Latest Articles

WATENDAJI WA UCHAGUZI WAKUMBUSHWA KUSHIRIKIANA NA WANAHABARI

  Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe.Magdalena Rwebangira amewakumbusha watendaji wa Uchaguzi ngazi ya Mkoa na Jimbo kushirikiana na Wanahabari ili wananchi waweze kufahamu mambo mbalimbali yahusuyo Uchaguzi.


Wito huo ameutoa leo alipokuwa akifunga mafunzo ya siku tatu kwa watendaji wa Uchaguzi ngazi ya Mkoa na Jimbo yaliyofanyika kwa siku tatu katika Kituo cha Tabora yaliyojumuisha watendaji kutoa Mikoa wa Tabora na Kigoma.

"Katika utekelezaji wa majukumu yenu, mtapaswa kutoa taarifa mbalimbali kwenye vyombo vya habari ili kuwajulisha wananchi na wadau wa Uchaguzi mambo mbalimbali yanayohusu Uchaguzi" alisema Mhe.Rwebangira.

Aidha Mhe.Rwebangira amewasisitiza watendaji hao kuhakikisha wanatunza rasilimali vifaa vya Uchaguzi watavyovipokea kwaajili ya Uchaguzi sambamba na kuhakikisha wanafuata Sheria, kanuni na miongozo kutoka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ili wakatimizie jukumu la usimamizi wa Uchaguzi kwa weledi.

Mafunzo haya ya siku tatu yenye lengo la kuwajengea uwezo watendaji wa Uchaguzi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 yamekamilika leo tarehe 17 Julai, 2025.
read more

BENK YA NMB NA OFISI YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI ZAIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA UTOAJI WA HUDUMA KWA WATEJA

  Ujumbe kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (OAG) ukiongozwa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Samwel M. Maneno, umetembelea makao makuu ya Benki ya NMB na kufanya kikao na uongozi wa benki hiyo ukiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu, Bi. Ruth Zaipuna.

Kikao hicho kilichofanyika katika makao makuu ya NMB jijini Dar es Salaam, kikilenga kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi hizo mbili, hususan katika kubadilishana uzoefu na mbinu bora za utoaji wa huduma kwa wateja.

Ujumbe wa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali uliambatana na viongozi mbalimbali wakiwemo Bw. Ipyana Mlilo – Mkurugenzi Msaidizi Uratibu, Bi. Leila Muhaji – Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Bw. Juma Mziray – Afisa TEHAMA Mwandamizi, na Bw. Nyamhanga Nyamhanga – Wakili wa Serikali.

Kupitia mazungumzo hayo, pande zote mbili zilitambua umuhimu wa ushirikiano wa karibu kati ya sekta ya umma na binafsi katika kukuza ufanisi wa utoaji huduma na kuleta maendeleo jumuishi.

Kikao hicho ni sehemu ya juhudi za pamoja za kuimarisha utawala bora na kuhimiza matumizi ya teknolojia katika utoaji wa huduma bora kwa wananchi. 




read more

MISS WORLD NA MISS AFRICA WATEMBELEA WODI YA NJITI PAMOJA NA DORIS MOLLEL FOUNDATION

 Wameguswa na kazi kubwa inayofanywa kuwahudumia watoto njiti na wamepongeza juhudi zinazofanyika na kuahidi kuchangia vifaa tiba na kusaidia hospitali nyingine zaidi kwenye maeneo yasiyofikiwa.

read more

MENEJIMENTI ZA INEC NA ZEC ZAKUTANA ZANZIBAR

 Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ndg. Ramadhani Kailima na Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Ndg. Thabit Idarus Faina (kulia) wakiongoza kikao cha pamoja cha wajumbe wa menejimenti baina ya Tume hizo mbili leo Julai 17,2025 kilichokutana katika Ofisi za ZEC Mjini Unguja Zanzibar. Kikao hicho ni maandalizi kuelekea kikao cha pamoja cha INEC na ZEC kitakachokutana hivi karibuni kisiwani humo. (Picha na INEC).

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ndg. Ramadhani Kailima na Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Ndg. Thabit Idarus Faina wakiongoza kikao cha pamoja cha wajumbe wa menejimenti baina ya Tume hizo mbili leo Julai 17,2025 kilichokutana katika Ofisi za ZEC Mjini Unguja Zanzibar. Kikao hicho ni maandalizi kuelekea kikao cha pamoja cha INEC na ZEC kitakachokutana hivi karibuni Kisiwani humo. (Picha na INEC).
read more

WANAFUNZI KUTOKA MAREKANI WAPATA UZOEFU HOSPITALI YA JK KIGAMBONI

    Dkt. Telesphory Kyaruzi akionyesha moja ya vifaa aliyopokea kutoka kwa Wamarekani waliofika katika Hospitali ya JK iliyopo Kigamboni Dar es Salaam mara baada ya kumaliza mafunzo ya kubadilishana  uzoefu kwa muda wa siku nne.  Juni 13, 2025.  .
 
    Dkt. Amani Msemakeili akizungumza na mgonjwa na kutoa maelezo kwa wanafunzi wa Chuo cha Merika katika Programu ya Afya ya Umma 2025 walikuwa wanafunzi 28 na Maprofesa 2 kutoka Marekani waliofika JK Hospital iliopo Kigamboni kubadiishana uzoefu kwa muda wa siku nne.

   Mtaalamu wa Wauguzi kutoka Chuo Kikuu cha Kentucky Marekani Prof. Dkt. Beth Killian akitoa elimu kwa wanafunzi wauguzi kutoka Marekani waliofika katika hospitali ya JK iliyopo Kigamboni Dar es Salaam.


   Mwanafunzi wa Uuguzi kutoka Marekani Gdney Deatherage akimpatia mtoto chanjo ya 
   Mtaalamu wa Wauguzi kutoka Chuo Kikuu cha Kentucky Marekani Prof. Dkt. Beth Killian akimkabidhi kifaa. Dkt. Telesphory Kyaruzi mara baada ya kumaliza mafunzo ya kubadilishana  uzoefu kwa muda wa siku nne katika hospitali ya JK iliyopo Kigamboni Dar es Salaam.
    Mkurugenzi wa Programu ya KIIS Prof.  Wiliam Mkanta akitoa historia fupi kwa Mkurugenzi Hospitali ya JK.  Dkt. Telesphory Kyaruzi juu ya ujio wa Wamarekani toka mwaka 2011 hadi 2025 wapatao Wamarekani 300 kwa vipindi tofautitofauti wamefika hospitalini hapo.

Mkurugenzi Hospitali ya JK akiwa katika picha ya pamoja na Wamarekani mara baada ya kubadilishana  uzoefu kwa muda wa siku nne.

 

 NA KHAMISI MUSSA, DAR ES SALAAM.

Zaidi ya wanazfunzi 300 kutoka nchini Marekani kubadilishana uzoefu na kuongeza ujuzi kwenye huduma za afya na wataalamu wa Hospitali ya JK iliyopo Kigamboni Dar es Salaam ikiwa ni mara ya 15 tangu waanze kubadilishana ujuzi huo.

Mafunzo hayo yameanza leo Juni 13, 2025 katika Hospitali ya JK ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo Dkt. Telesphory Kyaruzi amewashukuru Wamarekani kwakuja kubadilishana ujuzi na wataalamu wa afya wa hospitali hiyo.

“Ninashukuru sana kwa Ujio wa Marafiki zetu kutoka Nchini Marekani katika vyuo mbalimbai ambapo wamekuja maprofesa, maktari, walimu na wauguzi wanafunzi kimsingi wamekuja kujifunza kwa upande wetu wa Afrika lakini kama hospitali ya JK ambayo ni hopspitali binafsi wametusaidia kuleta uzoefu wa utaalamu na vifaa vingi tumepokea na ni vya kisasa vya Upasuaji.” Amesema Dkt. Kyaruzi.

Dkt. Kyaruzi ameeleza mafanikio ya utoaji huduma za afya katika hospitali hiyo, zikiwa ni huduma bora za kiafya kwa wakazi wa kigamboni na Dar es Salaam kwa ujumla kutokana na vifaa walivyopokea kutoka Marekani.

“Vifaa vitasaidia kuongeza utoaji wa huduma na kuboresha huduma katika Hospitali yetu ya JK, Ninaamini wananchi wengi watapata huduma bora, tunaomba mahusiano yetu yaendelee kudumu na yaendelee kuwepo mwaka hadi mwaka ili tuendelee kuwasaidia wananchi wetu watanzania wanaohitaji huduma bora za afya.” Ameeleza Dkt. Kyaruzi.

Vile vile, Dkt. Kyaruzi amewashukuru wote wataalamu wa afya wa hospitali hiyo na wale kutoka nchini Marekeni kwa moyo wao wa kujifunza na kubadilishana ujuzi ili waendelee kutoa huduma bora za kiafya kwa wananchi.

‘’Kipekee ninawashukuru wote kwa kuweza kufika katika kubadilishana uzoefu na ninaimani kwa mjumuiko huu wa wataalamu kutoka taasisi na hospitali mbalimbali tutahakikisha huduma hizi tunazitoa kwa viwango vya hali ya juu zaidi”. amesema Dkt. Kyaruzi

Mkurugenzi wa Programu ya KIIS Prof.  Wiliam Mkanta amesema toka mwaka 2011 kila mwaka wanakuja wanafunzi tofauti tofauti wakiwa ni wauguzi, madaktari, na wale wa elimu ya Afya

“Wote wanahusiana na masuala ya afya na progamu hii huleta wanafunzi kutoka vyuo vikuu vya Marekani na ni wanafunzi kutoka katika fani ya afya ya jamii, ambao huja kwaajili ya masomo ya muda mfupi kuanzia mwezi wa sita ,saba na nane” Amesema Prof. Mkanta.

Prof. Mkanta ameongeza kuwa wakati wanafunzi hao wanakuja kujifunza upenda kutembelea maeneo tofauti tofauti hapa nchini nan chi zingine za Afrika hii pia inakuza utalii.

“Wanaokuja Nchini Tanzania na tunakuwa tunakaa wiki nne zinakuwa za mafunzo ya vitendo nakutembelea maeneo ambayo ni maarufu ya nchini na kama sasa hivi tupo Mwanza kujifunza tamaduni za watu wa Tanzania, pamoja na nyanja za kiafya, huduma zakijamii kwa kuifata Jamii kwenye maeneo yao” Ameongeza Prof. Makanta. 

Naye, Ritha Raymondi amabaye ni mzazi amesema kuwa alipompeleka mtoto wake kliniki katika hospitali ya JK alikutana na wanafunzi kutoka vyuo tofauti nchini Marekani waliokuwa katika program ya afya ya umma mwaka 2025 na kufanikiwa kujua hali ya mtoto na kupata maelezo ya kina juu ya mwenendo wa afya ya mtoto wake aliyekuwa na areji.

“Kwa kweli nimefurahi sana ujio wa hawa ndugu zetu kutoka Nchini Marekani na wamesaidia kujua tatizo la mwanagu ambaye alikuwa akisumbuliwa na Areji na wamenielezea kiundani sana, sababu za hiyo areji na namna ya kuitibu, kwakweli ujio wao unafaida sana sana sana, tunashukuru sana kwa ujio wao na kuiomba JK Hospitali isiishi hapa na iweze kuwaleta tena mara kwa mara asanteni sana” Amesema Ritha.

 

 

read more

TANZIA: MHE.RAIS SAMIA ATUMA SALAMU ZA POLE KIFO CHA PAPA FRANCIS


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole  (kwa niaba ya Watanzania) kufuatia taarifa ya kifo cha Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis  kilichotokea jumatatu ya pasaka tarehe 21,  April 2025. 

 Rais Samia ameandika  "Nimesikitishwa na taarifa ya kifo cha Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francisko. Katika kipindi chote cha miaka 12 akiwa Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francisko ameishi maisha yake kama mwalimu na kiongozi aliyefundisha na kuhimiza ustawi na maendeleo ya watu pamoja na kudumisha amani"

Dkt Samia  ameongeza
"Kwa niaba ya Serikali na Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ninatuma salamu za pole kwa waumini wote wa Kanisa Katoliki hapa nchini na duniani kote."

Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema Peponi. 

Amiina

read more

PAC YARIDHISHWA NA MAENDELEO YA MIRADI NELSON MANDELA

  Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe.Japhet Hasunga akizungumza wakati wa kikao mara baada ya kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa mabweni ya wanafunzi ( Hosteli) unaotekelezwa na Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Machi 25,2025 Kampasi ya Tengeru jijini Arusha.


...........

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imeipongeza Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) kwa matumizi sahihi ya FORCE akaunti yenye kuleta tija kwenye miradi mbalimbali nchini.

Pongezi hizo zilitolewa Machi 24, 2025 Jijini Arusha, na Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Japhet Hasunga mara baada ya kamati kukagua ujenzi wa mradi wa mabweni ya wanafunzi.

Aidha Kamati hiyo pia imepongeza NM-AIST kwa kuzalisha bunifu110 huku bunifu 22 zikipata hati miliki na kusisitiza bunifu hizo kubishwarishwa ili kuleta tija zaidi katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) pamoja na nchi nyingine zinazofika kujifunza kuhusu masuala ya bunifu.

Vilevile, kamati hiyo imeiagiza NM-AIST kuhakikisha inaendelea kufanya bunifu ikiwemo kuzisajili kwa kupata hati miliki ili kuepuka Teknolojia hizo kuibiwa zinazogunduliwa na wabunifu.

