POLISI KUMCHUNGUZA NETANYAHU KWA KASFA YA UNUNUZI WA NYAMBIZI
Posted by khamisimussa77@gmail.com at 7:45 AM
Mwanasheria Mkuu wa utawala haramu wa Israel
ametoa agizo la kuchunguzwa Waziri Mkuu wa utawala huo wa Kizayuni,
Benjamin Netanyahu, anayeandamwa na kashfa ya ununuzi wa nyambizi kutoka
Ujerumani.
Avichai Mandelblit, Mwanasheria Mkuu wa Israel amesema
'ushahidi mpya' uliojitokeza katika kesi ya Avriel Bar-Yosef, aliyekuwa
mkuu wa Baraza la Usalama la utawala huo ghasibu umeonyesha kwamba
kulikuwepo na mkinzano mkubwa wa maslahi katika ununuzi wa nyambizi
hizo.
Bar-Yosef alikamatwa mapema mwezi huu na kupandishwa kizimbani akikabiliwa na shitaka la ufisadi na kupokea rushwa.
Televisheni ya Kizayuni ya Channel 10 imetangaza kuwa ushahidi wa
baruapepe ya David Shimron, wakili na mpambe wa karibu wa Netanyahu
umefichua kuwa Shimon alitumia ushawishi wake kulifanya shirika la
ThyssenKrupp la Ujerumani lishinde kandarasi ya kuizuia Israel nyambizi
tatu.
Mwezi Julai mwaka huu, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Israel ilisema
ripoti ya uchunguzi wa madai mengine ya ufisadi dhidi ya Netanyahu
itawekwa wazi karibuni, kukiwemo kupokea fedha katika njia zisizoeleweka
baada ya kuhifadhi kiti chake katika uchaguzi wa mwaka 2009.
Inaarifiwa kuwa, mbali na madai ya usafishaji wa fedha, moja ya
tuhuma kuu zinazomuandama Netanyahu ni kupokea rushwa kutoka kwa
bilionea mmoja wa Ufaransa kwa jina la Arno Mimran ambaye anakabiliwa na
kashfa ya kufanya udanganyifu katika masuala ya kiuchumi huko Ufaransa.
Mahakama hiyo ilimhukumu Mfaransa huyo miaka minane jela au faini ya
yuro milioni moja. Mimran alipatikana na hatia ya kufanya uharibifu
mkubwa wa kiuchumi wenye thamani ya dola bilioni moja, kati ya mwaka
2008 na 2009 katika moja ya kesi dhidi yake
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: