RAIS ASSAD: SINA IMANI NA TRUMP LAKINI AKIWA NA NIA YA KWELI YA KUPAMBANA NA UGAIDI, SYRIA ITASHIRIKIANA NAYE
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 10:15 PM
Rais Bashar al-Assad wa Syria amesema kuwa,
ikiwa Donald Trump, rais mteule wa Marekani atapambana kwa dhati na
magaidi, basi serikali yake itashirikiana naye.
Rais Assad amefafanua zaidi kuwa, ikiwa rais huyo mteule wa
Marekani atapambana na magaidi, basi atapata uungaji mkono wa nchi
kadhaa kama vile Russia na Iran na nchi nyingine ambazo zinataka
kuhitimisha wimbi la magaidi.
Akijibu swali kuhusu matumaini aliyonayo kutoka kwa Donald Trump,
Rais Assad amesema kuwa, hana imani na rais huyo mteule wa Marekani
lakini angependelea rais huyo asiegemee upande wowote, aheshimu sheria
za kimataifa, aache kuingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine na
akomeshe uungaji mkono wa nchi yake kwa makundi ya kigaidi unaofanywa na
serikali inayomaliza muda wake ya Rais Barack Obama.
Hayo yanajiri katika hali ambayo Trump ametangaza kuwa, amefikia
natija kwamba Rais Assad ni chaguo bora na njia nzuri kwa ajili ya
kupambana na ugaidi ambao umekita mizizi nchini Syria. Ni vyema
kuashiria kuwa, magenge mengi ya kigaidi na ukufurishaji yanayotekeleza
jinai za kutisha nchini Iraq na Syria yanapata himaya ya moja kwa moja
kutoka serikali ya Marekani, utawala haramu wa Kizayuni wa Israel na
baadhi ya nchi za eneo, hususan Saudia, Qatar na Uturuki.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: