofanywa na baadhi ya
watumishi wa umma kwa nia ya kuidhofisha
serikali ya awamu ya Tano yenye dhati ya kupunguza umaskini wa kipato
kwa walalahoi.
Ushauri huo umetolewa na Mwenyekiti
wa Chama Cha Wauza mkaa mkoani kigoma Fadhili Hamisi wakati akizungumza na Gazeti
hili juzi katika kijiji cha Mazungwe kilichopo Halmashauri ya wilaya ya Uvinza
Mkoa wa Kigoma.
Alisema changamoto iliyopo katika
rasilimali za umma hasa zao la misitu katika uvunaji wa bidhaa ya mkaa imekuwa
ya utata kwa walio na kibali cha uvunaji wa zao hilo,ambapo idara ya misitu ina
hulka ya kutoa kibali kwa wadau lakini haielekezi eneo la uvunaji.
Alifafanua kuwa,kitendo cha kutoa
kibali bila eneo elekezi inachangia wenye vibali kuvamia kila pori analodhani
ni fursa kwake kwa lengo la kufanya biashara kwa mujibu wa kibali chake,hali
inayotishia janga la njaa siku zijazo
kwa kuwa,miti inakatwa holela kitendo kinachochangia mabadiliko ya tabia Nchi.
Hamisi alishauri serikali ipunguze
ushuru usio na tija ya kuokoa rasilimali
misitu,akitolea mfano wa gunia moja la mkaa lenye ujazo wa kilo 100 linalipiwa
kwa kiasi cha fedha sh.27,500 ambapo serikali kuu inachukua sh.240 kwa kila
kilo ya mkaa na sh.1,000 kwa ajili ya upandaji miti .
Alisema kitendo hicho kinachangia
rushwa na urasimu baina ya watumishi wa
idara husika na wavunaji ambao wanafanya
biashara kwa mujibu wa mazingira wanayowekewa na kwa ushuru wa sh.27,500 wanapaswa wauze gunia moja la mkaa kwa sh.60,000
hali ambayo ingeathiri uchumi wa wajasiliamali wengi hasa wapika vitafuno na
walalahoikushindwa kumudu bidhaa.
Hamisi alitolea mfano wilaya ya
uvinza ambayo inakabiliwa na urasimu wa ulipaji wa gharama za mkaa hata ukiwa
na gunia moja ukalipie katika benki husika ambayo ipo wilaya ya kigoma mjini
kisha urudishe stakabadhi katika halmashauri ya uvinza bila kujali athari ya gharama
za uvunaji wa zao hilo ni uwepo wa rushwa.
Ameiomba serikali kupitia idara
hiyo iondoe ushuru wa sh.240 kwa kilo moja ya mkaa hadi sh.150 kwa kila kilo moja ya mkaa ili wavunaji wenye
kibali wavune zao hilo kwa sheria,taratibu zenye mashiko kwa wafanyabiashara wa
mkaa ambao unatumika kwa wakubwa na wasio na kipato kikubwa.
Alipohojiwa Mkuu wa Wilaya ya
Uvinza Mwanamvua Hoza juu ya kero hiyo
alisema ili kuondoa urasimu huo,walengwa wafikishe malalamiko kwa mandishi
ofisnini kwake ili wayafanyie kazi kwa pamoja kwa lengo la kuondoa makandokando
yasiyo na tija, ili kuimarisha uwajibikaji wa serikali ya awamu ya tano.
Mwisho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: