Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Methew Mtigumwe akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wa hadhara Kijijini Doroto
Baadhi
ya wananchi wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi
Methew Mtigumwe katika ziara yake katika Halmashauri ya Itigi
Mkuu
wa Wilaya ya Manyoni Mhe Godfrey Mwambe akiongea na wananchi katika
ziara ya mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Methew J. Mtigumwe
Na Mathias Canal
Mkuu wa mkoa wa Singida Mhe Mhandisi Mathew John Mtigumwe hii leo
ameanza ziara ya kikazi kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero za
wananchi katika Mkoa wa Singida.
Rc Mtigumwe ameanza ziara yake hiyo katika Halmashauri ya Itigi, iliyopo
katika Wilaya ya Manyoni ambapo atatembelea kata zote za halmashauri
hiyo.
Pamoja na kutambua kero za wananchi na mambo mengine pia
Mkuu huyo wa Mkoa wa Singida anatumia mikutano hiyo maalumu kwa ajili ya
kufahamiana na wanachi ikiwa ni pamoja kusikiliza kero zao ambazo
zimewasua kwa miaka mingi bila kupatiwa ufumbuzi.
Mtigumwe akiwa
katika Kijiji cha Doroto amehimiza zaidi wananchi kuandaa vyema mashaba
yao na kuzingatia kilimo chenye kustahimili ukame kwani kuna mabadiliko
makubwa ya tabia nchi jambo ambalo limepelekea kuchelewa kuanza kwa
mvua.
Mhe Mtigumwe amewaagiza maafisa kilimo wa Kata na Wilaya
zote za Mkoa wa Singida kutokaa ofisini kipindi hiki cha msimu wa kilimo
badala yake kwenda mashambani kuwasaidia wananchi mbinu bora za kilimo
sambamba na kuwasaidia namna bora ua kuandaa mashamba.
Sambamba
na hayo pia amewasisitiza wananchi kuzingatia maelekezo watakayopatiwa
na Maafisa kilimo ili kuwa na uhakika wa kuvuna mazao mengi zaidi kwa
kilimo chenye tija.
Katika ziara yake Mkuu wa Mkoa wa Singida
Mhandisi Mathew Mtigumwe ameambatana na Kamati ya ulinzi na usalama ya
Mkoa wa Singida.
KAWAIDA...!
RC SINGIDA AANZA ZIARA KUTEMBELEA KATA 136 ZA MKOANI SINGIDA
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Methew Mtigumwe akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wa hadhara Kijijini Doroto
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Methew Mtigumwe katika ziara yake katika Halmashauri ya Itigi
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe Godfrey Mwambe akiongea na wananchi katika ziara ya mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Methew J. Mtigumwe
Na Mathias Canal
Mkuu wa mkoa wa Singida Mhe Mhandisi Mathew John Mtigumwe hii leo ameanza ziara ya kikazi kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika Mkoa wa Singida.
Rc Mtigumwe ameanza ziara yake hiyo katika Halmashauri ya Itigi, iliyopo katika Wilaya ya Manyoni ambapo atatembelea kata zote za halmashauri hiyo.
Pamoja na kutambua kero za wananchi na mambo mengine pia Mkuu huyo wa Mkoa wa Singida anatumia mikutano hiyo maalumu kwa ajili ya kufahamiana na wanachi ikiwa ni pamoja kusikiliza kero zao ambazo zimewasua kwa miaka mingi bila kupatiwa ufumbuzi.
Mtigumwe akiwa katika Kijiji cha Doroto amehimiza zaidi wananchi kuandaa vyema mashaba yao na kuzingatia kilimo chenye kustahimili ukame kwani kuna mabadiliko makubwa ya tabia nchi jambo ambalo limepelekea kuchelewa kuanza kwa mvua.
Mhe Mtigumwe amewaagiza maafisa kilimo wa Kata na Wilaya zote za Mkoa wa Singida kutokaa ofisini kipindi hiki cha msimu wa kilimo badala yake kwenda mashambani kuwasaidia wananchi mbinu bora za kilimo sambamba na kuwasaidia namna bora ua kuandaa mashamba.
Sambamba nAa hayo pia amewasisitiza wananchi kuzingatia maelekezo watakayopatiwa na Maafisa kilimo ili kuwa na uhakika wa kuvuna mazao mengi zaidi kwa kilimo chenye tija.
Katika ziara yake Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe ameambatana na Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Singida.
0 comments: