Thursday, November 24, 2016

POLISI KUMCHUNGUZA NETANYAHU KWA KASFA YA UNUNUZI WA NYAMBIZI

Mwanasheria Mkuu wa utawala haramu wa Israel ametoa agizo la kuchunguzwa Waziri Mkuu wa utawala huo wa Kizayuni, Benjamin Netanyahu, anayeandamwa na kashfa ya ununuzi wa nyambizi kutoka Ujerumani.
Avichai Mandelblit, Mwanasheria Mkuu wa Israel amesema 'ushahidi mpya' uliojitokeza katika kesi ya Avriel Bar-Yosef, aliyekuwa mkuu wa Baraza la Usalama la utawala huo ghasibu umeonyesha kwamba kulikuwepo na mkinzano mkubwa wa maslahi katika ununuzi wa nyambizi hizo.
Bar-Yosef alikamatwa mapema mwezi huu na kupandishwa kizimbani akikabiliwa na shitaka la ufisadi na kupokea rushwa.
Nyambizi
Televisheni ya Kizayuni ya Channel 10 imetangaza kuwa ushahidi wa baruapepe ya David Shimron, wakili na mpambe wa karibu wa Netanyahu umefichua kuwa Shimon alitumia ushawishi wake kulifanya shirika la ThyssenKrupp la Ujerumani lishinde kandarasi ya kuizuia Israel nyambizi tatu.
Mwezi Julai mwaka huu, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Israel ilisema ripoti ya uchunguzi wa madai mengine ya ufisadi dhidi ya Netanyahu itawekwa wazi karibuni, kukiwemo kupokea fedha katika njia zisizoeleweka baada ya kuhifadhi kiti chake katika uchaguzi wa mwaka 2009.
Inaarifiwa kuwa, mbali na madai ya usafishaji wa fedha, moja ya tuhuma kuu zinazomuandama Netanyahu ni kupokea rushwa kutoka kwa bilionea mmoja wa Ufaransa kwa jina la Arno Mimran ambaye anakabiliwa na kashfa ya kufanya udanganyifu katika masuala ya kiuchumi huko Ufaransa.
Mahakama hiyo ilimhukumu Mfaransa huyo miaka minane jela au faini ya yuro milioni moja. Mimran alipatikana na hatia ya kufanya uharibifu mkubwa wa kiuchumi wenye thamani ya dola bilioni moja, kati ya mwaka 2008 na 2009 katika moja ya kesi dhidi yake

No comments:

Post a Comment