Mhe. Hasunga alisema, endapo bunifu hizo zikitoa matokeo ya bunifu upatikanaji wa hati miliki utasaidia wabunifu kutoibiwa mawazo yao sanjari na kuziuza ili wahusika waweze kupata kipato na kujikwamua kiuchumi.

"Bunifu zenu hakikisheni zinaingia sokoni lakini pia tunawapongeza kwa muonekano wa thamani halisi ya fedha za mradi huu ikiwemo matumizi ya force akaunti" Mhe.Hasunga

Akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, Profesa Maulilio Kipanyula ambaye ni Makamu Mkuu wa Taasisi hiyo, alisema jengo hilo la mabweni pacha matatu lina thamani ya sh bilioni 6.109 likiwa na vyumba 184 ambapo vyumba 160 ni vya kujitosheleza na vyumba 20 ni vya mfano wa apatimenti kwa ajili ya kinamama wenye watoto pamoja na vyumba vinne kwa ajili ya matumizi mtambuka.

Prof Kipanyula alisema mradi huo wa mabweni pacha matatu umefikia asilimia 74 na unatarajia kukamilika Juni 30, 2025 ambapo lengo kuu la taasisi hiyo, ni kutoa mafunzo ikiwemo utafiti ambapo hadi sasa kuna wanafunzi kutoka nchi 16 tofauti za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Kusini mwa j Nangwa la Sahara wanasoma katika taasisi hiyo.

Kuhusu ufafanuzi wa bunifu ya inzi lishe , Naibu Makamu Mkuu ,Taaluma,Utafiti na Ubunifu Profesa Anthony Mshandete alisema inzi chuma huyo ni nzi asiyeambukiza na hutaga mayai zaidi ya 500 ambayo huzilisha funza lishe kwa ajili ya kutengeneze chakula cha mifugo na mbolea.

Alisema uzalishaji wake unajali mazingira ikiwemo uchafu unaozalishwa na zao la mkonge kubuniwa na hatimaye kupata chakula hicho cha mifugo na mbolea rafiki kwa wakulima.

Awali wabunge wa kamati hiyo akiwemo, Mhe. Isack Kamwelwe mbunge wa Katavi na Mhe. Condester Sichalwe kutoka Momba walipongeza taasisi hiyo, kwa kufanya bunifu mbalimbali na ufanisi wa mradi wa bweni hilo ikiwemo mandhari nzuri ya taasisi hiyo.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe.Japhet Hasunga akizungumza wakati wa kikao mara baada ya kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa mabweni ya wanafunzi ( Hosteli) unaotekelezwa na Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Machi 25,2025 Kampasi ya Tengeru jijini Arusha.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo akiongea jambo wakati wa kikao na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali ( PAC) iliyofanya ziara ya kutembelea na kukagua Mradi wa Ujenzi wa Bweni la Wanafunzi katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Machi 25,2025 Kampasi ya Tengeru jijini Arusha.
Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Balozi Maimuna Tarish akizungumza wakati wa kikao na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) waliofanya ziara ya kukagua na kutembelea mradi wa ujenzi wa Bweni la Wanafunzi wa Taasisi hiyo, Machi 25,2025 Kampasi ya Tengeru jijini Arusha. 
Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof Maulilio Kipanyula akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi wa mabweni ya wanafunzi kwa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) , Machi 25,2025 kampasi ya Tengeru Jijini Arusha.
 Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe.Japhet Hasunga ( katikati) akiongoza wajumbe wa kamati ya Bunge katika kukagua mradi wa ujenzi wa bweni la wanafunzi katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Machi 25,2025 Kampasi ya Tengeru jijini Arusha.
 Mwenyekiti wa Mradi wa Ujenzi wa Bweni la Wanafunzi Prof. Kelvin Mtei ( katikati) akifafanua jambo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali ( PAC) walipotembelea mradi huo katikati Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Machi 25,2025 Kampasi ya Tengeru jijini Arusha.
 Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo akielezea maendeleo ya mradi wa ujenzi wa bweni la wanafunzi kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali ( PAC) iliyofanya ziara ya kutembelea na kukagua Mradi huo katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Machi 25,2025 Kampasi ya Tengeru jijini Arusha.
 Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakifuatilia wasilisho la taarifa ya utekelezaji wa mradi wa bweni la wanafunzi kutoka kwa Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof Maulilio Kipanyula ( hayupo katika picha) Machi 25,2025 Kampasi ya Tengeru jijini Arusha.
Wajumbe wa Menejimenti ya Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) wakiwa katika cha kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) mara baada ya ziara ya kukagua Mradi wa Ujenzi wa Bweni la Wanafunzi Machi 25,2025 Kampasi ya Tengeru jijini Arusha.
read more